Jumla ya ada ya kusoma degree ya udaktari katika chuo kikuu cha Kairuki kwa miaka yote mitano ni milioni 32, swali langu is it worth it ?

Jumla ya ada ya kusoma degree ya udaktari katika chuo kikuu cha Kairuki kwa miaka yote mitano ni milioni 32, swali langu is it worth it ?

View attachment 2893856

Jumla ya Ada kwa Miaka yote mitano: 32,769,250​

Tukumbuke hiyo ni ada tu haijajumlisha gharama za chakula, hostel, stationary, na mengineyo

Swali langu kwa mliosoma ama kusomesha watoto wenu degree ya udaktari Kairuki Is it worth it ?
Digrii ya udaktari ni muhimu sana. Madaktari wazee wanastaafu na wengine wanakufa kwahiyo damu changa inahitajika. Kama sijakosea hiyo gharama si halisia, bado serikali inawekeza katika kusomesha madaktari, vyuo vinapata misaada toka serikalini. Fani ya udaktari ni wito wa kutumikia na kuponya binadamu wengine si fani ya kufikiria kurudisha uwekezaji uliofanya. Serikali isipotoa ruzuku kwa vyuo vya Udaktari utakuta madaktari wote watakuwa wanatoka kwenye familia za kitajiri . Fani ya udaktari ni fani ambayo katika nchi kama Marekani na Uingereza ndiyo inayo ongoza kwa kulipa mishahara mizuri sana. Hapa Tz madaktari wanabangaiza pesa kwa kufanya kazi muda mrefu katika zaidi ya hospitali moja. Tunatakiwa kuwatia moyo wazazi wenye uwezo waendelee kusaidia serikali katika kusomesha madaktari wengi wenye wito kamili wa kutumikia na siyo kwaajili " status symbol "
 
Hapana Mkuu Daktari Bingwa Anaanza na Mshahara wa TGHS G ambao ni sawa na Tsh 2,270,000/ Basic..
Labda kama ni private ila kwa serikali huo ndio mshahara..
Ukiona watu wanalia Mtuhurumie..😀
Kwa kweli heshima Kwa madaktari kama bingwa analipwa hivyo asiye bingwa itakuaje na mbaya zaidi kazi za madaktari kosa dogo la kibinadamu linaleta madhara makubwa na wananchi na wanasiasa hatutambui bahati mbaya, kinachotokea ni kulaumu tu na kuwalaani.

Wakati sie wengine fani zetu tunaweza kukosea tena sana na madhara hayaonekani moja Kwa moja ila indirectly Yana athiri jamii kubwa inaonekana kawaida na tunatatua Kwa kukaa vikao na yanaisha
 
Ngoja niishie hapa
Yaani mtu asome masomo magumu advance, aende university akeshe miaka 5 , akeshe kujitolea mwaka mmoja, atafute kazi, afanye kazi, atafute elimu tena Ili aitwe bingwa then analipwa milioni 2.
Mimi sifanyi huo ujinga
 
Back
Top Bottom