Hii kesi inayoendelea mahakamani imeufungua macho umma wa Watanzania juu ya tabia ya askari huyo.
Aina ya Ushahidi ambao komando Urio ameutoa mahakamani umeacha maswali mengi sana ya umma juu ya tabia ya askari huyu lakini pia hata kuathiri taswira ya jeshi mbele ya umma.
Kuna haya mambo yafuatayo:
1. Je, jeshi lina taarifa za askari wake Denis Urio kumtafutia Mbowe walinzi ambao yeye Urio anasema walipanga kufanya uhaini? —Hata hivyo mahakamani Urio kasema hakuripoti Jeshini bali karipoti kwrnye mamlaka ya kipolisi. Je, hivi ndivyo askari wa JWTZ anavyopaswa kufanya pindi anapopata taarifa za uhaini?
2. Ushahidi wa Urio una matobo mengi, kuna kila sababu ya kudhani kuwa Urio anatoa ushahidi wa uwongo ili kuwaumiza raia wasio na hatia–Hapa JWTZ haina budi kufanya uchunguzi binafsi na kujiridhisha juu ya mwenendo na tabia za askari wake huyu Denis Urio
3. Mbele ya jamii ni vigumu kwa JWTZ kujiweka pembeni katika hii kesi kwa sababu, wananchi wanapata taswira mbaya kuwa JW inatumika kisiasa kuumiza wapinzani—Kwa hiyo ipo haja kwa JWTZ kujisafisha dhidi ya tabia na mwenendo wa Denis Urio kama ulivyothibitika katika ushahidi anaoutoa mahakamani.
Ndugu
Missile of the Nation zipo undoubtful facts kadhaa zimefunuliwa na kesi hii;
1. Kuna uwezekano wa 99% huyu Denis Urio si askari wa JW bali alipandikizwa huko na kupachikwa uaskari wa JW na cheo just for a special mission huku CDF Mabeyo akiwa anafahamu fika au akiwa hafahamu kabisa kinachofanyika...
USHAHIDI:
Haya yanathibitishwa na circumstantial evidence inayomzunguka huyu shahidi, mathalani;
å Elimu ya huyu bwana kwa maelezo yake ni sekondari K.4 Haiwezekani mtu mwenye elimu level hii apate cheo cha "u - luteni" hata kama atakuwa mwanajeshi miaka 30 unless afanye K.6 kisha apate ingalau shahada ya chuo kikuu...
å Kama nilivyosema, alikuwa kule kwa kazi maalumu. Haijui basics za kawaida kabisa za kijeshi. Kaifanya hiyo kazi, kaimaliza lakini in a awful and very disgraceful end....
Hata alipokuja mahamakani kutoa huo ushahidi wake, hakutokea na hayupo kazini kitambo tu. Ametokea mafichoni...!!
2. Taasisi zetu (Executive, Judiciary & Parliament) by in large ndizo zimekuwa chanzo cha maovu ktk taifa letu. Yaani ile hali ya lawlessness katika nchi yetu inaanzia juu kwa wenye mamlaka ya kulinda na kutetea katiba na sheria za nchi kuja chini kwa raia Wa kawaida....
Kaatika mazingira tunadhani nini kitatokea huko mbeleni? Honestly, yeyote anaweza kuwa na correct prediction, kuwa tusipobadili hàli peacefully sasa kwaa kusema enough is enough, basi tutakuja kuibadilisha kwa kuamuliwa na wengine...!
Kwa mfano, katika sçenario hii ya mwanajeshi Denis Leo Urio, hebu tujaribu tu kufikiri hili...
Kwamba, iweje mwanajeshi mwenye mafunzo ya kulinda usalama na mipaka ya nchi anavuka mipaka ya majukumu yake na kuanza kushiriki uovu wa kuhujumu haki za raia wa kawaida huku vyombo vyenye mamlaka vikiangalia tu uchafu huu..?
Nani amchunguze nañi sasa kwa sababu the whole system is corrupted..?