Juventus Special Thread

Juventus Special Thread

Washabiki wa Juventus napenda kujua toka kwenu, hivi hili jina la utani la Kibibi kizee (the old lady) lilikujaje kwa hii timu!?
 
Always expect the unexpected MosDef

Barca WASIJIDANGANYE kama wanaenda Berlin kupiga tu gwaride na kurudi na kombe!

Kambale wavumilivu wa Turin chini ya mkongwe Pirlo wanaweza mfunga team yeyote duniani kwa sasa

Hongereni sana wana Juventus!Soka la dunia hii sasa limerudi nyumbani!Tunamsubiri Liverpool nae awe sawa tukumbushie ya Belgium 1986
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
ImageUploadedByJamiiForums1431584128.527587.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1431584180.593841.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1431584379.011275.jpg
 
Mourinho naye alikua chini ya uvungu presha ilimshika ya miguu. Hahahahaaa nimemuona Mourinho anapita kimya kwa LIKE

Buluda huyu hajawahi kukimbia from a battle, toka tutimbe semi finals nimekua nawaacha mamluki nao wacomment humu na me nipate muda mzuri wa kuangalia game bila kubofyabofya vitufe, ndio maana mlikua mnakula likes tu
Mnataka mjadala? now is the time
 
Last edited by a moderator:
ImageUploadedByJamiiForums1431584879.576642.jpg kuna Ronaldo mmoko tu, not this copy cat mazafarting sh!t
Cc: Janjaweed
 
Last edited by a moderator:
Hongereni sn kwa kuingia fainali uzembe Wa Madrid ndio umewapa nafasi.

Umeumia sana Bianconeri kutimba fainali eeh?
Vua hiyo miwani ya chuki halafu kaangalie replays za both legs then utajua hatupo hapa by chance ila ni mipango thabiti ya Allegri na team yenye spirit ya ukweli ya kibuluda

#FinoAllaFinale
 
Kiukweli nimefurahi sana kuwaona Juve wakiingia Final, jana wakati narudi nyumbani nikakutana na vijana maeneo flani wakiwa wanajadili mpira, nikawaambia mechi ya leo ni ngumu sana na Real hawezi mzuia Juve asipate goal pale Bernabeu. Penat waliyopewa ilinikera sana, na Ronaldo haya ndio magoli yake kwa Penalty.
Hongereni sana tena sana kwa Final kwa mbinde, huyu Pogba huyuuu!!! Mtoto hatari sana huyu ana Confidence kubwa sana yaani kama Messi vile au Xavi enzi zake, ningependa kumuona akienda kucheza Barcelona mwaka 2016. Safi sana Pogba.
Kwa kumalizia ni kuwaambia tu kwamba, Kombe la UEFA CHAMPIONS LEAGUE HAMTABEBA, hili kombe linaenda kule katalunya CAMP NOU. Kuanzia sasa jipangeni mnavyoweza ili muweze kuwakabili Neymar, Suarez na Messi. Hakika Barcelona hawataacha mbebe hili Kombe.
 
Final Berlin ni Juventus v Chelsea.
 
hakuna kitachotuzuia kubeba ndoo labda fainali ingekuwa home and away kidogo mechi ingetiwa ugumu na marefa ila kwa kuwa fainali ni moja tu kilichomkuta dada mtu real madrid na mdogo wake wa kike barcelona kitamkuta hikohiko...ni mwendo wa kuwazimia fegi wale vigoli wao madoido kina messi.....

signora omicidi!
 
Ahsante sana Aleyn, huyo wannabe Ronaldo ushuzi tu, kazoea vya kutengewa na ile penati ya uongo ya jana iliniboa kweli ila mwisho wa siku waliishia kuwamwagia mabuluda mauno ya kufa mtu
Berlin tuna kibarua kimoja tu, kinaitwa Lionel Messi, tukikikamata hiki kikilikuu kazi kushney, Suarez nawasihi hata msimpange maana atapata life ban akikutana na nguli Chiellini na kidume Evra
Naomba address ya ofisi yako mpya ya usangoma, maana naona unapiga ramri na kuagua hapa nyumbani kwa mabuluda bila woga wala haya, lol
 
Last edited by a moderator:
Washabiki wa Juventus napenda kujua toka kwenu, hivi hili jina la utani la Kibibi kizee (the old lady) lilikujaje kwa hii timu!?

Juventus ilianzishwa na vijana wanafunzi wadogo sana kule Torino mwaka 1897.Ikaitwa Juventus (vijana) kwa sababu hiyo.Baadae ilipokua na kuchukuliwa na tajiri wa viwanda mzee Agnelli ikabatizwa jina la "la fidanzata d'italia" (the darling/girlfriend of Italy) na wafanyakazi wa viwandani toka Italia ya kusini.Kule Italy historically kuna mgawanyiko wa kitabaka,la walionacho na wasionacho.Matajiri wengi kihistoria wanatokea Northen Italy na walalahoi wengi wako Southern Italy,mahala ambako kuna wahamiaji wengi toka nje ya Italy ambao walikwenda kuajiriwa viwandani na mashambani miaka hiyo.Hivyo waitaliano wenyewe wanabaguana,wale wa North ambao wengi ni blondes wakijinasibu kuwa maburuda asilia na kuwaona watu wa South wenye nywele nyeusi walalahoi "wakuja".Sasa Juve ilikuwa Turin kwa matajiri lakini ikapata sapoti ya wafanyakazi wengi toka South kutokana na kuwa timu ya wanafunzi na wafanyakazi wa viwanda na mashamba ya akina Agnelli.In a special case,mashabiki hao wengi mwanzoni walikuwa waingereza waliokuwa viwandani kwa Agnelli.Hivyo kutokana na kupendwa na watu wengi toka pande zote za Italia na haswa Kusini kwa walalahoi walio wengi,Juve ikaitwa "mchumba" wa Italia.Kule Italy mwanamke anaheshimika sana na kuwakilisha upendo.Pia mwanamke mzee anaheshima zaidi kwa utamaduni wao miaka ile.Kwa hiyo Juve kuitwa "lady" ni kutokana na kupendwa sana enzi hizo.Miaka ya 1930's Juve maarufu iliyotwaa vikombe na kutoa wachezaji wengi kwenye national team ya mzee Pozzo iliyotwaa World Cup ilikuwa na wachezaji wenye umri mkubwa.Ndipo huyu Lady kwa utani akaanza kuitwa bibi mzee(la vechia signora).Kwamba it's no longer a team of young men (Juventus) but the opposite.Hadi leo Juve ina mashabiki wengi Italia ya kusini kwa akina Napoli kuliko kule North iliko Turin,Milan etc.Hii ndio sababu Juve ikicheza na timu za kusini kama Napoli huwa uwanja unajaa moshi wa fataki na polisi wanakuwa na kazi ngumu uwanjani.Ile ndio Yanga ya Italy.Hata mgawanyiko uliopelekea kuzaliwa Torino f.c ulitokana na hilo,pale baadhi walipotaka Juve ihame Turin,wengine wakapinga isihame na kujitoa kwenda kuanzisha Torino.Ndio kuna Derby Dela Mole ambapo juzi tulivyofungwa na Torino uliona Mourinho alikunywa bia wiki nzima kuondoa stress na hata ubingwa hakushangilia.Yeye kwake ubingwa ni hadi amfunge Torino.Naskia ubingwa wa mwaka huu hautambui na alibeba mayai viza kwenye ndege from Dar to Turin kwenda kuchafua basi la Torino kama kawa ha ha haa!
 
Last edited by a moderator:
hakuna kitachotuzuia kubeba ndoo labda fainali ingekuwa home and away kidogo mechi ingetiwa ugumu na marefa ila kwa kuwa fainali ni moja tu kilichomkuta dada mtu real madrid na mdogo wake wa kike barcelona kitamkuta hikohiko...ni mwendo wa kuwazimia fegi wale vigoli wao madoido kina messi.....

signora omicidi!

Teh teh teh teh, wapi Gang Chomba?
 
Last edited by a moderator:
EVRA Vs SUAREZ

Asked about facing Suarez again, Evra said: ‘A lot of people ask me this question. It doesn't matter. The most important thing is I play the final, you know.
'I am proud to be what I am, I am proud about my colour and I will shake his hand, it is no problem, but I will make sure he feels my presence on the pitch.’
ImageUploadedByJamiiForums1431589355.687530.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1431589376.103501.jpg
 
Back
Top Bottom