Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Inakuwaje mbona Wachagga mnapenda kuwa A A sana na kila kitu kizuri wanakuwa wa kwanza kwanza?? Kuna nini uchaggani??
 
Mbona sijaona wandali hapo na waona walambya. Wakati kila mwaka nawasaidia chakula
Wandali wapo ndugu na ninawafahamu vyema ni bahati mbaya tu hawakupata average ya A but wana wastani mzuri sana wa B kuelekea A. Cheki karibu na Wahangaza eneo lenye watu 320,000 utawaona. Na hata ukiwalinganisha na Walambia, utagundua utofauti wao. Halafu unipe uzoefu wako wa huko kwenu Ileje kama nitakuwa niko sawa. Pia nitaomba unisaidie kama Kata ya Mlangali ndiyo bora kwa Wandali ama kulikuwepo nyingine bora zaidi, mfano ile ya Masoko?
 
Mlangali sio bora hapo chukua kata ya sange ua ya lubanda
 
Kuongelea habari za kabila bilakutoa kipimo cha kupata kabila ni upumbavu.

Unapimaje hawa ni watu w akabilagani, wanaanzia wapi na kuishia wapi, wamehamahama vipi katikamuda upi, wamechanganyikanaje na wengine,na kuchanganyika huko kumeathirije dhana nzima ya kabila lao?

Siku hizi watu wanahamahama sanakufuata maisha mazuri zaidi, Wamasai wamekuja mpaka Morogoro na Pwani.Wasukuma wamefika mpaka Ufipa na Zambia.

Utawekaje habari za uchunguzi kwa data kwa kuangalia makabila?
 
Inakuwaje mbona Wachagga mnapenda kuwa A A sana na kila kitu kizuri wanakuwa wa kwanza kwanza?? Kuna nini uchaggani??
Ndugu unajua kinachosababisha mwanadamu awe na afya nzuri ni chakula chenye lishe, pamoja na kutokuwepo kwa magonjwa. Sasa kama umesoma jiografia utagundua kuwa vyakula vinasitawi vizuri sana kwenye maeneo yenye hali nzuri ya hewa - yaani mvua nyingi (hasa mm 1500 - 2000) na joto la kadri; udongo wenye rutuba na kutokuwepo kwa magonjwa hatari.
Kwenye hali ya hewa (mvua nyingi na joto la kadri) nchini, Miteremko ya Kilimanjaro inazidiwa na Rungwe na Bukoba pekee. Hata hivyo Miteremko hiyo inaizidi Rungwe na Bukoba kwa sababu kuna hali za hewa nyingi ndani ya eneo dogo linaloweza kuivisha mazao ya kila aina yanayoweza kuhimili baridi kali, ya kawaida, joto la wastani hadi joto jingi, pamoja na mvua nyingi sana (zaidi ya mm 1700 - Uri) nyingi (1500 - Marangu) ya kawaida (mm 1100 Siha) na chache (mm 800 - Mossi) na pakame kabisa (mm 500 - Kahe).
Eneo lote kuanzia Uri (mm 1700) hadi Kahe (mm 500) ni chini ya km 20. Huu ni umbali mdogo sana lakini ume-cover hali zote za hewa za Tanzania, hivyo kila zao linalolimwa hapa Tanzania linalimika kwenye Miteremko ya Kilimanjaro. Aidha, utofauti wa mwinuko (altitudes/relief) kati ya makazi ya juu kabisa (Marangu Magharibi mita 1800) hadi chini kabisa Kahe (mita 800) ni mita 1000. Hakuna sehemu nyingine barani Afrika yenye eneo lenye tofauti kubwa ya mwinuko kama huo ndani ya umbaliwa wastani wa km 20 tu.
Hiyo ni kitu kikubwa sana.
 
Wanyakyusa ni balaa. Mungu aliwajalia Kanda mbili tofauti kabisa za hali ya hewa:
  • Rungwe: Huku kuna baridi na mvua nyingi sana. Wanaishi kwa kutegemea zaidi ndizi.
  • Busokelo: Huku kuna baridi pamoja na joto la kadri. Wanaivisha ndizi na mikakao pia.
  • Kyela: Huku kuna joto na wanalima sana mpunga. Matunda pia ndio kwao. Ndizi pia zipo kibao. Ni wavuvi pia.
Ndicho kinachowafanya wawe na akili sana maana wanapata vya kula vya aina zote. Ukivikosa kwao, ni nadra kuvipata kwa makabila mengine.
Hakuna kabila lingine lililobarikiwa eneo kubwa lenye hali ya hewa na udongo wenye rutuba kama Wanyakyusa.
Baada ya Wanyakyusa, ndio wanafuatia Wahaya, bahati mbaya eneo la Wahaya halina rutuba kubwa kama maeneo yenye udongo wa volcano.

Rukwa rutuba tele
 
Wamasai umeandika wapo 300,000 wakati kwa mwaka 2011 walikuwa zaidi ya laki nane.

Mhmhmh!.
 
Mbeya na Kilimanjaro. Kweli hali ya hewa ina play role kubwa.
Ni kweli ndugu, kitendo cha vizazi na vizazi vya makabila kuwa vinakula vyakula vingi na vya aina nyingi ndio vimepelekea wawe na akili nyingi (za darasani).
Watu wengi kwa kutojua huwa wanakimbilia visababu vyepesi vyepesi eti maeneo hayo yameendelea kielimu kutokana na wakoloni kupendelea maeneo hayo kimiundombinu. Sasa, kama suala ni miundombinu, leo hii ni eneo lipi linatoa wasomi wanaofanikiwa sana katika elimu ya juu ya udoctorate kati ya manispaa za Mtwara, Lindi, Singida, Dodoma, Tabora na Shinyanga, dhidi ya Vijiji vilivyoko Rungwe, Kyela, Busokelo, Ileje, Ngara, Nyasa, Mbinga, Ukerewe, Ukara, Buhigwe, Arumeru, Rombo na Tarime?
Ask yourself.
 
Mlangali sio bora hapo chukua kata ya sange ua ya lubanda
Nashukuru sana kwa ushauri wako. Nitaufanyia kazi. Hata hivyo kwa kuwa, sijawahi kufikiri Ileje personally, nieleze ni kata gani ambako ndizi zimekuwa zikistawi zaidi kuliko nyingine?
Halafu uwe makini, usifuatilie sana ukuaji wa miji maana itakuchanganya ukashindwa kuelewa eneo bora la kiasili kwani miji imekuja tu Hivi karibuni. Very thanks.
 
Kuongelea habari za kabila bilakutoa kipimo cha kupata kabila ni upumbavu.

Unapimaje hawa ni watu w akabilagani, wanaanzia wapi na kuishia wapi, wamehamahama vipi katikamuda upi, wamechanganyikanaje na wengine,na kuchanganyika huko kumeathirije dhana nzima ya kabila lao?

Siku hizi watu wanahamahama sanakufuata maisha mazuri zaidi, Wamasai wamekuja mpaka Morogoro na Pwani.Wasukuma wamefika mpaka Ufipa na Zambia.

Utawekaje habari za uchunguzi kwa data kwa kuangalia makabila?
Ndugu unasema kweli kuwa, kwa sasa kuna mchanganyiko mkubwa wa watu wa makabila mbalimbali kiasi kupunguza sana asili na mipaka ya makabila hayo. Hata hivyo kuchanganyikana huko hakujapoteza uasili wa makabila kamwe. Hata hapa Dar ambako ni jiji la wote, bado huwa inaonyesha wazi Wazaramo na Wandengereko ndio wanaotia fora jijini. Kama hali ni hiyo, vipi huko mikoani?
Halafu kuingiliana huku kumeanza hasa baada ya kuingia kwa wazungu wakoloni, kiasi cha miaka 130 iliyopita. Miaka hii bado ni michache kulinganisha na miaka ambayo makabila yalijiumba tangu kuingia kwao hapa nchini kuanzia Karne ya 11.
Swali, je waafrika wako barani America tangu Karne ya 16, je wameshakuwa wazungu ama bado ni black, ask yourself. Intermingling na intermarriage haiwezi kuharibu asili ya kabila ndani ya kipindi kifupi, itachukua muda mrefu kwa makabila kuwa irrelevant. Labda suala hilo limewezekana zaidi Zanzibar ambako Watumbatu na Wahadimu wamemezwa na tamaduni zilizoingia visiwa humo miaka mingi iliyopita na zaidi hasa baada ya Sultan Seyyid Said kuhamishia makao ya visiwani humo mwaka 1840.
 
Nimekusoma mkuu wew ni mchaga tena wamarangu sio bure
No mimi siyo mchaga na hakuna haja ya kujitambulisha ili nisiwachanganye wachangiaji na kujikuta wanaingiza bias. Nawaomba tu kila mtu afuatilie vyema Kabila Lake halafu anikosoe kitu chochote nipate kumjibu nikikosa jibu, basi watanisaidia wanaotokea maeneo hayo husika.
 
Ndugu unasema kweli kuwa, kwa sasa kuna mchanganyiko mkubwa wa watu wa makabila mbalimbali kiasi kupunguza sana asili na mipaka ya makabila hayo. Hata hivyo kuchanganyikana huko hakujapoteza uasili wa makabila kamwe. Hata hapa Dar ambako ni jiji la wote, bado huwa inaonyesha wazi Wazaramo na Wandengereko ndio wanaotia fora jijini. Kama hali ni hiyo, vipi huko mikoani?
Halafu kuingiliana huku kumeanza hasa baada ya kuingia kwa wazungu wakoloni, kiasi cha miaka 130 iliyopita. Miaka hii bado ni michache kulinganisha na miaka ambayo makabila yalijiumba tangu kuingia kwao hapa nchini kuanzia Karne ya 11.
Swali, je waafrika wako barani America tangu Karne ya 16, je wameshakuwa wazungu ama bado ni black, ask yourself. Intermingling na intermarriage haiwezi kuharibu asili ya kabila ndani ya kipindi kifupi, itachukua muda mrefu kwa makabila kuwa irrelevant. Labda suala hilo limewezekana zaidi Zanzibar ambako Watumbatu na Wahadimu wamemezwa na tamaduni zilizoingia visiwa humo miaka mingi iliyopita na zaidi hasa baada ya Sultan Seyyid Said kuhamishia makao ya visiwani humo mwaka 1840.
Umechanganya madawakibaohalafu swalilangu la msingihujajibu.

Unatumia kipimo gani kusema huyu ni kabila fulani?

Maana unaweza kusema Mwalimu Nyerere ni Mzanaki, kwa sababu Baba yake Chifu Burito ni Mzanaki,kumbe Chifu Burito wala si Baba yake Mwalimu Nyerere.

Mama Mgaya alikimbia kutokacourt ya Chifu Burito,akakimbilia kusini kuelekea Mwanza,hukoakakutana na Msukuma, akatunga mimba ya Mwalimu Nyerere, halafu baada ya muda,akarudi kwa Chief Burito.

Na Chifu Burito alivyokuwa na wake wengi hata hakujua. Na zaidimila zao hazihesabu mtoto kwa baba, zinahesabu mtoto kwa mama na mjomba.

Sasa wewe unapimaje kabila?

Unatumia DNA?
 
Rukwa rutuba tele
Sawa nitaifanyia kazi hii ya rutuba, niangalie ukweli wake. Hata hivyo kwa uelewa wangu inaweza nikachelewa kupata kitu kipya kwangu so nitawaomba wafipa, Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyika, muchangie ukweli wa taarifa hii juu ya rutuba mkoani Rukwa na hata kwa Wapimbwe, Wabende, Wakonongo, Warungwa, Watonga, Waholoholo na Wabemba wa Katavi, kuchangia juu ya rutuba mikoani huko.
 
Umechanganya madawakibaohalafu swalilangu la msingihujajibu.

Unatumia kipimo gani kusema huyu ni kabila fulani?

Maana unaweza kusema Mwalimu Nyerere ni Mzanaki, kwa sababu Baba yake Chifu Burito ni Mzanaki,kumbe Chifu Burito wala si Baba yake Mwalimu Nyerere.

Mama Mgaya alikimbia kutokacourt ya Chifu Burito,akakimbilia kusini kuelekea Mwanza,hukoakakutana na Msukuma, akatunga mimba ya Mwalimu Nyerere, halafu baada ya muda,akarudi kwa Chief Burito.

Na Chifu Burito alivyokuwa na wake wengi hata hakujua. Na zaidimila zao hazihesabu mtoto kwa baba, zinahesabu mtoto kwa mama na mjomba.

Sasa wewe unapimaje kabila?

Unatumia DNA?
No nimeshaelewa concern yako, na mimi nakubaliana na wewe kuwa, kamwe haijawahi kutokea na haitatokea taifa, jamii, kabila, ama ukoo ambao ni 100% homogeneous. Hakuna sehemu yoyote, hata Wajerumani ambao waliwahi kupropagate kipindi cha Fuhrer Hitler kuwa wao ni super race (master aryans), nao walikuwa na mchanganyiko tu wa watu wasio Teutonic.
Hata hivyo, kwa kuwa kila Kabila lina watu wanaoolewa na wanaoozwa, basi wanaoolewa wanaingizwa kwenye utamaduni wa eneo hilo so tofauti siyo kubwa kihivyo. Ndiyo maana kwa mfano sisi tuliotokea kijijini, utakuta kijiji kila wastani wa wakazi 5,000 halafu kwa mwaka utakuta kuna wa harusi kumi, ambapo tuseme nusu wanao na nusu wataolewa. Kati ya wale nusu waliooa (5) utakuwa nusu ni wa Kabila hilo na nusu wa nje (2). Sasa watu wawili tu kuingia kwa mwaka imeharibu nini kwenye hicho kijiji?
 
Wamasai umeandika wapo 300,000 wakati kwa mwaka 2011 walikuwa zaidi ya laki nane.

Mhmhmh!.
Sorry nimeichukua kwenye rekodi za Joshuaproject.net ambalo nilicunter check Hivi karibuni nikakuta wengi wa wanadai amewaweka kwenye kundi la Wamasai waBaraguyu
 
Back
Top Bottom