Kabendera, unakoseaje kwenye kitabu mwaka aliofariki Sokoine, tena mara mbili kwa mpigo?

Kabendera, unakoseaje kwenye kitabu mwaka aliofariki Sokoine, tena mara mbili kwa mpigo?

Kiranga

Platinum Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
78,790
Reaction score
128,275
Disclaimer: This thread will contain some spoilers from the book ""In The Name Of The President: Memoirs Of A Jailed Journalist".

Naam,

Nasoma kitabu cha Erick Kabendera "In The Name Of The President: Memoirs Of A Jailed Journalist".

Kwa wanaonijua, mimi si mtetezi wa Magufuli, kwa hiyo uzi huu si wa kumtetea Magufuli.

Uzi huu ni wa kuhakiki kitabu. Kitabu kina mambo mengi sana ambayo yana utata, episodes za pajama, Osama kukaa Zanzibar, Magufuli kuwa responsible kwa mtoto wake kuwa na HIV, Magufuli kumpiga risasi Ben Saanane Ikulu, just to name a few.

Mimi sitayazungumzia yote hayo, nitazungumzia jambo moja tu ambalo halina utata.

Watu wote wanaojua historia wanajua Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alifariki April 12 1984.

Imekuwa vipi Erick Kabendera kaandika tarehe hiyo kama April 12 1983? Tena nilivyoona mara moja tu, nikafikiri hiyo ni typographical error tu, nikakuta karudia mara mbili, katika kurasa mbili zinazofuatana (108 na 109 in the printed book). Inaonekana ndiyo tarehe anayoifahamu.

Kitabu hakikuwa na editor? Hakikuwa na proofreader?

Leo Clubhouse (Watanganyika House) nimemsikia Absalom Kibanda akiomba msamaha kuwa alipewa kitabu kukifanyia proofreading, lakini hakukipitia vizuri, aliharakisha kukipitia, kaona kina makosa fulani ambayo yatasahihishwa katika second edition.

Nimemsikia pia Zitto Kabwe akisema kuwa kuna tatizo la timeline katika narrative ya tukio fulani.

Replays zipo "Watanganyika" Clubhouse.

Na hao ndio wahusika wachache tu waliokuwa tayari kukiongelea kitabu.

Hili linanipa swali, kama kitabu kimekosea mpaka mwaka aliofariki Edward Moringe Sokoine, je, kitabu kimekuwa rushed, hakijafanyiwa proofreading vizuri?

As much as wengine hawakumpenda Magufuli, ku rush kitabu na kufanya makosa kunawapa wanaompenda Magufuli ammunition ya kudismiss mengi yaliyoandikwa kuwa ni ya uongo.

Kabendera muandishi mkubwa kashindwa ku fact check tarehe ya kifo cha Sokoine hata kwenye Google? Proofreaders wake na editor wameshindwa pia?

Kama hili lina mushkeli, hili lililo wazi ambalo halina utata kabisa, tunaachwa tukijiuliza, mangapi yenye utata mwingi yana mushkeli pia?

Kabendera has to get not only the general narrative right, but the detail too.

Hopefully the second edition will correct this and any other inaccuracy.
 
Ni ishara ya kuwa mengi kwenye hiko kitabu sio ya kweli na labda yameongezewa chumvi na kuyatoa kwenye uhalisia.

Iliyotangulia imetangulia tu, hata kama yakiwepo masahihisho haitatosha kuamini kama upo ukweli.
 
Nachelea kuwa kitabu hata kama kina mengi mazuri ya kujifunza, makosa kama haya yatakifanya kisiaminike chote.
 
Hiyo ndiyo maana ya uandishi. Hilo kosa kidogo halibatilishi kwamba Sokoine alikufa. Tubaki kwenye reli,

Tanzania ilitawaliwa na Kichaa kuanzia mwaka 2015 hadi 2021. Asante Mungu kwa kumtupa Magufuli jehanam
 
Mimi ninalaani udikteta wa JPM.

Kitabu hiki ni kazi ya CCM chini ya boss wake kutafuta uhalali wa kuja kuchaguliwa tena na wananchi hapo Oktoba mwaka huu.

Magufuli ni zao la CCM, hivyo kila alichokifanya JPM kina baraka zote za CCM. Leo hatuwezi kumuweka kona moja JPM kisha tukaiweka CCM kwenye kiti kisafi. Hata huyu aliyepo naye ni mulemule ndo maana mauaji anayoyafanya yanatisha zaidi ya aliyoyafanya JPM.

Kitabu cha Kabendera ni sayansi kubwa imetumika kupitia akili ndogo lakini kimezidi kutuelimisha kwanini ni haki kuitokomeza CCM. Hapa tusijifanye tunamnanga Magufuli ambaye ni sehemu kubwa sana ya CCM kwenye kila kitu alichokuwa anakifanya.

Kibanda, Zitto ni karikenye wa kisiasa, ndivyo ninavyowaona
 
Wewe ukiandika Samio badala ya Samia na ukatudia (ukaridia, sorry ukarudia) tena Samie the next page haimaanishi kuwa unalozungumza juu ya Samia sio factual. Unasemaje?

Tuangalie zaidi Kabendera anasema nini katika kitabu chache errors na typos zipo hata kwa nguli wa uandishi.
 
Hakuna kitu kama hicho, kitabu Cha kabendeea kimejaa masimulizi ya kutungwa.

Et JPM akaenda Kwa Samia amevaa pajama😂😂😂

Yaan Rais MTU anaepangiwa kila tukio lake, aruhusiwe kutoka na kwenda Kwa Samia namna hiyo 😂😂😂😂

So hiyo mmeichomekea ili mpate msingi wankujadili Kifo Cha mtoto wa Hayati JPM
 
Mimi ninalaani udikteta wa JPM

Kitabu hiki ni kazi ya CCM chini ya boss wake kutafuta uhalali wa kuja kuchaguliwa tena na wananchi hapo Oktoba mwaka huu.

Magufuli ni zao la CCM, hivyo kila alichokifanya JPM kina baraka zote za CCM. Leo hatuwezi kumuweka kona moja JPM kisha tukaiweka CCM kwenye kiti kisafi. Hata huyu aliyepo naye ni mulemule ndo maana mauaji anayoyafanya yanatisha zaidi ya aliyoyafanya JPM.

Kitabu cha Kabendera ni sayansi kubwa imetumika kupitia akili ndogo lakini kimezidi kutuelimisha kwanini ni haki kuitokomeza CCM. Hapa tusijifanye tunamnanga Magufuli ambaye ni sehemu kubwa sana ya CCM kwenye kila kitu alichokuwa anakifanya.

Kibanda, Zitto ni karikenye wa kisiasa, ndivyo ninavyowaona
Mkuu,

Mimi sitaki controversies, conspiracy theories, mind bending politics.

Mimi nataka muandishi apatie facts tu.

Kama Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alifariki April 12 1984, aandike April 12 1984.

Muandishi akiandika kuwa Sokoine alifariki April 12 1983, akarudia mara mbili kwamba Sokoine alifariki 1983, kabla sijafika huko kwenye mambo ya utata naona kuna tatizo la basic fact checking.
 
Wewe ukiandika Samio badala ya Samia na ukatudia tena Samie the next page haimaanishi kuwa unalozungumza juu ya Samia sio factual. Unasemaje?

Tuangalie zaidi Kabendera anasema nini katika kitabu chache errors na typos zipo hata kwa nguli wa uandishi.
Naelewa hilo,

Lakini kwa muandishi nguli this was such a basic thing. Na hapo kuna watu watachukua point za kuhoji credibility ya kitabu.

Mimi sijajitanabahisha kuwa muandishi nguli ninayeuza vitabu.

I expected a little better from someone who wrote for The Economist Intelligence Unit, The Guardian, The London Times, The East African etc.

The book was rushed to the printer without sufficient proofreading and fact checking. That is becoming apparent now.

Had it (the error) been once, I would have chalked it up to a typo, the error was made twice in two consecutive page. It seems that Kabendera thinks Sokoine died in 1983 and was going by what he had on his head, and nobody fact checked this.

Where were his proofreaders, fact checkers, editors?

Nyani Ngabu
 
Mkuu,

Mimi sitaki controversies, c9nspiracy tgeories, mind bending politics.

Mimi nataka muandishi apatie facts tu.

Kama Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alifariki April 12 1984, aandike April 12 1984.

Muandishi akiandika kuwa Sokoine alifariki April 12 1983, akarudia mara mbili kwamba Sokoine alifariki 1983, kabla sijafika huko kwenye mambo ya utata naona kuna tatizo la basic fact checking.
Naunga mkono hoja.

Je utetezi wa Kibanda aliyefanya uhariri una mashiko?

Inaonesha walikuwa wanaharakisha kitabu kitoke kwa deadline ya mlipaji wa zumari
 
Nilikushangaa sana mwanzo, Magufuli anasingiziwa mengi mno!

Mwandishi ana tatizo la kisaikolojia kama siyo issue ya afya ya akili! Yule mwandishi aliyemfanyia cross examination, akamwambia tuanze na chapter ya mwisho, juu ya kifo cha mama yake, kuonesha kitabu kimesukumwa na chuki, na trauma ya Kabendera kufungwa na umati wa mzazi wake akiwa jela!

Kuendesha familia tu mke na mtoto watu wanashindwa sembuse nchi.

Mwandishi kasukumwa na apate hela, mauzo makubwa, na kupata hifadhi ulaya. Mwandishi, kama walivyo vijana wengi wanaolelewa na malezi ya mzazi mmoja hasa wa kike, wanakosa udhibiti wa nafsi, kila wazo linalokuja, twende hawachuji!

Matokeo yake: Ukubwani wakikutana na mwanaume , ana act ule u manhood, hawampendi asilani.
 
Back
Top Bottom