JWTZ ifanye uchunguzi dhidi ya tabia na mwenendo wa askari wake Denis Urio

Chadema mnajitahidi sana kupotosha ili gaidi asifungwe lakini hamtafanikiwa.

Denis Urio alipewa ruhusa na DCI aendelee kusbirikiana na Mbowe ili mradi tu awe anatoa taarifa ya kila kitu kinachoendelea.
Kama hujui kitu kaa kimya! Unaonekana ulivyopewa ujinga. Denis hakua na jamhuri alivyonaswa kwenye michongo yake we unadhani Ni mtu mwema.
 
Nimewaza hivyo pia,
 
Acha kuunga unfa mambo wewe.unajifanya unajua kumbe hakuna lolote.mwenendo wa Kesi uko live mahakamani nakila mtu anaona kinachoendelea.hizo mbwembwe zako zakujifanya unajua kaa nazo mwenyewe maana ni roho mbaya na chuki tu vinakusumbua.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Issue ni JWTZ kuingizwa kwemye mambo ya kisiasa badala ya kufanya kazi na majujumu yake.
 
Wanajua ukweli kwamba mwenyekiti wao ana maisha mengine nyuma ya Pazia.
 
Ukilaza wake upo wapi.kahitaji vijana wakumlinda hayo mengine yametengenezwa na watu kwasababu zao.kwahiyo badala yakuona ukilaza wa mbowe jiulize wewe uko salama kiasi gani hapo ulipo na hao unaoshirikiana nao kila siku.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Urio ushahidi wake utaleta maana pale tu ambapo wale Makomando nao watakubali kuwa walikuwa mamluki...

Kwasababu huwez chukua raia ukawadanganye halafu uje uwageuke tena....Urio amewakosea sana wenzake..

Nafikiri hata huko makambini mambo yatabadilika sana,, Wanajeshi wataanza kutoaminiana wao kwa wao.
 
mimi n imeongea sheria, wewe unaongea porojo. kwanini usijibu hoja kwa hoja? unatumia kamasi kufikiri?
 
Wanajua ukweli kwamba mwenyekiti wao ana maisha mengine nyuma ya Pazia.
hivi kweli kwa akili zao, na kwa utawala huu, mtu aanze tu kumshitaki mbowe kwa ugaidi bila sababu ya msingi? kweli? akili zao wameuza wapi hawa? kitu pekee mwenyekiti DJ alichokuwa anahitaji ni msamaha, na kwa kusoma upepo msamaha ulitaka kutoka, lakini kina Tundu lisu na wenzake wakajifanya ati hana kosa anasamehewa nini? wanaleta jeuri wakatu watu wana ushahidi? subirini sasa wenzenu wawaonyeshe kwamba kumbe alikuwa na kosa. asote gerezani hadi akome kwa kiburi na jeuri. ukitaka kufanya jeuri na kibri, hakikisha huna makosa.
 
Hii kesi unaweza kuiona kama unavyoona rula kwenye maji ukadhani imepinda. Ila kwa mdau wa sheria anajua kama kuna kesi au la maana kinachotakiwa ni kuona kama kuna elements za kula njama kweli na pia kama kuna elements za kutenda vitendo vya kigaidi. Hizo elements lazima ziwepo na kama zinakosekana, then hazitapatikana.
 
Uchunguzi utafanyika tu kama CDF Mabeyo si fofofo.... yaani urio anajiamulia tu kama vile hajui taratibu za kijeshi zinavyomtaka? Mabeyo amka... huyo mtu kawachafua sana JWT. Eti alikuwa anajiamulia yeye mwenyewe ni wapi na kwa nani na kwa wakati gani atoe taarifa... hivi huko jeshini ndivyo Mlivyo mfundisha kweli au ni magumamshi mengine?
 
wewe ndio unasema ameshindwa, lakini wenye kesi wanajua kwanini wamemleta, ili aje aunganishe dot kwenye ushahidi wa yupi ambaye labda ameshatoa ushahidi au anakuja kutoa ushahidi baada yake. ndio maana tunasema msubiri hadi kesi iishe. msikurupuke.
Kuna kanuni ya kisheria inasema 'haki isitendeke tu, bali ionekane ikitendeka'.
 
Kuna kanuni ya kisheria inasema 'haki isitendeke tu, bali ionekane ikitendeka'.
hiyo kanuni ndio itamtoa mbowe, au nguvu ya ushahidi? hayo ni maneno ya siasa za sheria tu, ila ukifika mahakamani kinachoangaliwa ni uwepo au kutokuwepo ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…