Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Ndizi zinastawi zaidi kwenye kata ya lubanda
 
Unapimaje ubora kwa kuangalia uvuvi maeneo ambayo hayana uvuvi??? Mfano ukichukua mkoa wa Dodoma katika wilaya ya kondoa ambapo kuna warangi ni wazi watapata D cuz hakuna ziwa hata bwawa. Kwa hio mi naona ungepima kulingana na ubora kulingana na vitu au rasilimali zilizopo eneo husika.\
Tukienda Iramba ambako ndiko kwa Wanyiramba, umesema uvuvi ni alama "D". lakini mimi najua kuna samaki wengi tu pale kutoka ziwa kiteka na Jioni na asubuhi kuna soko la samaki pale Kiomboi!. Kwangu mimi naona D katika uvuvi kwa Wanyiramba sio sahihi.
Turudi katika uzalishaji wa chakula (mahindi), Wilaya ya Iramba inazalisha kiasi kikubwa sana cha mahindi na mikoa kama shinyanga inalishwa na mahindi ya Wanyiramba. Upande mwingine kule kagera kwa wahaya ndio kila mwaka njaa na mhaindi ya mgawo pamoja na uji wa vijiko 2 vya unga maji lita.
So far umejitahidi kuanalyse japo imekosa uhalisia.
 
Utafiti huo hauna ukweli. Mikoa ya kusini utaiachaje kwa mfano?
 
:
1: Wachaga
2: Wanyakyusa
3: Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
6: Waarusha
7: Wazanzibar (Wapemba, Watumbatu & Wahadimu)
8: Wakara
9: Waluguru
10: Wakurya
11: Waha
12: Wabondei
13: Wajaluo
14: Wasambaa
15: Wavidunda

Nawapongeza sana Wazanzibar hawanaga upumbavu huu! wee kabira gani? wao nchi yao ndio utambulisho.
 
Mkuu umesema hii ni kazi yako ya miaka 10, nakupa hongera kwa hili, naomba kujua

Mabadiliko ya tabianchi hayajaathiri utafiti wako?
In a sense kwamba kwa miaka 3 mfululizo ukaona Mkoa A unaongoza kwenye chati lakini kufikia mwaka wa tano ni Mkoa G ndiyo ukachukua nafasi.
 
Hongera mtafiti, data nzuri na kuna ukweli wa kiwango cha juu sana. Lakini pia kuna changamoto kadhaa, mfano upatikanaji wa chakula kwa wakerewe kwa miaka ya hivi karibuni ni mbaya sana na hawawezi kupata wastani wa A
 
Uko vizuri sana
 
Nashukuru sana kwa kufuatilia vyema. Changamoto niliyoipata ni kuelewa kama Ziwa dogo kama hilo limekuwa na samaki so nitaiconsider kwenye taarifa mpya.
Hata hivyo kwenye uzalishaji wa vyakula, nimewapa Wanyilamba D kwa sababu wana alternative ndogo sana ya kuliwa mazao ya vyakula kutokana na kuwa na mzima mfupi wa kilimo. Kwa kuwa eneo hilo linapata mvua chache (chini ya mm 850), limekuwa na rainfall unreliability, hivyo wanaweza kuzalisha vyakula kwa wingi but still njaa imekuwa ya mara kwa mara kulinganisha na maeneo yenye misimu mirefu ya mvua.
Mfano: mwezi unaopata mvua chini ya mm 60 kwa mwezi basi ni mwezi wenye ukame na ikiwa ni mm 30 ni ukame mkubwa, so angalia nimechukua eneo bora la Kionboi but still wana miezi sita pekee ya mvua isiyo ya ukame. Huwezi kulinganisha na maeneo yenye bi-modal.
 
Asante nitalifanyia kazi ili kwenye taarifa yangu comprehensive ninayoandaa, ndiyo nitaiweka. Pliz kama kuna Mndali mwenye mtazamo tofauti na Kata hii anisaidie ili tuque ni kata gani wako vizuri kwa uzalishaji wa vyakula hasa ndizi?
Sawa mkuu tusubiri wengine waje wataje
 
Utafiti huo hauna ukweli. Mikoa ya kusini utaiachaje kwa mfano?
Nimeiacha wapi ndugu yangu? Uchambuzi haukuhusu mikoa bali ulihusu jamii (makabila) zetu. Hebu angalia vizuri nimeweka makabila yote ya Kusini isipokuwa tu Wandonde kutokana na kukosekana nafasi.
Sema makabila hayo hayaja-perform vyema kulingana na vigezo hivyo.
Mfano ukiangalia mvua huko inanyesha yenye zaidi ya mm 60 kwa miezi mitano hadi Sita pekee na miezi mingine yote ni ukame tu. Pia udongo wake hauna rutuba kama let's say kwenye maeneo ya volkano. Angalia huko kuna malaria ni endemic (ya kurithi) kutokana na kuwa chini ya mita 1000 kutoka usawa wa bahari. Mbu wanapenda sana joto. Vilevile, angalia huko kuna mbung'o wengi inayoeneza magonjwa ya malale (kwa binadamu) na nagana (kwa mifugo). Je huko kuna ufugaji mkubwa wa ng'ombe kama mikoa ya kati?
Fuatilia kwa utulivu ndugu, utaviona vyema hivyo vigezo.
 
Nawapongeza sana Wazanzibar hawanaga upumbavu huu! wee kabira gani? wao nchi yao ndio utambulisho.
Ndiyo maana ukiangalia vigezo vyangu sikutaka kuangalia vigezo vya sasa. Nine huku a vigezo hivyo kihistoria. Ndiyo maana mwanzoni nilitoa angalizo nikitolea mfano wa Kabila la Wakwere kuwa Lina maeneo manne yaliyoendelea - Bagamoyo, Chalinze, Mlandizi na Kibaha, so usipokuwa pia makini utajikuta unachagua mojawapo ya maeneo hayo lakini Mimi nimechagua Tarafa ya Yombo kuwa ndiyo bora kiasili kuwakilisha Wakwere. Nenda usukumani, kwa nini sikuchagua Mwanza ama kwa Wazaramo Dar es Salaam ama Wasafwa Mbeya? Sikubabaishwa na maendeleo ya sasa, nilichagua kwa kuangalia kihistoria eneo bora kabla ya kuja utamaduni wa kikoloni nchini.
Maeneo niliyochagua kwa kila kabila ndiyo yenye uwezo wa kutoa watu wenye akili zaidi kwa Kabila husika. Lengo ndilo hilo kama nimekosea tusaidiane ili niboreshe kazi hiyo.
 
Hongera mtafiti, data nzuri na kuna ukweli wa kiwango cha juu sana. Lakini pia kuna changamoto kadhaa, mfano upatikanaji wa chakula kwa wakerewe kwa miaka ya hivi karibuni ni mbaya sana na hawawezi kupata wastani wa A
Yes, nakubaliana na wewe, utafiti huu haujaangalia mazingira ya sasa, kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi tangu miaka ya 1990s. Niliwahi kuambiwa kuwa, Ukerewe haikuwahi kukumbwa na njaa tangu kuwepo kwake lakini kwa mara ya kwanza walianza kupokea cha kula cha misaada miaka ya 2010 baada ya zao Lao la mihogo kuharibiwa na ugonjwa tangu miaka ya 2003. So sijazingatia matatizo ya sasa maana yatakufanya usijue eneo ambalo limekuwa bora kihistoria.
Mfano kwa sasa, Mkoa wa Kagera nao umekumbwa na tatizo la mnyauko wa migomba na limewaathiri sana Wahaya na kulazimika kula chakula ambacho hawakuwahi kukitegemea. Naambiwa miaka ya 1970, Kagera pekee ilikuwa inazalisha kiasi cha asilimia 70% ya ndizi zote Tanzania but nowadays they are almost nowhere to be found, very very and very very sad story in our country. Ni story ya nchi nzima so nilikuwa makini kuignore effects za mabadiliko ya tabianchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…