Kabla hujakopa ama kukopeshwa na app za mitandaoni elewa yafuatayo

Kabla hujakopa ama kukopeshwa na app za mitandaoni elewa yafuatayo

Hypersonic

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2012
Posts
829
Reaction score
1,564
Wanajamvi kufuatia mkopo aliyokopa mdogo wangu kwenye APP za mitandaoni nami kujikuta muathiriwa kwa kuwa namba yangu imo kwenye simu yake, hivo basi natamani mfaham yafuatayo:-
Application Date 13/02/2024
Due Date 19/02/2024
Platfoam Fee 45500TZS
Amount Receivable 84500TZS
Repayment 182,000 TZS
Wallet Type TIGO
Day Overdue 8Days
Overdue Amount 455000TZS.

Hapa ndo mchezo ulipo Ukichukuwa Platfoam Fee + Amount Receivable = 130000. ( Deni linahesabika umepokea laki na 30, ili hali kiuhalisia umepokea 84500/= Wao wanabaki na 45500 ( pengine ni sawa kwa sababu hata baadhi ya benki huwa wanachaji service charge na Insuarance)

Baada ya siku ulizojicomit kupita huyu mtu wangu yeye aliweka siku 8 unatakiwa urudishe 182,000. Riba 52,000 ndani ya siku nane.

Ukichelewa siku moja manake kuanzia siku ya tisa una faini ya 45500TZS.

Uhalisia umedanganywa, umekopa 84,500 unatakiwa urudishe elfu 84500 na ziada ya shilingi 97500. Faida yao ni zaidi ya asilimia moja.

Hapo ni endapo utarudisha kwa wakati ndani ya siku 9 unatakiwa 143,000 TZS katika mkopo wa 84.5K. Wataalam wa mahesabu mtanisahihisha labda hasira imezidi sielewi.
 
kwanza kwann ukope alfusamanini ni uzwazwa alafu unalipa laki na kitu ndio uzezeta kabisaaaaaaaaa.....

sikatai kuna kukwama ila kama huna mtu wa kukupa alfu samanini kwenye mzunguko wa watu ulio nao basi ww ni useless na hopeless...
 
Wanajamvi kufuatia mkopo aliyokopa mdogo wangu kwenye APP za mitandaoni nami kujikuta muathiriwa kwa kuwa namba yangu imo kwenye simu yake, hivo basi natamani mfaham yafuatayo:...
Ni wapi umeomba wakakupa mkopo? Loan apps ni scam! Ni matapeli hakuna cha hela wala nini! Uenda mleta uzi ni mmojawapo wa hao anatafuta wa kuwapiga
 
Habari ndugu mdhamini ama jamaa wakaribu wa ndugu xxxxx. Xxxxxi miaka ( 00)mwenye no, 07xxxxxxxx..Ni tapeli amekopa kiasi cha shillingi.Xxxxxxxxx0.Kutoka kampuni ya pesa m loan.Anataka kutapeli, apokei simu anatoa ahadi za uongo, ukiwa kama mtu wake wa karibu tunaomba umuambie alipe deni lake kabla hatujaanza kumpost yeye na vitambulisho vyake na kuchukua hatua nyingine juu yake tunaomba umfikishie ujumbe huu ndani ya nusu saa atapata taarifa nyingine za kisheria zaidi ya hizi
 
Nyingine hii hapa

Habari!..samahani Kwa usumbufu,kama mtu wa karibu nilikuwa nakuomba uwasiliane na "XXXXXX XXXXX" wa namba 0XXXXXXXX , utusaidie kumwambia afanye rejesho la mkopo wake wa kampuni ya "CREDIT LAND" maana huku kwetu hapokei simu ,....Asante
,Mimi ni Afisa mkopo!!!
 
Uhalisia umedanganywa, umekopa 84,500 unatakiwa urudishe elfu 84500 na ziada ya shilingi 97500. Faida yao ni zaidi ya asilimia moja.
Mkuu, There is no such thing as a Free Lunch.

Ukiacha utapeli wa wakopeshaji ila bado NJAA na Umasikini ndio vinapelekea matatizo yote hayo. Japo kubwa zaidi ni UJINGA.

LINGINE, Nafikiri wanaweka riba kubwa kwasababu wanakuwa wamechukua RISK kubwa sana pia, kukupa hela bila dhamana yoyote ni RISK kubwa sana.

Ukizingatia Watanzania wakikopa huwa wanawaza njia za kukimbia deni na kutolipa, hii ni tabia ya kishenzi sana. Kumkopesha hela mtanzania ni sawa na kununua ugomvi usio wa lazima. Edit; Comment No 16 itumike kama Mfano

NA WASHENZI NASIKIA WANADAI KISAWASAWA, YANI VURUGU MECHI, wasingedai hivyo naamini wasingelipwa kabisa.
 
Ni wapi umeomba wakakupa mkopo? Loan apps ni scam! Ni matapeli hakuna cha hela wala nini! Uenda mleta uzi ni mmojawapo wa hao anatafuta wa kuwapiga
Usikulupuke soma vizuri uelewa sijakwambia ukakope ukitaka nenda for your own Risky. Mimi nimekumbana na hiki kisanga kwa sababu mdogo wangu kwa kushawishiwa na wenzake alijukuta kaingia huo Mkenge.

Mimi nimeajua hawa watu kufuatia sms wanazotuma kwa sababu mtu akishakopa wao huingia kwenye simu ya mkopaji na kupigia kila mtu aliyekuwa saved kwenye phone book.

So kama una akili chukuwa hili somo kuliko kujifanya mjuaji. Ni hayo tu.
 
Nyingine hii hapa

Habari!..samahani Kwa usumbufu,kama mtu wa karibu nilikuwa nakuomba uwasiliane na "XXXXXX XXXXX" wa namba 0XXXXXXXX , utusaidie kumwambia afanye rejesho la mkopo wake wa kampuni ya "CREDIT LAND" maana huku kwetu hapokei simu ,....Asante
,Mimi ni Afisa mkopo!!!
Aisee hawa watu wanakera alafu unakuta mtu hata hujui huyo mtu alikopa lini na wapi
 
Usikulupuke soma vizuri uelewa sijakwambia ukakope ukitaka nenda for your own Risky. Mimi nimekumbana na hiki kisanga kwa sababu mdogo wangu kwa kushawishiwa na wenzake alijukuta kaingia huo Mkenge. Mimi nimeajua hawa watu kufuatia sms wanazotuma kwa sababu mtu akishakopa wao huingia kwenye simu ya mkopaji na kupigia kila mtu aliyekuwa saved kwenye phone book. So kama una akili chukuwa hili somo kuliko kujifanya mjuaji. Ni hayo tu.

Mdogo wako HAMNAZO, kopa ulipe
 
kwanza kwann ukope alfusamanini ni uzwazwa alafu unalipa laki na kitu ndio uzezeta kabisaaaaaaaaa.....

sikatai kuna kukwama ila kama huna mtu wa kukupa alfu samanini kwenye mzunguko wa watu ulio nao basi ww ni useless na hopeless...
MAISHA SIO RAHISI... KAMA WEWE UNAO WA KUKUAZIMA HELA TULIA TU HAPO HAPO USITIKISIKE SANA UTAJISAHAU MWISHO UBWAGE CHINI.
 
Dah siku hizi wanaingia kwenye phone book wanatumia Meseji Ndugu zako, nimeshapokea meseji kadhaa. Yaani kumpa mtu namba siku hizi jiulize mara nyingi sana. Sijawahi kumdhamini MTU
Nasikia unavo install unatakiwa accept phonebook yako waisome ndohapo wanapata namba za simu yako..
 
Pamoja na yaliyowakuta TALA na BRANCH bado hizi kampuni zinarudi bongo tena? Sema nn, ukitaka kukopa futa namba zote kwenye phonebook weka namba ambazo hazipo halafu kopa ili kila wakitaka kuanza kusambaza sms kwa ndugu na jamaa ziwe zina bounce.
Nice idea.unasajili lain mpya na fake number tu.
 
Pamoja na yaliyowakuta TALA na BRANCH bado hizi kampuni zinarudi bongo tena? Sema nn, ukitaka kukopa futa namba zote kwenye phonebook weka namba ambazo hazipo halafu kopa ili kila wakitaka kuanza kusambaza sms kwa ndugu na jamaa ziwe zina bounce.
Kianzio wanakukopa shingap?
 
Back
Top Bottom