Awamu ya 5 haukuwa utawala bali lilikuwa genge la wahalifu. Wakati mhusika mkuu wa genge hili la kihalifu hatunaye, walioshirikiana naye bado wapo. Hawa wakamatwe na kuhojiwa. Wakithibitika kushiriki uovu pasipo shaka, taarifa itolewe hadharani, na wale ambao makosa yao yalikuwa ya kupindukia, wafikishwe mahakamani, na waadhibiwe sawasawa na uovu wao.
Lakini viingozi wa CCM pia wahojiwe, ilikuwaje mtu mwovu wa kiwango kile, jina lake kulipeleka kwa Wananchi na kisha kuwahadaa wananchi kwa kumpamba sifa nyingi nzuri wakati wakijua wazi mhusika alikuwa na mwovu kupindukia.
Rais wa sasa, japo alikuwa miongoni mwa wasaidizi kwenye utawali ule dhalimu, yeye usihusike kuhojiwa wala kushtakiwa maana ndivyo katiba yetu isemavyo, labda tuibadilishe. Na hata ikibadilishwa, bado yeye hatahusika na mabadiliko hayo kwa yale aliyoyashiriki wakati katiba ikiwa inamlinda kutokushtakiwa.