JWTZ imejifunzaje kwa Armenia vs Azerbaijan?

JWTZ imejifunzaje kwa Armenia vs Azerbaijan?

Rwanda walianzisha chokochoko vita itapigwa ndani ya ardhi yake .

Tutampiga upande wa kagera

Tutaingia burundj tutampiga

Tutaingia kongo tutampiga

Tutaingia Uganda tutampiga

Yaani tutamzunguka kote kote tunampiga
Nashangaa sana watu wanaipa promo sana Rwanda wakati tuliisha wahi mshikisha adabu huyu dogo, well labda ni kweli wanajiandaa but kwa Tanzania labda Rwanda ingeweza kupata ushindi enzi za mwendazake, hakutumia hiyo oportunity, sasa hivi asahau kabisa
 
Sisi hatupo vitani,ila tunayo ya kujifunza.
1. Miaka mingi iliyopita Armenia ilitandika Azerbaijan na kunyang'anya maeneo makubwa.

2. Mwaka 2020 Azerbaijan ilijipanga ikaanzisha vita, Armenia walikuwa na majeahi na silaha nzito mno lkn hawakujua alichokuwa nacho adui yao.

3. Armenia alipigwa,wanajeshi wake waliuawa hadi wakaweka silaha chini.hadi sasa Azwebaijan amerudisha maeneo yake.

4. Vita vya siku hizi sio vya maguvu,ni vya akili na technologia.

5. Wakati Armenia amekuja na vifaru na jeshi imara kama tulivyozoea, Azerbaijan alikuja na Drones,nyingi na efficient zikaua wanajeshi wengi.

6. Walinunua drones bora sana toka kwa Israel na Uturuki. Amini usiamini,wameshinda vita yote kwa deones.

7. Kwa sasa Israel,uturuki,china,ufaransa na marekani wameboresha sana technolojia hii.

8. Azerbaijan ni nchi ya kiislam lkn ni ally wa israel dhidi ya Iran,mosas hupitia pale kupeleleza na kutandika iran. Armenia ni pure christian ila hawana faida kwa israel. Wanajeshi wengi sana wa Azerbaijan wamekuwa trained kwa tech mpya,ans it yielded.

9. Israel wapo very close na Rwanda,wamewauzia silaha,na tech hii ndio walitaka watujaribishie kipindi kile tunataka kuwatwanga. Tungepigwa kama watoto. Hawakufanya hivyo kwasababu israel inatuhitaji na hawapendi adui ukanda huu. Ila tukileta fyokofyoko wangetufanya lolote.tushukuru Mungu kumtumia Blair.

NB:-Siongei hivi kwa kuichukia israel,mimi ni pro-israel na pro-jrws. Mungu ibariki Israel.

10. Jeshi letu pia wanunue vifaa vya kisasa,kama huamini,soma kilichotokea vita ya Armenia mwaka jana,waloaibika kupita kiasi. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Unashangaza sana kama siyo kufanya utani. Yaani Rwanda wana uwezo mkubwa kiuchumi (kuliko Tanzania) hivyo kuweza kununua silaha kali ambazo Tanzania haiwezi kununua. Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.
 
Rwanda wasingeweza kutupiga,tungefunga maombi ya siku tatu kwisha habari na drones zao
 
Chezea Taasisi zote lakini sio JWTZ
JWTZ wako vizuri saana kwa military discipline lakini serikali iwaboreshee vifaa vya kisasa na mafunzo ya kisasa. Vita ya Sasa Ni ya drones na sophisticated defense system pamoja na nuclear energy.

JWTZ wanavunja tu matofali... Ukiona military display yao unashangaa.. na siku hizi kijeshi Kama hautengenezi silaha Basi huna cha kuficha co ukinunua tu silaha mtandao husika una Haki ya kupublish

Rwanda wamenunua red arrow missile kutoka China.. Dunia nzima ikajua.... Tanzania hadi Sasa hana silaha Kali alizonunua zaidi ya kuamini kwa wingi wa Askari wake.

Vita vya siku hizi sio military personnel number Bali smart weapons hata Askari waki 20 wanaweza kutandika watu milion 60.
 
Unashangaza sana kama siyo kufanya utani. Yaani Rwanda wana uwezo mkubwa kiuchumi (kuliko Tanzania) hivyo kuweza kununua silaha kali ambazo Tanzania haiwezi kununua. Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi.
Rwanda pesa zake anapata pale Congo anapoiba madini na sio GDP yake Wala nini.
 
Siraha zinazonunuliwa na Jeshi letu hawawezi kuzitangaza kwa kila mtu kama huamini waambie wabeep
Silaha kubwa ya kwanza kwenye vita ni UMOJA unaotokana na UZALENDO kwa nchi yako.

Wakati Tanzania inapigana na Uganda, haikuwa na vifaa vya kijeshi kumzidi Amini.

Tena Idd Amin alikuwa na madege ya kivita yale yenye kasi, alipewa na Gadaff na ndio maana alikuwa na kiburi sana cha kutaka vita.

Ila Watanzania walipigana ile vita kwa moyo sana. Karibia kila mtu alishiriki. Hata vijana wa mtaani tu ambao hawakuwa wanajeshi walienda.

Muhimu kwa vita za sasa hivi, ni UMOJA ( UZALENDO ) na TEKNOLOJIA ndio vitu muhimu. Hivi vitu ndio vinaibeba hata Israel.
 
Silaha kubwa ya kwanza kwenye vita ni UMOJA unaotokana na UZALENDO kwa nchi yako.

Wakati Tanzania inapigana na Uganda, haikuwa na vifaa vya kijeshi kumzidi Amini.

Tena Idd Amin alikuwa na madege ya kivita yale yenye kasi, alipewa na Gadaff na ndio maana alikuwa na kiburi sana cha kutaka vita.

Ila Watanzania walipigana ile vita kwa moyo sana. Karibia kila mtu alishiriki. Hata vijana wa mtaani tu ambao hawakuwa wanajeshi walienda.

Muhimu kwa vita za sasa hivi, ni UMOJA ( UZALENDO ) na TEKNOLOJIA ndio vitu muhimu. Hivi vitu ndio vinaibeba hata Israel.
Israel ina kitu Cha ziada... Israel Wana smart weapons ever... Hata wake waarabu wote milion 500 hawatoboi. Vinu vya nuclear alivyo navyo Israeli sio mchezo.

Kwanini England iliweza kutawala nchi nyingi kubwa za Dunia miaka ile.. walikuwa na silaha imara kwanza.
 
Tangu M23 wapigwe kama mbwa koko. .nina imani Rwanda hamna kitu compared to Tz .sasa Azerbaijan umesema aliuza mafuta akalundika drones, sasa Rwanda atauza nini awe na uwezo wa kupingana na mighty JWTZ. Ondoa cheap propaganda uchumi wa RwandA haujafikia hata gdp per capita ya Tz na tunawazidi population mara tano . Wale ni inferior mno kwa kila kitu isipokuwa kujitangaza sana.. na kuidanganya wavivu wa kutafuta takwimu kama wewe . Elimika ujenge hoja zenye mashiko. Katika vitu ambavyo hawezi Rwand kuthubutu ni kupigana na Tz. Huo itakuwa mwisho wa Kagame na Tz inaweza ikampiga na ikasimika utawla wa kihutu ambao ndio wengi kama ilivyofanya kwa Nkurunziza alipopinduliwa , JK alimrudisha Nkurunziza ndani ya masaa. Waasi wa Burundi walishangaa kupigana na watu wasiojua kuongea kirundi, kumbe Tz ameishamwambia Nkurunziza atulie hawezi kupinduliwa akiwa Tz. Mind you Kagame aliwasupport wale waasi kichinichini lakini Muziki wa JW asingeuweza akaishia kuwalinda waasi baada ya kufurushwa . Rwanda hana uwezo na wala hawezi tamani vita na Tz. Hata kule congo analindwa na maslahi ya Marekani na Uingereza wote wakipora utajiri wa congo. Imagine sheia za UN haziruhusu majeshi ya walinda amani kuwafuata waasi kwenye maficho na kuwatwanga. Inatakiwa tu wakishambuliwa wachukue hata za kujilinda pale walipo. Kama sio hivyo Jeshi la JW wangewapiga miaka ile tumekaa congo kulinda amani. Kule Congo wakubwa wameishajimegea machimbo ya madini mwingereza, marekani ,mfaransa mbelgiji kila mtu ana vitalu mle maporini. Halafu ndio wanawafinance waasi ili congo isipate amani waendelee kuchota.
Na wao wanapora dhahabu na coltan za kutengeneza simu na computers( congo ana 80 per cent ya reserve ya madini hayo duniani ndio maana haiwezi para amani.
 
Mbona tuliwafurusha Rwanda huko mashariki ya Congo ndani ya wiki 2 kupitia kwa mamluki wao m-23 hadi kagame akapanic. Sisi tuna mkataba wa miaka 100 wa wachina kutupa mafunzo ya kijeshi na silaha. Na kipindi cha Kikwete alivyomleta Obama hapa kuna vitu vizuri tulipewa. Ni siri tu. Rwanda mtoto mdogo Sana. Labda Kenya
 
Hii inaitwa red arrow anti tank missiles inayoweza kutandika medium range kwa maana ya any range ndani ya East Africa.

Ana negotiate kununua Air defense system itakayomuwezesha kujilinda na mashambulizi yote ya anga.

Anavyopenda utawala yule bwana tunaweza kujikuta whole East Africa block tunaongea kinyarwanda siku moja.. Kagame Ni war monger.View attachment 1797033View attachment 1797034View attachment 1797035
Wewe umevurugwa..hujui unachoongea. Muulize Rwanda kwanini anaacha vyuo vyote vya kijeshi Africa, analeta wanajeshi wake kuja kufundishwa vita hapa Tanzania
 
Acha kuichukulia poa nchi yako, Rwanda ni nchi ndogo sana hata awe na hizo drones unazosema hawezi kutoboa kwa JWTZ
 
sorry to tell you this ww umeangalia vita moja tu.
America wana moja ya jeshi kubwa la anga.. including drones.
but even today bado wanatuma infantry forces kufanya kazi nzito, huku jeshi la anga likibaki kama support kutoka angani.

Rwanda wangekuwa superior kuliko sis. wasingekuwa wanaleta vijana wao kula coz za uongozi monduli au chuo cha usalama. kila mwaka wanaleta watu wao kujifunza.

Pili huwez shinda vita only buy deploying drones. lazimanu deploy na other forces pia.
I beg to correct many of you who have contributed in this topic, Rwanda haina uwezo au nguvu juu ya Tanzania, hiyo haipo na haitotokea. sikuandika kumaanisha hivyo. nilichotaka kusema ni kwa mataifa makubwa kumtumia, na sio yeye binafsi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Usitufanye wajinga,kwa hiyo Hako kainchi kenu kana uwezo kuliko Tanzania 🇹🇿?
 
Hii inaitwa red arrow anti tank missiles inayoweza kutandika medium range kwa maana ya any range ndani ya East Africa.

Ana negotiate kununua Air defense system itakayomuwezesha kujilinda na mashambulizi yote ya anga.

Anavyopenda utawala yule bwana tunaweza kujikuta whole East Africa block tunaongea kinyarwanda siku moja.. Kagame Ni war monger.View attachment 1797033View attachment 1797034View attachment 1797035
Picha ya kwanza hizo ATM haziwezi piga popote East Africa. ATM zote zikienda mbali ni 10km range. Ziwe man portable, vehicle mounted au helicopter launched.

Picha ya pili ni Pantsir short range air defense system kutoka Russia. Rwanda hana hizi system, hapa Afrika zinaweza kuwa Egypt na Algeria tu. Pale Libya zimepelekwa na UAE kumsaidia Khalifa Haftar.
 
Hii mada nilitaka kuiandika leo nikaona uvivu
Unajua chochote kuhusu hii vita? Nina taarifa za kinyume na za huu Uzi, nimeacha kuzifuatilia mpaka nirudi tena kwenye mafaili na itanichukua muda.
 
Unajua chochote kuhusu hii vita? Nina taarifa za kinyume na za huu Uzi, nimeacha kuzifuatilia mpaka nirudi tena kwenye mafaili na itanichukua muda.
Hakuna vita nimefatilia kama hii kwa miaka ya hivi karibuni. Kwanza hii ilikuwa na taarifa za kila siku angalau kuliko kule Syria na Libya ambako taarifa nyingi zinatoka upande mmoja.

Bahati mbaya mvivu kuanzisha nyuzi
 
Back
Top Bottom