Juventus Special Thread

Juventus Special Thread

Wakuu naomba mnisamehe leo nitarudi baada ya mtanange kwisha.nina presha sana kwa kweli.nazima tv,simu na pc hadi saa sita.thanks.
 
Leo artist Pirlo atatoa mapande ya PHD yaliokwenda shule wareno watatoka patupu FORZA Juventus. juventus 2-0
 
Belo sio kama mashindano hayawezi muziki wa Benfica mzito
 
Shughuli kushney.haya,hongera zao.Benfica ila kama tunashindwa timu kama hizi sijui zile za CL tutaziweza mwakani?
 
Tutalifumuafumua kama ATM walivyolifanya Yutong la Chelsea

Forza Bianconeri, Forza Conte

Kila la kheri mkuu japo nimejisahau kucheki gemu, nilienda kujipendekeza kwenye maandamano kisha nikapitia ATM bilabila nikafikia kumeza hedex na kupinduka, kesho bora nisiende kazini maana ntakuwa kama shifta niwabinukie sarakasi za kitaulo wanipige BAN.
 
Benfica wako pungufu tangu dk 66, una Vidal,Pirlo,Pogba,Tevez,Lorrente,Buffon,Chielini then Benfica anakusumbua nyumbani

Acha hizo hata Real Madrid ya kina Ronaldo, Figo, Roberto Carlos, Zidane ilikuwa inatolewa makamasi na vitimu vidogo itakuwa Juventus hii?
 
Acha hizo hata Real Madrid ya kina Ronaldo, Figo, Roberto Carlos, Zidane ilikuwa inatolewa makamasi na vitimu vidogo itakuwa Juventus hii?

Msimu huu Juventus ametolewa Champions league kwenye kundi ambalo alistahilI kupita akaangukia kwenye Uropa na yeye ndio alipewa nafasi kubwa kuchukua kombe. Game ya ugenini walipata matokeo mazuri walifungwa 2 -1 so walihitaji goli moja tu na tangu dakika ya 66 Benfica wako pungufu
 
Benfica wako pungufu tangu dk 66, una Vidal,Pirlo,Pogba,Tevez,Lorrente,Buffon,Chielini then Benfica anakusumbua nyumbani

We need another coach.najua ntaonekana wa ajabu au anayekata tamaa mapema but believe me,kwa nilivyoona uchezaji wetu kwenye CL ya mwaka huu hadi europa,Conte hawezi ulaya.tena nimekumbuka safari ya robo fainali ya mwaka jana ilikuwa chini ya makocha wasaidizi.Conte ni mzuri mazoezini lakini ujanja wa uwanjani hana.ikitokea timu inahitaji something extra kwenye mechi,hana msaada.ndio maana mourinho huwa unalalamikia sub zake.
 
Benfica wako pungufu tangu dk 66, una Vidal,Pirlo,Pogba,Tevez,Lorrente,Buffon,Chielini then Benfica anakusumbua nyumbani

Mkuu wape credit Benfica walikuja na game plan wakaitumia na ikafanya kazi. Kuwa mtu pungufu sio lazima ufungwe
 
Mourinho kakimbia jukwaa leo nadhani mapigo ya moyo hayakuwa sawa, poleni sana mabuluda wote ila nawakaribisha May 24 mumuunge mkono buluda mwenzenu Ancelot.
 
Mkuu wape credit Benfica walikuja na game plan wakaitumia na ikafanya kazi. Kuwa mtu pungufu sio lazima ufungwe

Ok kudos to Benfica vipi kuhusu champions league? Kumbuka Juve weekend huenda wakachukua Scudeto msimu wa 3 mfululizo
 
Hahaha Chelsea waliondolewa katika group stage wakati walikuwa watetezi. Inatokea hiyo mkuu, afu kumbuka Juve bado wanajaribu kurudi katika level waliyokuwa nayo kabla hawajashushwa daraja kwa sababu ya fixing.
 
Mkuu wape credit Benfica walikuja na game plan wakaitumia na ikafanya kazi. Kuwa mtu pungufu sio lazima ufungwe

Conte analalamika Benfica hawakucheza mpira.Anadai mpira ulichezwa kwa dk 40 tu,muda uliobaki jamaa walifanya obstractions kibao,na refa akaruhusu kwa kupiga filimbi nyingi na kuruhusu upotezaji muda.
 
Back
Top Bottom