Kabendera, unakoseaje kwenye kitabu mwaka aliofariki Sokoine, tena mara mbili kwa mpigo?

Disclaimer: This thread will contain some spoilers from the book ""In The Name Of The President: Memoirs Of A Jailed Journalist".

Naam,

Nasoma kitabu cha Erick Kabendera "In The Name Of The President: Memoirs Of A Jailed Journalist".

Kwa wanaonijua, mimi si mtetezi wa Magufuli, kwa hiyo uzi huu si wa kumtetea Magufuli.

Uzi huu ni wa kuhakiki kitabu. Kitabu kina mambo mengi sana ambayo yana utata, episodes za pajama, Osama kukaa Zanzibar, Magufuli kuwa responsible kwa mtoto wake kuwa na HIV, Magufuli kumpiga risasi Ben Saanane Ikulu, just to name a few.

Mimi sitayazungumzia yote hayo, nitazungumzia jambo moja tu ambalo halina utata.

Watu wote wanaojua historia wanajua Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alifariki April 12 1984.

Imekuwa vipi Erick Kabendera kaandika tarehe hiyo kama April 12 1983? Tena nilivyoona mara moja tu, nikafikiri hiyo ni typographical error tu, nikakuta karudia mara mbili, katika kurasa mbili zinazofuatana (108 na 109 in the printed book). Inaonekana ndiyo tarehe anayoifahamu.

Kitabu hakikuwa na editor? Hakikuwa na proofreader?

Leo Clubhouse (Watanganyika House) nimemsikia Absalom Kibanda akiomba msamaha kuwa alipewa kitabu kukifanyia proofreading, lakini hakukipitia vizuri, aliharakisha kukipitia, kaona kina makosa fulani ambayo yatasahihishwa katika second edition.

Nimemsikia pia Zitto Kabwe akisema kuwa kuna tatizo la timeline katika narrative ya tukio fulani.

Replays zipo "Watanganyika" Clubhouse.

Na hao ndio wahusika wachache tu waliokuwa tayari kukiongelea kitabu.

Hili linanipa swali, kama kitabu kimekosea mpaka mwaka aliofariki Edward Moringe Sokoine, je, kitabu kimekuwa rushed, hakijafanyiwa proofreading vizuri?

As much as wengine hawakumpenda Magufuli, ku rush kitabu na kufanya makosa kunawapa wanaompenda Magufuli ammunition ya kudismiss mengi yaliyoandikwa kuwa ni ya uongo.

Kabendera muandishi mkubwa kashindwa ku fact check tarehe ya kifo cha Sokoine hata kwenye Google? Proofreaders wake na editor wameshindwa pia?

Kama hili lina mushkeli, hili lililo wazi ambalo halina utata kabisa, tunaachwa tukijiuliza, mangapi yenye utata mwingi yana mushkeli pia?

Kabendera has to get not only the general narrative right, but the detail too.

Hopefully the second edition will correct this and any other inaccuracy.
Hicho kitabu lazima tu kingekua na makosa maana hayo matukio yote anayoyasimulia anadai kua yeye alipewa tu na "wadau" mbalimbali DM kwenye mitandao yake. Huenda hata inshu ya sokoine aliambiwa hivo kua alifariki 1983..

Kwahiyo hata hizo drama za Jiwe zitakua ni hekaya za abunuwasi nani ataziamini??? Hahahah...

Nanukuu andiko lake aliloliandika huko X zamani Twitter kuhusu namna alivokua anapewa taarifa kutoka kwa wadau wake..
[emoji116][emoji116][emoji116]

"Ndugu zangu,
Ahsanteni sana kwa mijadala na mirejesho yenu. Hata hivyo, wote tukubaliane kuwa huwezi kukijadili vizuri kitabu bila kukisoma kwanza. Ushauri wangu kwenu ni kukitafuta, kukisoma, kukielewa na kujadili.
Nilitaka pia niwakumbushe jambo moja. Mwalimu wangu wa uandishi wa habari za uchunguzi (Investigative Journalism) alinipatia msaada wa shillingi 30,000 mwaka 2003 ili mimi na mwenzangu tupate nauli na pesa za kutoa nakala (photocopy) ya nyaraka zaidi ya 2,000 tulizozikusanya wakati tukichunguza habari kuhusu watumishi wa umma 175 wakiwemo mawaziri waliotumia vyeti feki kuomba kujiunga UDSM kati ya mwaka 1997 na 2002. Kazi hiyo si tu ilinipatia ajira ya kudumu lakini ilinifundisha kuwa watu wanatakiwa kujenga imani kubwa na wewe ili wakupe taarifa au kuwekeza katika ukuaji wako wa kitaaluma. Unatakiwa kuwa na uadilifu wa hali ya juu na kusimamia ukweli ili uaminike. Hii ni mojawapo ya sababu zilizopelekea watu zaidi ya 250 wakubali kuongea na mimi, kunipatia nyaraka na taarifa ambazo zimesaidia kufanikisha kazi hii toka 2017. Sikuwahi kukutana uso kwa uso na wengi wa watoa taarifa hawa lakini wamejenga imani kubwa kupitia kazi zangu na kuamua kuwasiliana na mimi bila kushawishiwa na mtu yoyote. Hakuna rafiki wala ndugu au mtu yoyote anayewajua watu hawa hata kwa kuhisi tu. Shukrani zangu kwao ni kwenda na majina yao kaburini kama ambavyo miiko ya kazi hii inatutaka tufanye. Nimetumia zaidi ya miaka sita kuchuja na kudhibitisha kila taarifa niliyoipokea. Kila mtu aliyenisaidia katika safari ya maisha yangu binafsi au ya kitaaluma alikuwa ananiandaa kuandika kitabu hiki na vingine vilivyoko njiani. Ahsanteni sana.!"

Mwisho wa nukuu.. za kuambiwa changanya na zako
 
Hii ya mwaka aliofariki Sokoine ni suala la Google search moja tu kuihakiki. Hakuna hata haja ya classified document hapo.
 
Yap ndo maana nikasema kama anaweza kukosea hivo hata main content yake inakosa justice maana watu wataamini vipi? Mbaya zaidi kasema hayo aliyoyaandika kasimuliwa na watu mbalimbali..
Ina maana kuna uongo mwingi "uongo ni kama mende, ukiona mmoja jua Kuna wengine.."
Kikubwa nachojua kabendera katumia vizuri "fursa"
 
Mimi pia nimejaribu kupitia kitabu. Kuna matukio kadhaa ambayo Kabendera ameyakosea tarehe. Kwa mfano, anaelezea tukio la kukamatwa kwake na kutaja tarehe ambayo hailingani na tarehe halisi ya kukamatwa kwake kulingana na rekodi za mahakama alikamatwa tarehe 29 Julai, 2019
 
Alimfirimba nani? Sisi tuko hai wakati yeye amekuwa chakula cha minyoo kuanzia 27/ 03/ 2021.

Endelea kumuabudu marehemu, misukule nyie akili zenu aliondoka nazo
Yale yale anayoyakataa Kiranga una uhakika Magu alikufa tarehe hiyo uliyoitaja.

Pamoja na kwamba uko hai nakuhakikishia wewe hata ukifa 2100 utasahaulika mapema kuliko yeye aliyekufa 2021 na hutamfikia hata 1/1000 ya mazuri aliyoyafanya.
 
Mimi pia nimejaribu kupitia kitabu. Kuna matukio kadhaa ambayo Kabendera ameyakosea tarehe. Kwa mfano, anaelezea tukio la kukamatwa kwake na kutaja tarehe ambayo hailingani na tarehe halisi ya kukamatwa kwake kulingana na rekodi za mahakama alikamatwa tarehe 29 Julai, 2019
Hiyo 29 Julai ni ya Kabendera kukamatwa au kufikishwa mahakamani?

Utajuaje Kabendera kakosea na si mahakama imekosea?

Naona hata gazeti la Mwananchi limeandika Kabendera alikamatwa Julai 29.

Rekodi zipo sawa alikamatwa julai 29, 2019. Mahakamani kafikishwa 05/08/2019
 
Rekodi zipo sawa alikamatwa julai 29, 2019
Kwa hiyo kakosea mpaka tarehe aliyokamatwa yeye mwenyewe?

This book needs a second edition, fast.
 
Hiyo ndiyo maana ya uandishi. Hilo kosa kidogo halibatilishi kwamba Sokoine alikufa. Tubaki kwenye reli,

Tanzania ilitawaliwa na Kichaa kuanzia mwaka 2015 hadi 2021. Asante Mungu kwa kumtupa Magufuli jehanam
Iyo dp apo alinifurahishaga san uyo mwamba 🤣 pmj na ukichaa aliokuwa nao jiwe bado mwamba hakumuogopa ata kdg 🤣
 
Disclaimer: This thread will contain some spoilers from the book ""In The Name Of The President: Memoirs Of A Jailed Journalist".

Naam,

Nasoma kitabu cha Erick Kabendera "In The Name Of The President: Memoirs Of A Jailed Journalist".

Kwa wanaonijua, mimi si mtetezi wa Magufuli, kwa hiyo uzi huu si wa kumtetea Magufuli.

Uzi huu ni wa kuhakiki kitabu. Kitabu kina mambo mengi sana ambayo yana utata, episodes za pajama, Osama kukaa Zanzibar, Magufuli kuwa responsible kwa mtoto wake kuwa na HIV, Magufuli kumpiga risasi Ben Saanane Ikulu, just to name a few.

Mimi sitayazungumzia yote hayo, nitazungumzia jambo moja tu ambalo halina utata.

Watu wote wanaojua historia wanajua Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alifariki April 12 1984.

Imekuwa vipi Erick Kabendera kaandika tarehe hiyo kama April 12 1983? Tena nilivyoona mara moja tu, nikafikiri hiyo ni typographical error tu, nikakuta karudia mara mbili, katika kurasa mbili zinazofuatana (108 na 109 in the printed book). Inaonekana ndiyo tarehe anayoifahamu.

Kitabu hakikuwa na editor? Hakikuwa na proofreader?

Leo Clubhouse (Watanganyika House) nimemsikia Absalom Kibanda akiomba msamaha kuwa alipewa kitabu kukifanyia proofreading, lakini hakukipitia vizuri, aliharakisha kukipitia, kaona kina makosa fulani ambayo yatasahihishwa katika second edition.

Nimemsikia pia Zitto Kabwe akisema kuwa kuna tatizo la timeline katika narrative ya tukio fulani.

Replays zipo "Watanganyika" Clubhouse.

Na hao ndio wahusika wachache tu waliokuwa tayari kukiongelea kitabu.

Hili linanipa swali, kama kitabu kimekosea mpaka mwaka aliofariki Edward Moringe Sokoine, je, kitabu kimekuwa rushed, hakijafanyiwa proofreading vizuri?

As much as wengine hawakumpenda Magufuli, ku rush kitabu na kufanya makosa kunawapa wanaompenda Magufuli ammunition ya kudismiss mengi yaliyoandikwa kuwa ni ya uongo.

Kabendera muandishi mkubwa kashindwa ku fact check tarehe ya kifo cha Sokoine hata kwenye Google? Proofreaders wake na editor wameshindwa pia?

Kama hili lina mushkeli, hili lililo wazi ambalo halina utata kabisa, tunaachwa tukijiuliza, mangapi yenye utata mwingi yana mushkeli pia?

Kabendera has to get not only the general narrative right, but the detail too.

Hopefully the second edition will correct this and any other inaccuracy.
JK aliwahi kusema waandishi kanjanja, hivyo ukajanjanja bado wanao
 
Hiyo 29 Julai ni ya Kabendera kukamatwa au kufikishwa mahakamani?

Utajuaje Kabendera kakosea na si mahakama imekosea?

Naona hata gazeti la Mwananchi limeandika Kabendera alikamatwa Julai 29.

Zitto pia kasema kuna story nyingine yake imekosewa timeline na na narrative.
Inaonesha kitabu kimejaa makosa madogo madogo mengi sana ambayo hayakuatakiwa kuwepo na hii inatuonyesha Kwamba hata baadhi ya mambo aliyoyaelezea ya Magufuli ya gizani pia inabidi tuanze kuyatialia mashaka kama ni ya kweli.
 
Kwanza kabisa, the book is a memoir, so by definition hii ni personal account.

Pili, suala kuwa personal hakulidogoshi validity yake. Mtu mmoja akionewa akaandika kuhusu uonevu alioupata, mwanya wa uonevu huo ukazibwa mara moja, hapo anakuwa kasaidia wengine wasionewe kama yeye. Tuangalie claim ni valid au si valid.

Tatu, mpaka kati ya personal na public issue ni mgumu kuuweka vizuri.

Mfano, ni kweli Kabendera kaongelea saana kesi yake, maisha yake, alivyoonewa yeye.

Lakini je, hiyo issue kuwa yake binafsi inamaanisha si issue ya kitaifa?

Kama watu wengi wametekwa sana, wameonewa sana, wameuliwa sana, hii issue si personal issue ya Kabendera, Kabendera ni mfano personal wa a national issue.

Nne, Kabendera kaandika mambo mengi ambayo si personal, kaandika historia ya nchi, kaandika matatizo ya kimfumo ya uongozi, kaandika matatizo ya criminal justice system. Hayo si mambo personal.
 
Hiyo ni taiping era tu mkuu ni sawa na yule waziri wa ulinzi aliyeshika binoculars kinyumenyume. Sehemu ya kutizamia vitu vilivyo mbali akaigeuza upande wa mbele. Lakini hata hivyo usiwe na shaka maana nimeshamuagiza mkuu wa mkoa hili nalo akaliangalie.
 
Inaonesha kitabu kimejaa makosa madogo madogo mengi sana ambayo hayakuatakiwa kuwepo na hii inatuonyesha Kwamba hata baadhi ya mambo aliyoyaelezea ya Magufuli ya gizani pia inabidi tuanze kuyatialia mashaka kama ni ya kweli.
Hata kama kitabu kisingekuwa na kosa dogo au kubwa hata moja ulitakiwa kutilia shaka aliyoyaeleza Kabendera kuhusu Magufuli na kutafuta ushahidi zaidi wa kutoka sehemu tofauti tofauti.
 
Hiyo ni taiping era tu mkuu ni sawa na yule waziri wa ulinzi aliyeshika binoculars kinyumenyume. Sehemu ya kutizamia vitu vilivyo mbali akaigeuza upande wa mbele
Typing error unafanya mara moja mara ya pili unapatia, hiyo ndiyo typographical error niliyoitaja.

Ukikosea mwaka aliofariki Sokoine mara mbili katika kurasa mbili zinazofuatiliana, hiyo si typo, hiyo ni timeline error.
 
Mimi ninalaani udikteta wa JPM.

Kitabu hiki ni kazi ya CCM chini ya boss wake kutafuta uhalali wa kuja kuchaguliwa tena na wananchi hapo Oktoba mwaka huu.

Magufuli ni zao la CCM, hivyo kila alichokifanya JPM kina baraka zote za CCM. Leo hatuwezi kumuweka kona moja JPM kisha tukaiweka CCM kwenye kiti kisafi. Hata huyu aliyepo naye ni mulemule ndo maana mauaji anayoyafanya yanatisha zaidi ya aliyoyafanya JPM.

Kitabu cha Kabendera ni sayansi kubwa imetumika kupitia akili ndogo lakini kimezidi kutuelimisha kwanini ni haki kuitokomeza CCM. Hapa tusijifanye tunamnanga Magufuli ambaye ni sehemu kubwa sana ya CCM kwenye kila kitu alichokuwa anakifanya.

Kibanda, Zitto ni karikenye wa kisiasa, ndivyo ninavyowaona
Maendeleo ya Tanzania bila udikteta ni magumu sana,lazima tuumie kwanza ili tufurahi baadae
 
Back
Top Bottom