JWTZ ifanye uchunguzi dhidi ya tabia na mwenendo wa askari wake Denis Urio

JWTZ ifanye uchunguzi dhidi ya tabia na mwenendo wa askari wake Denis Urio

Chadema mnajitahidi sana kupotosha ili gaidi asifungwe lakini hamtafanikiwa.

Denis Urio alipewa ruhusa na DCI aendelee kusbirikiana na Mbowe ili mradi tu awe anatoa taarifa ya kila kitu kinachoendelea.
Kama hujui kitu kaa kimya! Unaonekana ulivyopewa ujinga. Denis hakua na jamhuri alivyonaswa kwenye michongo yake we unadhani Ni mtu mwema.
 
Mpaka sasa inaonyesha huyu urio huko nyuma alikuwa na mawasiliano mazuri tuu na mbowe tena yenye maslahi ya kumtafutia vijana wa kumlinda mbowe
Na inavyoonyesha katika kuwasiliana kwao huenda walidukuliwa bila wao kujua.
Sasa ilipokuja kushtukiza kukamatwa huyu bwana urio inaonyesha alikamatwa kimya kimya akapangwa kum badilikia mbowe ili mbowe aonekane kuwa alidhamiria sasa kinachotokea huyu urio na akina kingai na huu mpango hawakuupanga vizuri ndio maana kwa sasa inaonekana mi mavi inamrukia urio.
Huku mbele kesi inavyoenda msishangae huyu urio akaja kiri kuwa alipangwa aseme hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimewaza hivyo pia,
 
ukisikia kitu kinaitwa " Proof beyond reasonable doubt - uthibitisho usioacha shaka"haitegemei shahidi mmoja, wakati mwingine huwa unategemea circumstantial evidence ambayo ili uthibitishe unatakiwa uwe na ushahidi wa matukio yasiyokatika kwenye mnyororo wake.....hivyo kila shahidi anakuwa na kakitu kake anakuja kuthibitisha anaondoa,ninyi mtahangaika kupuyanga kwenye cross examination kuuliza maswali ya kufurahisha umma kumbe wenzenu kile walichomleta aje kuthibitisha sicho kile mnachokishambulia. ndilo linalotokea hapo kwenye kesi, hadi nawaonea huruma hao mawakili wa mbowe. hawaelewi kitu, ila wanajua kuufurahisha umma ambao hawa haujui mambo ya kisheria zaidi ya ushabiki wa kisiasa.
Acha kuunga unfa mambo wewe.unajifanya unajua kumbe hakuna lolote.mwenendo wa Kesi uko live mahakamani nakila mtu anaona kinachoendelea.hizo mbwembwe zako zakujifanya unajua kaa nazo mwenyewe maana ni roho mbaya na chuki tu vinakusumbua.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
sasa, tufanye amejichanganya, nini mnachoumia ni nini? si ndio maana tunasema subirini kesi iishe ili maamuzi yatoke, kama mnajiamini kwanini mnaogopa kesi kuendelea? au mnaogopa mashahidi wengine, ambao hamuwajui watakuja kupigilia msumari? tulieni dawa iwaingine.mambo yapo mikonini mwa mahakama.
Issue ni JWTZ kuingizwa kwemye mambo ya kisiasa badala ya kufanya kazi na majujumu yake.
 
sasa, tufanye amejichanganya, nini mnachoumia ni nini? si ndio maana tunasema subirini kesi iishe ili maamuzi yatoke, kama mnajiamini kwanini mnaogopa kesi kuendelea? au mnaogopa mashahidi wengine, ambao hamuwajui watakuja kupigilia msumari? tulieni dawa iwaingine.mambo yapo mikonini mwa mahakama.
Wanajua ukweli kwamba mwenyekiti wao ana maisha mengine nyuma ya Pazia.
 
Kwa upande mwingine hii issue imewathibitishia wenye akili timamu jinsi Mbowe alivyo kilaza.

Kipi kilimfanya amuamini Urio kiasi hicho? Kisa u-homeboy pekee?

Hivi kama ungesukwa mkakati wa kumpelekea watu wa usalama badala ya hao akina Lijenje angesanuka?

Hata jeshi letu la polisi halina tu watu makini,huyo jamaa alikuwa kajivisha kitanzi mwenyewe.
Ukilaza wake upo wapi.kahitaji vijana wakumlinda hayo mengine yametengenezwa na watu kwasababu zao.kwahiyo badala yakuona ukilaza wa mbowe jiulize wewe uko salama kiasi gani hapo ulipo na hao unaoshirikiana nao kila siku.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Urio ushahidi wake utaleta maana pale tu ambapo wale Makomando nao watakubali kuwa walikuwa mamluki...

Kwasababu huwez chukua raia ukawadanganye halafu uje uwageuke tena....Urio amewakosea sana wenzake..

Nafikiri hata huko makambini mambo yatabadilika sana,, Wanajeshi wataanza kutoaminiana wao kwa wao.
 
Acha kuunga unfa mambo wewe.unajifanya unajua kumbe hakuna lolote.mwenendo wa Kesi uko live mahakamani nakila mtu anaona kinachoendelea.hizo mbwembwe zako zakujifanya unajua kaa nazo mwenyewe maana ni roho mbaya na chuki tu vinakusumbua.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
mimi n imeongea sheria, wewe unaongea porojo. kwanini usijibu hoja kwa hoja? unatumia kamasi kufikiri?
 
Wanajua ukweli kwamba mwenyekiti wao ana maisha mengine nyuma ya Pazia.
hivi kweli kwa akili zao, na kwa utawala huu, mtu aanze tu kumshitaki mbowe kwa ugaidi bila sababu ya msingi? kweli? akili zao wameuza wapi hawa? kitu pekee mwenyekiti DJ alichokuwa anahitaji ni msamaha, na kwa kusoma upepo msamaha ulitaka kutoka, lakini kina Tundu lisu na wenzake wakajifanya ati hana kosa anasamehewa nini? wanaleta jeuri wakatu watu wana ushahidi? subirini sasa wenzenu wawaonyeshe kwamba kumbe alikuwa na kosa. asote gerezani hadi akome kwa kiburi na jeuri. ukitaka kufanya jeuri na kibri, hakikisha huna makosa.
 
Shida mnakuja hapa na kujifanya mnajua kumbe wasindikizaji tu. unafikiri kweli jeshi halina taarifa za kutosha na mtu wao hadi anakuja kutoa ushahidi? pia, tuchukulie mfano, Mbowe ambaye alikuwa anamwita urio "homeboy", ameamua kuingia kwake ili amtafutie walinzi na akaamua kumshirikisha huyo homeboy wake uovu anaotaka kuufanya akijua kwamba urio hatamsaliti kwasababu wametoka mbali na ni homeboy, urio akafikisha taarifa ile kwa wakubwa zake, lazima wakubwa zake watamwelekeza akende polisi, na akifika polisi lazima tu watamwambia "ili tumpate mbowe na uovu anaouwaza, jifanye kushirikiana naye".

Hapo watashirikiana hadi kuwapata hao walinzi na mambo yote yaliyoendelea mbowe akiamini kuwa urio yupo upande wake kumbe mwenzake ameshakuwa pandikizi. kumbuka kuwa hayo mambo ua uovu lazima yalikuwepo kitambo na serikali ilikuwa inatafuta namna ya kureveal kupata ushahidi. mbowe akaingia king...na ndio yupo hapo anashangaashangaa tu anatokaje, anasubiri tu huruma za wananchi na serikali. ukweli halisi anaujua mbowe, na Mungu anamuona.
Hii kesi unaweza kuiona kama unavyoona rula kwenye maji ukadhani imepinda. Ila kwa mdau wa sheria anajua kama kuna kesi au la maana kinachotakiwa ni kuona kama kuna elements za kula njama kweli na pia kama kuna elements za kutenda vitendo vya kigaidi. Hizo elements lazima ziwepo na kama zinakosekana, then hazitapatikana.
 
Uchunguzi utafanyika tu kama CDF Mabeyo si fofofo.... yaani urio anajiamulia tu kama vile hajui taratibu za kijeshi zinavyomtaka? Mabeyo amka... huyo mtu kawachafua sana JWT. Eti alikuwa anajiamulia yeye mwenyewe ni wapi na kwa nani na kwa wakati gani atoe taarifa... hivi huko jeshini ndivyo Mlivyo mfundisha kweli au ni magumamshi mengine?
 
wewe ndio unasema ameshindwa, lakini wenye kesi wanajua kwanini wamemleta, ili aje aunganishe dot kwenye ushahidi wa yupi ambaye labda ameshatoa ushahidi au anakuja kutoa ushahidi baada yake. ndio maana tunasema msubiri hadi kesi iishe. msikurupuke.
Kuna kanuni ya kisheria inasema 'haki isitendeke tu, bali ionekane ikitendeka'.
 
Kuna kanuni ya kisheria inasema 'haki isitendeke tu, bali ionekane ikitendeka'.
hiyo kanuni ndio itamtoa mbowe, au nguvu ya ushahidi? hayo ni maneno ya siasa za sheria tu, ila ukifika mahakamani kinachoangaliwa ni uwepo au kutokuwepo ushahidi.
 
Back
Top Bottom