Kabendera: Nimeombwa kuwasilisha vielelezo kuhusu vitisho vya Jaji Biswalo

Narudia tena, Biswalo hawezi kufanywa chochote hata kama lipo zengwe labda chochote anachoweza kufanywa, ni wamuue tu.

DPP anazo siri nyingi mno za hao Viongozi.
Hakuna siri kubwa aliyo nayo zaidi ya yeye alivyoshirikiana na mwendazake kupora fedha za watu.
 
Kupitia Twitter mwandishi wa habari mkongwe Eric Kabendera amesema ameitwa kuwasilisha vielelezo vyake baada ya kutishiwa na aliyekuwa DPP wa Serikali Dr. Biswalo Mganga

Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.

Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.

Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.

Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.

Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.

View attachment 2386947

Pia soma: Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete
Wanaume aina ya Kabendera ndo wanaohitajika katika kipindi hiki...bravo Kabendera...!hakuna kuogopa wala kurudi nyuma
 
Huyu mtusi anatumika vibaya na siku wanaomtumia wakimchoka sijui atakimbilia wapi
Ulikuwepo wakati anafanyiwa hayo?
Au alistahili hayo sababu ni mtutsi?

Jipe muda mahakama zipo tutajua ukweli uko wapi
 
Narudia tena, Biswalo hawezi kufanywa chochote hata kama lipo zengwe labda chochote anachoweza kufanywa, ni wamuue tu.

DPP anazo siri nyingi mno za hao Viongozi.
Wamuue? Sasa mbona unasema hawezi kufanywa kitu?
Hujui kuna watu wamezulumiwa majumba yao sasa hivi wamepewa bure ndugu na washikaji wa Biswalo na wenzake? Na wapo waliojiapia jicho kwa jicho!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kupitia Twitter mwandishi wa habari mkongwe Eric Kabendera amesema ameitwa kuwasilisha vielelezo vyake baada ya kutishiwa na aliyekuwa DPP wa Serikali Dr. Biswalo Mganga

Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.

Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.

Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.

Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.

Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.

View attachment 2386947

Pia soma: Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete
Eric bana ....
 
Inatumika nguvu kubwa kulazimisha kuaminisha umma et jiwe alikua mtu mbaya sana!! lkn kina sisi tupo hapa kumtetea na tunaamini aliwanyoosha wapuuzi kama huyo kakitenge na wapuuzi wengine wa aina hiyo.

Wenye vyeti, wapiga dili ,majizi na washenzi walikiona cha moto kipindi cha jiwe.. akwende zake mpuuzi huyo
 
Kila zama na kitabu chake. Huwezi amini kama haya yangetokea miaka 3 nyuma. Dunia duara na hakuna ajuaye kesho yake. Tutakanyage ardhi Kwa staha
Dunia ni mapishano. Yule alitupisha sasa yupo Samia. Kuna waliomfaidi wanamsifia, kuna walioteseka wanalaani. Wengine wlitesa watu sababu tu walidhani wanamfurahisha
 
Kwenu nyie maCcm ambao hamtaki ukweli mtasema an atumika.
Ila ukweli uko wazi Magu alikuwa muuaji na jambazi.
Subirini watu wateme nyongo. Mlizowea vya kunyonga sasa subirini tule vya kuchinja.
Ni zamu yao ngoja wapitishwe
 
Huyu mtusi anatumika vibaya na siku wanaomtumia wakimchoka sijui atakimbilia wapi
Erick Kabendera ni Mhaya kutoka Kamachumu Muleba. Hana uhusiano na Marehemu Kabendera Shinani aliyekuwa mwanahabari wa radio za Rwanda wakati wa Hyabarimana. Msiandike kwa ku ASSUME
 
Back
Top Bottom