Technolojia mpya zote duniani huanzia majeshini, pote, marekani, Israel, Urusi, nk. Hii ni kwa sababu huko ndipo bongo kubwa kabisa huajiriwa. Usitegemee jeshi lililopatikana kwa ajira za vimemo vya wakubwa na kadi za vyama, likuletee matokeo ya ujuzi. Mbali na majeshini, tuelewe kuwa Nchi zote duniani zimepiga hatua kubwa kwa kuwategemea wenye akili kubwa kama watafiti, wangunduzi na watalaam tu
Teknolojia mpya pote duniani imeanzia majeshini, huko ndipo wenye akili kubwa huajiriwa. Ukiwa na jeshi lililopatikana kwa vimemo vya wakubwa na kadi za vyama vyao, usitegemee matokeo ya kiujuzi. Uliyemwajiri alitumia kadi, jina la mkuu fulani au ushabiki wa kisiasa, kumtaka akupe matokeo mazuri ya ujuzi asiokuwa nao, ni kumuonea sana
Teknolojia Bora kabisa katika nchi kubwa kama Marekani, Urusi, Israel, China, Uingereza nk zilianzia jeshini. Wao wanaajiri akili kubwa. Kama ajira ilitokana na ushabiki wa vyama, kadi za vyama na majina ya wakubwa na sio sifa na ujuzi, hatutegemei matokeo tofauti na walivyoingia jeshini. Tunavuna mapando tuliyopanda. Hata maendeleo ya kawaida, nchi zote duniani zimeemdelea kwa kuheshimu, kutumia na kufuata ushauri wa watafiti, wangunduzi na watalaam wabobevu katika nyanja zote, iwe ktk afya, viwanda, elimu ya anga, mawasiliano nk. Ila tukikubali kuongozwa na matamko ya siasa tu ( ambayo kimsingi sio mbaya) tuvumilie maumivu yake miaka mamia yajayo. Ukweli mchungu ni kuwa kuna mambo hayataki kabisa siasa hata kidogo, ingawa siasa Ina mahala pake. Bado hatujachelewa kubadilika,, ila tukiamua.