Kabla ya kukubali kuoa ama kuolewa na mtu inapaswa muwe na maongezi marefu kuhusu engo zote za maisha
1. Jadilini kuhusu bilis za maisha atakuwa anazilipa nani na kama mtalipa wote ni kwa mgawanyo gani, usiingie kwenye ndoa kimya kimya ukiwa na expectations za mimi mwanaume nitakuwa nadili na mambo makubwa ya ujenzi wa nyumba ama kununua magari na wewe mwanamke utakuwa unalisha familia. ni lazima mjadiliane mapema kabla hamjafunga ndoa.
2.Mitindo ya malezi, maana kuna watu wanapenda malezi ya kizungu na wengine wanapenda malezi ya ukizingua ni viboko
3. Mtazamo kuhusu mikopo. maana kuna watu wanapenda kukopa na kuna watu hawapendi kukopa lazima mjuane kila mmoja yupo upande gani
4. Madeni ya nyuma mliyonayo. ni vizuri ukajua mwenza wako kama anadaiwa kiasi gani kabla hamjafunga ndoa
5. Jadilini kuhusu imani za kidini, maana mtu anaweza kuwa KKKT ila anapenda mikesha ya manabii. ili kwenye ndoa usishangae atakapokuwa anaenda mikesha hiyo. msigombane
6. Jinsi ya kushughulika na familia zenu yaani wakwe na mawifi na hata kuishi na ndugu .
7. Imani gani itawekwa kwa watoto wenu
8. Trauma za utotoni ambazo umepitia ili mwenza asikushangae kipindi una Anxiety ama uoga wa jambo fulani
9. Matarajio ya Tendo la ndoa ama sex. kama umezoea kula tigo ama kuliwa tigo ni vizuri mwenza wako ajue mapema ili asishangae uwanjani
10. Matarajio kwa mwenzi, vizuri ukamueleza mchumba wako kwamba una expect nini kutoka kwake kwenye ndoa
11. Matarajio ya kifedha. ni vizuri kujadili views zenu kwenye maswala ya utafutaji pesa na hata utumiaji pesa. kuna watu wanapenda simple life na kuna watu wanapenda life lenye heka heka za utumiaji pesa kuanzia harusi tu anataka ya kutrend instagram .
12. Historia ya afya ya familia zenu. msifichane hili lina umuhimu mkubwa.
13. Historia ya afya ya akili. muhimu pia kujadili hili ili mwenza wako akuelewe ajue jinsi ya kudili na wewe ukivurugwa kuepusha mauaji ama divorce
14. Orodha ya ndoto zenu. ni lazima muambiane ndoto zenu mapema. ili mwenza asishangae kipindi unafanya jambo fulani. mfano unaacha kazi Bank na kwenda kujiajiri Sokoni mwenza asipige kelele za ajabu
14. Makazi ya familia yawe wapi ? hii muhimu sana kujua base yenu itakuwa wapi.. maana isije kuwa mke anapenda kuishi dar es salaam na mume anapenda kuishi morogoro ama mwanza. ikaja leta makelele
15. Kazi na elimu zenu ni muhimu muambiane ukweli. isije kuwa mwenza anajua anaolewa na professa mtarajiwa kumbe mume huna malengo hayo ya kielimu na hata ka certificate ka amazon college huna
16. Jadilini kuhusu maoni ya kisiasa na chochote kingine kinachokuja akilini maana Upendo HAUTOSHI.
View attachment 2936439