JWTZ ifanye uchunguzi dhidi ya tabia na mwenendo wa askari wake Denis Urio

Hiyo akili hawana,watu wanapiga posho ndefu!Fikiria Jaji,Mawakili wa Serikali,waendesha mashtaka,maafisa mahakama,magereza nk,wanalipwa bei gani@moja kwa siku mara miezi kibao.Tozo zetu zinateketea!
Tunapodai Katiba Mpya tunamaanisha.
na wewe kasome ulipwe kama unawatamania mzee.
 
Wewe hujui ni nini viapo vya jeshi sababu hujawahi kuwa mwanajeshi.
Hapo ni kwamba jeshi linaepushwa na hizi kadhia za uraiani.

Akishatamka kwamba aliwataarifu nini kinachofuatia kama si kutaka jeshi kupitia maafisa wake kuja kuthibitisha kwenye civilian courts??

Kuwa muelewa.
Huko baadae atakuja shahidi wa serikali kueleza jinsi walivyopokea taarifa za Luteni Urio na taratibu walizochukuwa kutoka kwa mamlaka husika.

Bado mashahidi zaidi ya kumi wanaletwa.

Hakuna papara!
 
Lazima CDF anajua! Huenda ni agizo la Amiri Mkuu kuomba jeshi lisaidie kuokoa jahazi.
 
na wewe kasome ulipwe kama unawatamania mzee.
Nipo vema,sijui wewe?Sikuwa natamani wanacholipwa bali jinsi tulivyosababishiwa gharama na waroho wachache kwa tamaa za fedha na vyeo wasivyostahili.
Kesi ni ya mchongo na haikustahili kuwa mahakamani.
 
Chadema mnajitahidi sana kupotosha ili gaidi asifungwe lakini hamtafanikiwa.

Denis Urio alipewa ruhusa na DCI aendelee kusbirikiana na Mbowe ili mradi tu awe anatoa taarifa ya kila kitu kinachoendelea.
DCI na JWTZ wanahusiana vipi?
 
Samia sio mwanasheria, usitegemee mtu ambaye sio mwanasheria awe perfect kwenye kauli, kwa taarifa yako leo hii kuna watu huwa wanaamini ukifungua kesi polisi, imeshafunguliwa mahakamani. msishikilie bango kitu ambacho hakina hata mantiki.
Kutokuwa mwanasheria ni tiketi ya kusema uwongo?
 
Kama hicho unachosema ni sahihi basi amechanganya mambo mengi sana Urio.

Moja ameoneshwa print out leo number zimetofautiana na amekiri yeye haifahamu hivyo inaleta ukakasi kwemye ushahidi wake.

Pili fedha alizotumiwa hazieleweki ni kiasi gani zilienda kwa watuhumiwa na kiasi kilichobaikia. Vingijevyo na Ltn Urio anakuwa mnufaika wa fedha za ugaidi

Tatu anakana wale sio magaidi ni watu wema. Hivyo ushahidi wake unatia shaka. Maana kila mara anabadilisha kauli yake.

Lakini pia ameshindwa kuonyesha call log kwemye simu kama alivyoonesha msg kwemye simu hivyo ushahidi wa voda/tigo/airtel unakosa locus kwa maana hakuna maana kwenye simu inaonyesha alipiga kutoka handset......kwenda kwa recipient... tofauti na hiyoprintout ya operators.

Pia kwa mahojiano ya leo anakiri kwamba hakushorikisha mamlaka za juu yake zaidi ya kutoa taarifa polisi na kuna taarifa alificha.

Yaani mapungufu ni mengi kuweza kusema ushahidi wake ni credible.

All in all tusubirie tuone kama kuna shahidi mwingine ataluja kufanya curing ya mapungufu yaliyojitokeza.
 
inaonekana wanajeshi wanawaamini kina kingai na mahita ku deal na materrorist kuliko hapo jeshini kwao kuna shida mahala tena kubwa sana
 
Sawa Afisa Viapo wa Jeshi! Kiapo kimwambie kukusanya magaidi afu kimkataze kulitaarifu Jeshi!!!
 
ndio maana tunasema mnafikiria kwa kutumia kamasi, sio ubongo ninyi. akilini mwako umeweka kwamba gaidi ni yule anayevaa mabom, soma sheria ya ugaidi utaelewa vizuri kuliko kushika pua kama mwimba taarabu.
Gaidi akate mti aweke barabarani una Mapooza ya akili kweli. Juzi pale barabara ya Moro dodoma maeneo ya mkundi watu wameweka miti baada ya mtoto kugongwa Ni magaidi wale.kuzalisha Kizazi Cha Aina yako kisichoweza kufikili kinasifiwa sana na jamii ya kina ndiyoooooooooo
 
m nahis hawana nia ya kumfunga jamaa bali ni kumtoa mchezon kisaikoloji ili kuudhofisha upande wa pili kwa kishindo
ukiwa mcheza chess unaweza ona kama mim
 
Sawa Afisa Viapo wa Jeshi! Kiapo kimwambie kukusanya magaidi afu kimkataze kulitaarifu Jeshi!!!
Alitoa taarifa kwa ngazi husika na tangia hapo ndipo mission nzima ikaanza utekelezaji.

Hakuwatafuta kabla ya kutoa taarifa.

Tena amesema wazi kwamba mwanzoni alidhani ni walinzi lakini alipogundua malengo siyo ulinzi ndipo alipowahi mapema.
 
acheni ujinga, just google sheria ya ugaidi tanzania, nenda nyumbani kwako kasomee vipengele vyote, utashangaa yale ambayo wewe haujui kama ni ugaidi, ni ugaidi. tatizo mnaamini gaidi lazima avae mabomu ndio shida yenu. namna zingine za ugaidi zikifanyika hamuamini kwasababu mabomu hayakuvaliwa. someni sheria ili muache ubishi. vichwa vyenu vimeliwa na funza nyie.
 
2-2 =0 ndio akili yako ilivo
 
sasa, tufanye amejichanganya, nini mnachoumia ni nini? si ndio maana tunasema subirini kesi iishe ili maamuzi yatoke, kama mnajiamini kwanini mnaogopa kesi kuendelea? au mnaogopa mashahidi wengine, ambao hamuwajui watakuja kupigilia msumari? tulieni dawa iwaingine.mambo yapo mikonini mwa mahakama.
 
Nipo vema,sijui wewe?Sikuwa natamani wanacholipwa bali jinsi tulivyosababishiwa gharama na waroho wachache kwa tamaa za fedha na vyeo wasivyostahili.
Kesi ni ya mchongo na haikustahili kuwa mahakamani.
usingelalamika kwa kulipwa kwao kama upo vyema. kinachokuuma ni nini sasa? ati umekaa nyumbani huna mbele wala nyuma alafu unasema kesi ya mchongo, hujui kilichomo kwenye jalada, unasubiri tu usikie kwenye magazeti, izo ni akili au matope?
 
Mpaka sasa inaonyesha huyu urio huko nyuma alikuwa na mawasiliano mazuri tuu na mbowe tena yenye maslahi ya kumtafutia vijana wa kumlinda Mbowe.
Na inavyoonyesha katika kuwasiliana kwao huenda walidukuliwa bila wao kujua.

Sasa ilipokuja kushtukiza kukamatwa huyu bwana urio inaonyesha alikamatwa kimya kimya akapangwa kum badilikia mbowe ili mbowe aonekane kuwa alidhamiria sasa kinachotokea huyu urio na akina kingai na huu mpango hawakuupanga vizuri ndio maana kwa sasa inaonekana mi mavi inamrukia Urio.

Huku mbele kesi inavyoenda msishangae huyu Urio akaja kiri kuwa alipangwa aseme hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usingelalamika kwa kulipwa kwao kama upo vyema. kinachokuuma ni nini sasa? ati umekaa nyumbani huna mbele wala nyuma alafu unasema kesi ya mchongo, hujui kilichomo kwenye jalada, unasubiri tu usikie kwenye magazeti, izo ni akili au matope?
Jibu swali, unateseka ukiwa wapi? Gazeti nilisomalo kama ni chombo cha habari inakuwaje tatizo ilhali nawe unaliperuzi?
Usikisie maisha ya wengine.Kesi kuwa ya mchongo hilo hatubishanii maana hata wewe ni shuhuda.Hayo ya akili tope nadhani yanakuhusu mwenyewe,siyo kawaida kum-Judge usiyemfahamu.Dont Judge people according to your own mentality,you're bound to fall.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…