Jumuiya ya umoja wa mabaharia Tanzania yampongeza waziri Kombo kwa kazi nzuri ya kuhudumia mabaharia wa Tanzania nje ya nchi

Jumuiya ya umoja wa mabaharia Tanzania yampongeza waziri Kombo kwa kazi nzuri ya kuhudumia mabaharia wa Tanzania nje ya nchi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
JUMUIYA YA UMOJA WA MABAHARIA TANZANIA YAMPONGEZA WAZIRI KOMBO KWA KAZI NZURI YA KUHUDUMIA MABAHARIA WA TANZANIA NJE YA NCHI

Jumuiya ya Umoja wa Mabaharia Tanzania imempongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuhakikisha mabaharia wa Tanzania wanapata huduma bora nje ya nchi.

Halfa fupi ya kumpongeza Waziri Kombo ilifanyika tarehe 24 Desemba 2024, katika ukumbi wa Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI), ambapo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Bwana Juma Simba Gaddaf, alimkabidhi Mhe. Waziri Cheti Maalum cha Heshima kutambua mchango wake katika kutetea, kulinda, na kuendeleza haki na ustawi wa mabaharia wa Tanzania nje ya nchi.
Bwana Gaddaf alieleza kuwa, akiwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Kombo alijitolea kuwafuatilia mabaharia wa Kitanzania na kuhakikisha wanapata huduma bora.

Alijishusha na kufuatilia changamoto za mabaharia kwa karibu, hatua iliyomwezesha kubuni mikakati madhubuti ya kuzitatua, ikiwemo upatikanaji wa Hati ya Kusafiria (Passport), ambayo ni nyenzo muhimu wakati wa kutafuta ajira ndani na nje ya nchi.

“Mhe. Balozi Kombo ameacha alama nzuri nchini Italia kwa kujenga mahusiano bora kati ya mabaharia na ubalozi, pamoja na nchi zinazohudumiwa na ubalozi huo, ambapo pia alisistiza umuhimu wa kukuza diplomasia ya Tanzania katika mataifa ya nje,” aliongeza Bwana Gaddaf.

Akizungumza baada ya kupokea cheti maalum cha heshima, Mhe. Balozi Kombo aliishukuru Jumuiya hiyo ya Mabaharia kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza mabaharia na aliwahaidi kuimarisha ushirikiano nao kwa upana zaidi, hata katika nafasi yake ya Uwaziri.

Halfa hiyo ya salaam za pongezi ilitanguliwa na hafla nyingine fupi iliyofanywa na Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam, ambapo Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tumaini Shabani Gurumo, alimkabidhi Mhe. Balozi Kombo Tuzo Maalum ya kutambua mchango wake katika kuendeleza elimu na mafunzo ya ubaharia nchini.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mhe. Kombo aliishauri menejimenti ya DMI kuwatumia kikamilifu mabaharia wastaafu kupitia programu za mafunzo, ili watoe elimu ya kitaaluma na uzoefu kwa vijana hatimaye kuwajengea uwezo wa kushindania fursa zitakazojitokeza zikiwemo Kazi za Kimataifa.
 

Attachments

  • IMG-20241226-WA0140(1).jpg
    IMG-20241226-WA0140(1).jpg
    275.9 KB · Views: 6
Back
Top Bottom