Any relevance or effect ya hayo kwenye content yote?
Kuna watu wanajifunza historia watajifunza kuwa Sokoine kafariki 1983, na ukiweka huo mwaka kwenye timeline ya mambo mengine italeta confusion sana. Yani timeline haitakaa sawa mtu asiyejua hili kosa atapata matatizo kuunganisha vitu.
Kabendera kaandika kitabu kwa dunia nzima, watu wengi watajifunzia historia ya Tanzania kwenye kitabu hiki na kupotoshwa.
Pia, kuna watu wana faksafa ya "pipa likishaingia mkojo kidogo tu ndiyo maji yote mkojo tu, hayafai kunywa". Watatumia makosa kama haya ku discredit kitabu kizima na kusema mtu anayekosea kitu cha wazi, kisicho na controversy, kama tarehe ya kifo cha Sokoine, hayo mengine ya ma pajama, Magufuli kumpiga risasi Saanane, kuwa responsibke na mtoto wake kupata HIV, Osama kuka Zanzibar, tutamuamini vipi? So it ruins Kabendera's credibility.
Zaidi, Kabendera hapa amejionesha hayupo makini kwenye sourcing, anapiga hadithi kama anavyofikiri kichwani mwake badala ya kutegemea sources na verification, kwa hiyo wanahistoria wanaotaka serious sourcing wataona tatizo sana hapo.
Ukikosea kitu cha ku verify kwa Google search ya dakika moja, mambo yanayohitaji intricate verification with multiple sources tutajuaje kuwa utaweza kweli?