Kabendera: Nimeombwa kuwasilisha vielelezo kuhusu vitisho vya Jaji Biswalo

Sio Rais wa Tz tu . hizi Nchi zetu Africa [emoji288] Zina Marais wenye miguvu Mikubwa zid ya watawaliwa.

S
 
Hatua kali zichukuliwe kama mashtaka yakithibitika
 
Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.[emoji2827]
 
Awamu ya 5 haukuwa utawala bali lilikuwa genge la wahalifu. Wakati mhusika mkuu wa genge hili la kihalifu hatunaye, walioshirikiana naye bado wapo. Hawa wakamatwe na kuhojiwa. Wakithibitika kushiriki uovu pasipo shaka, taarifa itolewe hadharani, na wale ambao makosa yao yalikuwa ya kupindukia, wafikishwe mahakamani, na waadhibiwe sawasawa na uovu wao.

Lakini viingozi wa CCM pia wahojiwe, ilikuwaje mtu mwovu wa kiwango kile, jina lake kulipeleka kwa Wananchi na kisha kuwahadaa wananchi kwa kumpamba sifa nyingi nzuri wakati wakijua wazi mhusika alikuwa na mwovu kupindukia.

Rais wa sasa, japo alikuwa miongoni mwa wasaidizi kwenye utawali ule dhalimu, yeye usihusike kuhojiwa wala kushtakiwa maana ndivyo katiba yetu isemavyo, labda tuibadilishe. Na hata ikibadilishwa, bado yeye hatahusika na mabadiliko hayo kwa yale aliyoyashiriki wakati katiba ikiwa inamlinda kutokushtakiwa.
 
Kusoma hujui hata picha huoni?
Uwendawazimu huanza kama hivyo unavyopitia. Wenzio wanajadili hoja, wewe unaropoka chochote kilicho karibu na kinywa chako. Kafanye uchunguzi wa afya ya akili haraka ili kujiridhisha kuwa unayoyaenena hayana uhusiano na maradhi ya akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…