JWTZ imejifunzaje kwa Armenia vs Azerbaijan?

JWTZ imejifunzaje kwa Armenia vs Azerbaijan?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Sisi hatupo vitani,ila tunayo ya kujifunza.
1. Miaka mingi iliyopita Armenia ilitandika Azerbaijan na kunyang'anya maeneo makubwa.

2. Mwaka 2020 Azerbaijan ilijipanga ikaanzisha vita, Armenia walikuwa na majeshi na silaha nzito mno lkn hawakujua alichokuwa nacho adui yao.

3. Armenia alipigwa,wanajeshi wake waliuawa hadi wakaweka silaha chini.hadi sasa Azerbaijan amerudisha maeneo yake.

4. Vita vya siku hizi sio vya maguvu,ni vya akili na technologia.

5. Wakati Armenia amekuja na vifaru na jeshi imara kama tulivyozoea, Azerbaijan alikuja na Drones,nyingi na efficient zikaua wanajeshi wengi.

6. Walinunua drones bora sana toka kwa Israel na Uturuki. Amini usiamini,wameshinda vita yote kwa drones.

7. Kwa sasa Israel,uturuki,china,ufaransa na marekani wameboresha sana technolojia hii.

8. Azerbaijan ni nchi ya kiislam lakini ni ally wa israel dhidi ya Iran,mosas hupitia pale kupeleleza na kutandika iran. Armenia ni pure christian ila hawana faida kwa israel. Wanajeshi wengi sana wa Azerbaijan wamekuwa trained kwa tech mpya,ans it yielded.

9. Israel wapo very close na Rwanda,wamewauzia silaha,na tech hii ndio walitaka watujaribishie kipindi kile tunataka kuwatwanga. Tungepigwa kama watoto. Hawakufanya hivyo kwasababu israel inatuhitaji na hawapendi adui ukanda huu. Ila tukileta fyokofyoko wangetufanya lolote.tushukuru Mungu kumtumia Blair.

NB:-Siongei hivi kwa kuichukia israel,mimi ni pro-israel na pro-jrws. Mungu ibariki Israel.

10. Jeshi letu pia wanunue vifaa vya kisasa,kama huamini,soma kilichotokea vita ya Armenia mwaka jana,waloaibika kupita kiasi. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Sikuhizi ni mwendo wa jicho la mwewe tu kunako angani kwa kutumia teknolojia ya drones ambayo inaweza kurushwa na binti mdogo tu akiwa ofisini mkono moja kashika kikombe cha chai mwengine anateketeza maadui kwa drone.

Hakuna kujificha mbele ya drone, kitu kipo angani kina camera inayo zoom, ikiku zoom unalo.

Mnaweza kupitia mafunzo ya ukakamavubwa hali ya juu karibu mwaka mzima, ila kwa drone, hata binti ambae ni kuruta alie na muda wa wiki 1 tu kambini anaweza kuteketeza hao wote walipotia mafunzi makali mwaka mzima, achana na teknolojia aisee.

Mkuu wa majeshi ya Iran pamoja na mabidi gadi wake aliishia kupigwa na drone kipindi cha trump, achana na teknolojia aisee.

Yani ni kama mtu anacheza game tu kumbe anafanya kweli,

 
Hv kwanini unakaa Tanzania ikiwa unadharau nchi yako hivyo? Seriously unawezaje ukadharau nchi yako na kulinganishabna kaanchi kadogo tena tunayoijua kupitiliza.

Chezea Taasisi zote lakini sio JWTZ
Hakuna anayeidharau nchi yake,kwa taarifa yako discussions kama hizi ni za wapenda nchi kuliko wewe mwenye kiburi na unafiki. Nchi kubwa mara nyingi zinatumia nchi ndogo kufanya test ya silaha walizotengeneza, Armenia ni nchi ndogo sana ukilinganisha na azerbijan,wana jeshi imara na vita vya miaka ile waliwatandika azerbaijan hadi wakanyoosha mikono,hata walipoenda vitani juzi walijua mteremko. Kumbe Azerbaijan waliuza gas na mafuta mengi wakanunua drones za kisasa. Wakaua sana wanajeshi,na kushinda vita. Rwanda hana uwezo kutushinda na igomvi huo ungeenda miaka mingi tusingekubali kushindwa,ninachosema mataifa kama israel ambao yayari wamesaply vifaru vya kisasa rwanda,na wanawachukulia kama ni genocide survivors wenzao,wangewasaidia. Sidharau nchi wala jeshi,sitafanya hivyo hata siku moja.
 
Hv kwanini unakaa Tanzania ikiwa unadharau nchi yako hivyo? Seriously unawezaje ukadharau nchi yako na kulinganishabna kaanchi kadogo tena tunayoijua kupitiliza.

Chezea Taasisi zote lakini sio JWTZ
Akili kama za kwako ni za kutumia nguvu hata kufikiri,na watu kama wewe ndio hawana faida hapa nchini,kwasababu hamtaki mawazo mbadala,hata kama ni mazuri. Enendeni na utawala mpya wa mama. Fikra duni na za kusaidiwa hata kufikiri awamu hii ya 6 ya mama zimeshazikwa.
 
Siku hizi usiombeee vita kabisa! hata nchi adui iwe dhaifu kiasi gani, kwani mkianzisha vita tu huo ugomvi mnawauzia Urusi, Marekani,China au NATO. Watawageuza nyie kuwa uwanja wa kujaribishia silaha na tech. zao mpya.
Mwisho wa siku mtakaoumia na kuteseka na nyie.

Tupambane vita ya kiroho tu kwa kumuomba Mungu na kutafuta pesa basi, haya mengine tuwaachie wababe wa dunia.
 
Sikuhizi ni mwendo wa jicho la mwewe tu kunako angani kwa kutumia teknolojia ya drones ambayo inaweza kurushwa ma mtu anae irusha anaweza akawa ni binti mdogo tu akiwa ofisini mkono moja anashika kikombe cha chai mwengine anasulubisha maadui.

Hakuna kujificha mbele ya drone, kitu kipo angani kina camera inayo zoom, ikiku zoom unalo.

Mnaweza kupitia mafunzo ya ukakamavubwa hali ya juu karibu mwaka mzima, ila kwa drone, hata binti ambae ni kuruta alie na muda wa wiki 1 tu kambini anaweza kuteketeza hao wote walipotia mafunzi makali mwaka mzima, achana na teknolojia aisee.

Mkuu wa majeshi ya Iran pamoja na mabidi gadi wake aliishia kupigwa na drone kipindi cha trump, achana na teknolojia aisee.

Yani ni kama mtu anacheza game tu kumbe anafanya kweli,


Drone ulizoelezea hapa ni zile za kwenye movie,ndizo zinaweza operetiwa na kabinti,halafu unaioverate sana teknolojia ya drone wakati ambapo Huwezi kimshoot mtu aliye eneo jingine mpaka uwe na watu hapo wanaokufeed information . accuracy ya drone ni 40%.
 
Si nimeona juzi kati kuwa kampuni ya Lugumi ndo itaendelea na ku-supply vifaa ktk geshi letu....[emoji848]
Sijui atakuwa na connection na huko unakokusema kuwa wako juu ki-tech...!!?
Hivi, huku sikia kashfa zake,
 
Back
Top Bottom