JWTZ imejifunzaje kwa Armenia vs Azerbaijan?

Siraha zinazonunuliwa na Jeshi letu hawawezi kuzitangaza kwa kila mtu kama huamini waambie wabeep
Siku hizi kila kitu kiko wazi... Jeshi likinunua military weapons kokote kule inajulikana. Rwanda kanunua mizigo ya maana kutoka kwa China ba Israel... It's very risk kumuingia Rwanda mzima mzima anakuadhiri mapema tu.

Muhimu jeshi letu lazma liwe modernized and world class army lenye silaha za kisasa zaidi.
 
We unafikiri kwanini Congo Hadi leo anatandikwa na kanchi Kama rwanda? Vita sio ukubwa wa nchi... Vita Ni investment kwenye silaha na intelligence unit Basi.
 
Siri za jeshi zipo kwenye mikakati zaidi na uendeshaji, ila kama unanunua siraha kutoka nje, ni ngumu sana kuwa na usiri labda kama wangekuwa wanatengeneza
 
Kila mbongo sasa hivi akisoma article ya masuala ya jeshi nae anajifanya expert kuja kufundisha jeshi letu.
Uchumi wa nchi una reflect na jeshi lake... Sababu siku hizi uchumi wako ndio utaamua uimara wa jeshi lako. Rwanda kapiga hela kibao toka Congo kwa hiyo ana mkwanja saana na kanunua world class jet fighter za kutosha anazofanyia uhalifu wake kule Congo.
Ambazo sisi bado hatujanunua sababu hazionekani kwenye global index ya weapons purchasing.
 
Hii inaitwa red arrow anti tank missiles inayoweza kutandika medium range kwa maana ya any range ndani ya East Africa.

Ana negotiate kununua Air defense system itakayomuwezesha kujilinda na mashambulizi yote ya anga.

Anavyopenda utawala yule bwana tunaweza kujikuta whole East Africa block tunaongea kinyarwanda siku moja.. Kagame Ni war monger.
 
Hela kibao zipo wapi? Ni kawaida sana madikteta kujisifia kwamba wapo vizuri ila uhalisia huwa ni tofauti.
 
Mkuu, kwanza niseme umetoa somo zuri sana, tena sana cause mazoezi ya kivita na maandalizi yote ya kivita hufanywa kukiwa na AMANI sio wakati wa matatizo, kilicho nileta ni hiyo No 9; Kagame na Rwanda vinakuzwa sana, hivi unakikumbuka kipindi kile JK akiwa rais aliombwaga na UN kwenda Congo kuwadhibiti M23? Unadhani hasa lengo lilikua ni wale M23? Lengo lilikua ni Kagame, KAgame hana hamu na JK, nahisi hata sasa kakata tena mawasiliano na sisi cause rafiki yake kaitwa mbele za haki, sasa hivi tena regime ya Bongo ni kama imerudi the JK regime; KAgame aliomba poo kwa JK mkuu. Tafadhari, rekebisha hiyo No 9, Rwanda sio size yetu kabisa, tuongeage na Kenya labda na Uganda but sio ule nusu mkoa wa Mwanza, Iringa, Tanga nk, Rwanda inakuzwa mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…