Wachangiaji wengi humu wanaendeshwa na mihemko ya ufuasi wa Mbowe.
Huku wakiwa hawajui mfumo mzima wa mambo mengi wanayoyajadili humu.
Wengi hawajui kwamba hata Jeshini kuna kitengo cha intelijensia za kijeshi.
Kitengo hiki kiko ndani ya makambi pamoja na uraiani pia.
Kinawajibika kuangalia na kufuatilia mienendo ya askari wake wote.
Tabia na Mienendo yao toka ndani ya makambi hadi huku uraiani,hufuatiliwa kwa umakini wa hali ya juu.
Na pale askari anapobainika kwenda kinyume na sheria za kijeshi,basi hukamatwa na kesi zao hufanyika huko huko jeshini kwenye mahakama zao za kijeshi.
Ndio maana tunawaona wale Military Police maarufu kama ma-MP.
Linapokuja suala la kina Adamoo,Luteni Urio sio mjinga kama wafuasi wa chadema mnavyojiamisha.
1 - Kwanza ni lazima atakuwa alitoa taarifa kwenye ngazi husika ndani ya jeshi alikoajiriwa.
Hii ndio maana haijamletea mgogoro kati yake na mwajiri wake.
2 - Lazima ieleweke kwamba suala la kina Adamoo wakati wa tukio hilo tayari walikuwa si wanajeshi.(kutokana na kufukuzwa).
Hivyo Walikuwa ni raia wa kawaida.
Na hivyo kulikuwa hakuna namna jeshi lingeanza kuhusika na ufuatiliaji wa mambo yaliyohusu kesi ya matukio ya uraiani.
Ambayo pia ilikihusu chama cha siasa nchini.
3 - Na hivyo hakuna kitengo sahihi kwa makosa ya Jinai ya uraiani zaidi ya ofisi ya DCI.
4 - Luteni Urio atakuwa alifanya hivyo kutokana na maelekezo toka uongozi wa pande mbili.na alipata ridhaa kutoka kwa viongozi wake pia.
Na ndio maana amekuja mahakamani kama Shahidi wa serikali,dhidi ya Aikaeli Mbowe na wenzake watatu.
Kama kina Adamoo wangekuwa wakipanga mipango ya kulihujumu jeshi moja kwa moja.
Pia kuna kitengo maalum jeshini ambacho kingehusika nao mpaka mwisho.
Ila mwisho wa siku kesi yao ingeangukia kwenye uhaini na wangeshitakiwa kwenye mahakama za kiraia.Sababu walikwisha poteza sifa kuu ya kushitakiwa kwenye mahakama za kijeshi.
5 - Nina amini kwamba hata Luteni Urio,baada ya kuripoti tukio hilo kwenye ngazi husika,lazima naye alibaki kwenye uchunguzi au ufuatiliwaji wa nyendo zake zote na vitengo husika toka ndani ya jeshi.
My take:
Sioni sababu ya kila mwanachama wa chadema kugeukia uanasheria,wakati chama kimeweka Mawakili Wasomi kazini.
Vinginevyo ni kujiumiza na kupoteza muda kwa mijadala isiyoweza kubadili ukweli halisi wa mwenendo wa mahakamani kuhusiana na kesi iliyoko kortini.