Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

Dstv compact sasa tunacheck laliga na EPL kwa sh 83500 tu,me haya makampuni mengine nilijua yatakuwa uzushi tu kuja kujaza madishi nyumba zenyewe za kupanga.Dstv Mdogo Mdogo Mpira naomba waulete walau mpaka Family bouquet.
 
Unapozungumzia kituo cha televisheni Tanzania kinacholeta mapinduzi katika biashara ni AZAM. Aisee hawa jamaa wako vizuri kuanzia uandaaji wa vipindi, studio za kisasa, picha zake HD hata katika uandaaji na uwasilishaji wa habari kwa mtazamji. Tanzania hakuna kituo cha televisheni kinachotumia camera ya anga au aerial kwa jina rahisi camera ya ndege/helkopta.

Hawa jamaa wanajua biashara sio mchezo, supersport pamoja na ubora wao wote lakini wameshindwa kufurukuta mbele ya Azam katika haki ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya Uganda.

Wachezaji wetu walikuwa wanapata tabu kukusanya taarifa zao pindi wanapoitwa nje ya nchi kufanya majaribio. Ilikuwa ngumu sana kujua taarifa za mchezaji, hii ikapelekea mpaka wachezaji wetu kukosa nafasi za kucheza nje ya nchi.Leo wakiojiwa wachezaji wetu wanaelezea kwa kicheko kwamba Azam imewarahisishia kupata taarifa zao husika.

Azam anadhamini ligi kuu ya Tanzania, kituo pekee kilichotoa pesa nzuri ya udhamini kwa vilabu kuliko vituo vingine vyote vilivyo wahi kudhamini. Ujio wao ni neema kwa vilabu maskini kama majimaji,mgambo n.k

Azam bado ana nafasi katika uboreshaji wa changamozo zinazomkabili kama walizotoa wadau hapo juu, maana hata DSTV kashusha bei ya vifurushi vyake kutokana na ushindani wa kibiashara anaopata kutoka kwa visimbusi vingine kama Azam.

Mwaka jana boss wa FRANCE 24 alitembelea studio za Azam alishangaa kuona mitambo ya kisasa ya Azam, nanukuu alivyosema."Azam upande wa vifaa mmeifikia teknolojia wanazotumia ulaya, mnachotakiwa kuboresha vipindi na viwe vya kisasa"

AZAM KAMA KITUO CHA TELEVISHENI CHA KIZALENDO BADO ANA NAFASI TANZANIA, HIZO ZINGINE NI CHANGAMOTO.
 
TATIZO LA WABONGO WAKIPATA MATTAKO HULIA MBWATA..HUYO DADA UTAKUTA ANALIPWA LAKI TATU MMMAE ZAKE NA MAPOUZI KIBAOO WANJA UMEMJAA MDOMONI UTADHANI KANYWA DAMU ..MM WANANIUDHI WATU WENYE MAPOZI NA KAZI ZA WATU
 
Mwaka jana boss wa FRANCE 24 alitembelea studio za Azam alishangaa kuona mitambo ya kisasa ya Azam, nanukuu alivyosema."Azam upande wa vifaa mmeifikia teknolojia wanazotumia ulaya, mnachotakiwa kuboresha vipindi na viwe vya kisasa"
SASA KWA NINI HAWABORESHI?
mimi nimekasirika sana nilikuwa nishajipanga naenda kununua azam kumbe ni maboya tu...dah!1 boresheni na wasikilizeni wateja wanataka nini sisi mnatujazia machaneli ya kihindi ili iweje? wahindi wenu wawekeeni ila na sisi wekeni kile roho inappenda la sivyo tutawarudisha kwenu omani/zanzibar
 
mdau tununue kipi sasa ? star times au dstv
 
Dstv ...yes ni nzuri kakini expensive
Azam....inakwenda vizuri tuwape muda
Azam.... wanazo OB van za kisasa kabisa ktk kanda zote na the best srudios south of sahara.
Time is the best nedicine
Hizo ob van na studio za kisasa ni zao wala hazinisaidii chochote, mi nataka channel za maana we unaongelea mambo ya studio za kisasa
 
Pumba tupu, ligi ya Uganda nani anaitaka?Studio zao zinanisaidia nini mimi?
 
kumbuka chaneli ambazo huzipendi wengine tunazipenda like indian movies i like bollywood more
 
kuna vifurushi vingi. kwa hiyo ongeza mtonyo upate more. like me am enjoy la liga there have more competition
Hujui unachokisema ww, channel zake eti etv, MBC 2,3,4, wao ni kuonyesha movie za zamani afu full kuzirudia, eti fox, Mara full wahindi ona aibu aisee
 
Inaonekana wewe ni msemaji wa Azam pia kumbuka azam wanatumia camera nzur ila sio HD! pili hatutaki studio nzur tunataka Huduma bora sio kutuwekea Chanel kibao za kihindi!
channel ziwe kwenye mpangilio sio moja huku nyingine Kigoma!
 
mdau tununue kipi sasa ? star times au dstv
Fanya utafiti mkuu jarib kuangalia Zuku, cmntiental au Digitek ila jiridhishe kwanza kabla hujanunua! lengo la Uzi huu ni usijenunua then ukajuta!
 
Kiukweli, bado DSTV ni bora kuliko watoa huduma wengine.
 
af nasikia usipolipia wanakata hadi channel za ndani aisee wakat mi startimes mwaka sasa sijalipia na kula channels za ndani mpk rahaa
Huu uongo mwingine hauna tija, niba azam tv sijalipa toka juni mwaka jana na napata channel zote, muda mwengine huwa wanatoa ofa kwa channel za bure kuangalia ht km hujalipia
 
Azam hamna kitu kabisa wakuu, wamenikera sana kukata channel za ndani pale kifurushi kinapoisha! Wanabakiza tbc 1 tu! Nimerudi Startimes
Mpango mkakati huu, uongo mzuri sana huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…