Final whistle,atletico 1 juve 0.
Mambo saba;
(a)tumetawala sehemu kubwa ya mchezo lakini hakuna cha maana tulichokifanya kwa kukosa creativity nje ya penalty box ya wapinzani.
(b)Wachezaji wetu hawana mobility ya kutosha kufungua vyumba na kufanya quick attacks.
(c)tuna defence nzuri lakini matatizo ya Man U yamehamia Juve through Evra,ni mzuri kushambulia but poor in defending especially counter attacks,kuzuia cross,kushuka haraka.Atletico waliamua kumtumia Evra kwa ushindi leo,walimpangia watu watatu waliokuwa kila wakati wanajaa upande wake na ndiko goli lilikotokea.
(d)Jamaa wa goal.com waliosema kuwa Juve is better without Pirlo nadhani wamepata jibu leo.Laiti angekuwepo kwenye mechi tuliyocheza mpira mwingi eneo lake la trequetista,na zile faulo mbili nzuri tulizokosa zote...
(e)Refa ameharibu mechi kwa filimbi nyingi mno,ikawa advantage kwa Atletico ambao dk za mwisho waliharibu mechi kabisa kwa kujiangusha baada ya kugundua udhaifu wa refa,na hii ni dalili walikuwa wamezidiwa kimpira na Juve.
(f)kama hii ndio Atletico ya mwaka huu,basi wajiandae kula dozi nzito Turin na wasipoangalia Olympiakos wanaweza kulazimisha droo,na hali ikawa ngumu kwao.Sijaridhika na kiwango chao,ni udhaifu wa creativity upande wa Juve ndio umewapa ushindi lakini walizidiwa sana hadi uwanja ukawa kimyaa.
(g)Tatizo la creativity katika kushambulia ni kubwa mno Juve,linatunyima ushindi sana,na hili ni suala la usajili,halitengenezwi uwanjani pekee.Hatuna playmakers creative wenye pace na wepesi. Pirlo,Vidal,Pogba wana akili lakini wazito,hawana pace,kuna mechi zinahitaji pace kufungua mifumo ya wapinzani,kama hii.Unapokosa creativity unalazimika kutumia long balls kupeleka attacks na ndicho tulichofanya leo,na yote ikaishia miguuni na vichwani mwa mabeki wa atletico waliofanya kazi moja tu ya kujaa golini kwao.
HITIMISHO;Bado tuna safari ndefu.