Nina visa vingi, ila hiki ndo kinanipaga hype mnoo.
Primary, toka drs la 1 had la 7, nilikua nashika nafas ya kwanza tu.
Sasa tukiwa drs la 5 walihamia wanafunzi 2 mtu na dogo ake wote tulisoma drs 1, sasa kunae m1 huko walikotoka ndo alikua anashika hilo drs lao,
Kuja pale kukuta mie ndo kipanga wa drs, asianze kuhamaki, mara oooh haiwezekan, anajifaragua eti kuanzia sahiv class ntashikilia mie, yaan huyu ndo awe genius wa drs sikubali, na vile eglish aliiweza kdg, aliona kamaliza, bas coca mie zangu kimya nione huyo mgeni ana jambo lipi la kutisha,
Kuja mtihani, matokeo yalivyotoka, alinipita somo la English tyuuh mengine yote nilimtupilia kulee. Nikaibuka zangu kidedea, toka pale ikaanza vita baina yake na yangu, nlikua nampita tUuh, kubwa zaidi, ni NECTA drs la 7, dadekii nikaibuka zangu na marks 223, yeye 197, mwenzake nikachaguliwa shule ya bweni kitaifa, yeye ya kata.
😂😂😂😂😂😂 nilimyoosha yule kijana, na hanisahau, alikua ananidharau kwa jinsi nilivyo, asijue akili na ufahamu nimebarikiwa.