Uchaguzi 2020 Jumuiya ya Madola yatoa taarifa rasmi kusikitishwa na yaliyotokea Tanzania kipindi cha uchaguzi mkuu ikiwemo udanganyifu na mauaji

Uchaguzi 2020 Jumuiya ya Madola yatoa taarifa rasmi kusikitishwa na yaliyotokea Tanzania kipindi cha uchaguzi mkuu ikiwemo udanganyifu na mauaji

Tanzania ya leo ukiwa mpinzani inabidi uwe kama digidigi maana unaweza kunyimwa haki zako za msingi.
 
Uhuru Kenyatta ndio atakapo aibika, mwanachama wa Common Wealth Countries halafu kajifanya kusifia na kumpongeza Mfalme kwa yaliofanyika.

Ndio watakapomuona kituko.
Rais Uhuru Kenyatta alipewa Tausi wetu tuliowatunza na kuwaenzi toka tupate Uhuru yeye na Museveni wakapewa bure bila ridhaa ya wananchi labda sasa anataka apewe tembo wetu maana kwao wamepungua sana kazi ya majangiri. Awamu hii itatuacha wananchi masikini wa kutupwa wa kila kitu!
 
Commonwealth with no common sense.. Suck it losers, hamna issue tena. Hamna taifa linalojielewa linalowajali siku hizi
 
Hawa kina Zitto na Lissu na watu wachache Sana wa chadema cjui kitu gani wanataka, hatuna tatizo Kama Ni kuiba hata mbowe anaibaga hela za chadema ni utamaduni wetu Ila Mambo yanaenda, so Magu kashinda kihalali plus na vikura kidogo vya kuchakachua kuwaondoa wabunge wapiga kelele.

Sisi watanzania Ni waangaliaji tunaenjoy Sana drama za siasa Ila kamwe hatushiriki kamwe, naawaambia tunapenda drama.
Watu hamuelewi kushinda Magu inaweza siyo tatizo lakini njia za ushindi wake pamoja na 99.999 ya wabunge wa chama chake hakuna binadamu mwenye akili zake anaweza sema kila jambo lilienda sawa.. Tuacheni ushabiki wa kuumiza matakwa ya wananchi, TZ ni yetu sote na kila mmoja anapaswa kutendewa haki, ndiyo maana ya uwepo wa chaguzi kama hizi...
 
Mbuzi wa kafara sijui atakuwa nani katika hili??
Mambo-now atasalimika kweli?

Tusubirie list ya mbuzi wa kafara! Atawachinjia baharini watu kadhaa..

Everyday is Saturday............................... 😎
 
......has strongly urged authorities to investigate allegations .....
Haya ni madai (taarifa isiyothibika bado), naona mleta mada kafanya conclusion zake mwenyewe , Tuelewe maana ya kuwa allegedly.
 
Yaani kuna watu wanajua demokrasia ni hadi ashinde mpinzani😅😅😅. Mara ooh tumekamata kura wakiambiwa wazipeleke zikachunguzwe na kulinganisha kama kweli ni sawa na zile za nec hawataki kupeleka! Basi tuonesheni huyo mtu mlie mkamata nazo oooh hatujui alipo! Basi hizo kura zina namba tusomeeni hizo namba ili tuangalie ni kutoka katika kitabu gani cha kura kati ya vilivyo gawanywa na nec oooh sisi hatutaki tunataka tu tuzichome moto! 🤣🤣🤣🤣🤣SI MKUBALI TU MMESHINDWA. Kura za mh. Magufuli zipo ndani ya boksi la kura na ndizo zilizo hesabiwa hizo za nje ni za kwenu njama yenu imeshtukiwa tafuteni pa kuzipeleka au kama kweli mnajiamini ni vidume chukueni sampuli japo kura 2 tu mpeleke mahakamani zikalinganishwe.

MAGUFULI4LIFE.

Kwa mahakama zipi na jeshi lipi la polisi upeleke ushahidi? Hizo mahakama zilizobambikia kesi ya uhujumu uchumi watu waliokamatwa wakiandamana kupinga genge la wahuni wa ccm, kwa kushirikiana na vyombo vya dola kunajisi uchaguzi? Hao polisi wanaosimama hadharani na kusema lazima ccm ishinde? Hao comonwealth sio wahuni au genge la wapora uchaguzi wa EA ndio maana wamesema ukweli mchungu.
 
Over and above, let's come to our senses....the election is over. We should not create dramas. We need the outside world to work with us, if we really need to pursue development agendas
 
View attachment 1618126View attachment 1618125
Ì
My Take
Pamoja na ukweli wa mambo yasiyo ya kawaida,ila ndugu zetu wa damu jumuia za Afrika zinasema mambo yalikuwa shwari.
Hao AU ndio baadhi yao walishuhudia uchaguzi.Jumuia ya madola wao wanarejea kwenye barua ya Beberu Amsterdam.Hakuna kitu hapo.Tunachotizama sasa ni Rais wetu wa Tanzania kuapishwa tarehe 5 mambo yaendelee mbele. Mmoja ameshaapishwa tayari.
Jumuiia ya madola tunaimani kwamba hawaungi mkono hujuma zilizotaka kufanywa.Tutahitaji msaada kwa mtu mwenye nia ya dhati na Tanzania lakini yule ambaye anasikia tu la kuambiwa na kuamini hapohapo bila kupata ukweli hatutaki msaada wake si wa mali wala wa hali.
 
Ukishaona kundi au mtu anapewa airtime na ccm, jua huyo Ni muhuni mwenzao katika kunajisi chaguzi za nchi. Ule upuuzi juzi kila mtu kajionea, na yote yale Ni maelekezo ya muhuni mmoja mlevi wa madaraka.
Hivi wewe dogo Lisu alisema watu wakishapiga kura wakae mita mia mbili kulinda kura na mh. Magufuli rais wetu alituambia tukisha piga kura turudi nyumbani na ndicho kilichotokea mpaka hapo huoni wengi tuliopiga kura tuliungana rais wetu? Halafu wewe ulitegemea muujiza gani wa Lisu kushinda kwenye boksi la kura?

2/3 ya wapiga kura hawakujitokeza kwenye huo ushenzi uitwao uchaguzi. Na bado kwenye hiyo 1/3 hamkupata kura zote. Sina tatizo la Lisu kushindwa iwapo angeshindwa kwa uhalali. Sio kwa hizo kura zilizokuwa zinasambazwa na vyombo vya dola. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Yaani kuna watu wanajua demokrasia ni hadi ashinde mpinzani😅😅😅. Mara ooh tumekamata kura wakiambiwa wazipeleke zikachunguzwe na kulinganisha kama kweli ni sawa na zile za nec hawataki kupeleka! Basi tuonesheni huyo mtu mlie mkamata nazo oooh hatujui alipo! Basi hizo kura zina namba tusomeeni hizo namba ili tuangalie ni kutoka katika kitabu gani cha kura kati ya vilivyo gawanywa na nec oooh sisi hatutaki tunataka tu tuzichome moto! 🤣🤣🤣🤣🤣SI MKUBALI TU MMESHINDWA. Kura za mh. Magufuli zipo ndani ya boksi la kura na ndizo zilizo hesabiwa hizo za nje ni za kwenu njama yenu imeshtukiwa tafuteni pa kuzipeleka au kama kweli mnajiamini ni vidume chukueni sampuli japo kura 2 tu mpeleke mahakamani zikalinganishwe.

MAGUFULI4LIFE.
Unajikuta anajua sana kumbe ulichoandika ni utumbo mtup
 
Uhuru Kenyatta ndio tuseme ile "HONGO ULIOPEWA YA NDEGE TAUSI" imekufanya usifie uchaguzi wa dhuluma???

Ndio atakapo aibika, mwanachama wa Common Wealth Countries halafu kajifanya kusifia na kumpongeza Mfalme kwa yaliofanyika. Wakati viongozi wa CWC wamesikitishwa na uchaguzi huo.

Ndio watakapomuona kituko Uhuru Kenyata.
Sio Tausi, alivopelekshwa mchaka mchaka hivi juzi hapa kwenye kususiana alishika adabu. Kakaa na kuwaza akiwazua akaona aweke maslahi ya taifa lake kwanza kabla ya ukweli halisi
 
Hawa bado hawajanishawishi.

Huwezi kumpa mamlaka ya ku restore peace mtu aliye ondoa peace.

Wawaondoe walio baka demokrasia kwanza.
 
Inamaana viongozi wa Afrika Mashariki ná viongozi wa SADC hawakuyaona haya?
Wanamtegemea Katibu Mtendaji wa SADC na viongozi wengine kama wa Zimbabwe Kuwapa matumaini ya muda mfupi serikali ya CCM Mpya awamu ya 6 . Katibu Mtendaji wa SADC ni mtanzania rejea hapa Katibu Mkuu wa SADC :

KUTOKA KUMBUKUMBU ZA INTANETI
Leo Jumatano Februari 5, 2020 Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya mazungumzo Ikulu ya Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (Sadc), Dk Stergomena Tax
 
They are people of the same club
 
Back
Top Bottom