Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

Ukitoka peleka invoice dstv wakulipe kwa matangazo yako...
Kuna jirani yngu juzi aliamua kung,oa Dish la Azam kapachika Dstv kwa sabb ya hizo figisu figisu zao,,

Kwani Azam sio Local Channel kwann wanakata usipolipia,,
Kweli wengi watakimbia huku kwenye Chapati.
 
wakati Azam wanaanza kutoa huduma walitoa na vipeperushi wakionyesha channels za bure na za kulipia lakini jambo la kushangaza baada ya muda wa malipo kuisha na wiki tatu kupita walikata hata zile walizotuambia kwenye vipeperushi ni bure! sikuelewa wapi nipeleke malalamiko maana ilikuwa kama utapeli wa kibiashara. niliama kutoka Azam maana sikuona mantiki ya kulipia ITV, tbc na hata aljezira na channels zote ambazo ni bure. Mwezi wa kwanza mwishoni nlirudisha Azam na kifurushi cha pure kimekwisha nasubiri week tatu nione kama watakata hizi ambazo ni za bure kisha niuze hiki king'amuzi chao na kama yuko mtu anapenda ajiandae tufanye biashara
 
Nimatumaini yangu kuwa wengi ni buheri wa afya na manaendelea vema na majukumu ya kila siku! .....Ukweli kuwa wengi wetu tuna mategemeo makubwa kutoka Azam tv tofauti na ukweli ulivyo...Lengo la Uzi huu si kuharibu biashara ya Azam Bali kueleza uma ukweli halisi wa mambo! so nitaelezea mambo muhimu ya kuyafahamu kabla ya kununua Azam TV.
1. Bei ya decoder hubadilika wakat wowote bila taarifa! mwezi wa 1,2016 nimenunua 140,000 hadi sasa tar 7 Marc imefika 170,000.
2. Channel ya kawaida tuu kama bbc,fox ,CNN ,aljezeera, France 24, mpaka ulipe 20,000 kwa mwezi.
3.sinema zetu utapata bongo movie za 2005 kushuka chini Mara nyingine movie hurudiwa kwa week Mara 3, No latest movie ujue hivyo!
3.organization ya channel iko hovyo! unaweza kulipwa kifurushi cha 12,000 lakini kupata channel moja hadi nyingine ni shughuli! channel za kihundi tuu ndo ziko pamoja!.
4.Tegemea kupata channel kibao za kiarabu na nyingine zisizoeleweka ni lugha gani!
5. Wapenzi wa channel "e" mujue kuwa haipo Azam TV!
6. ukienda kununua watakuambia vipeperushi vya list za channel na bei ya vifurushi vimeisha maana wanajua ukiangalia channel zao na bei utaghair kununua" maana haviendani!!!
Thanx
Kwanza ccn hakuna azam na kuhusu channels za kiarabu azam sio nyingi,haya mapungufu wanayaona maana nasikia wana wao maalumu ambao wanapita kwenye mitandao yote kusoma qanavyoandikwa
 
Kila king'amuzi kinatolewa malalamiko aisee!

Dstv bei ya vifurushi iko juu

Azam wanachannel za hovyo na wanapisha hadi local chanel

Star times kinascratch sana

Continental ni kama star times.

Vipi kuhusu TING?
 
Dstv ...yes ni nzuri kakini expensive
Azam....inakwenda vizuri tuwape muda
Azam.... wanazo OB van za kisasa kabisa ktk kanda zote na the best srudios south of sahara.
Time is the best nedicine
Kama wana vifaa vizuri lakini content zako hazina tofauti na StartTV hivyo vifaa havina maana.Angalia chanel za Kenya utaona tofauti
 
af nasikia usipolipia wanakata hadi channel za ndani aisee wakat mi startimes mwaka sasa sijalipia na kula channels za ndani mpk rahaa
Huo upuuzi na continental wameanza usipolipia hupati Chanel hata moja.. Yaan hakuna cha local wala international
 
Mie na startimes damu damu sijawahi kumuamini mfanyabiashara hasa kama azam bora kidogo mtetezi wa wanyonge anabakia kuwa startimes local chanel napata kama TBC1,TV1,CHANEL10,STARTV,ITV,EATV,CLOUDSTV, na zingine kibao tu kama za dini na sijalipia karibu mwaka sasa kama mpira nitaangalia kwenye kibanda umiza
 
Kwani CNN siku hizi iko Azam?? Kifurushi gani??
Kama nikipata CNN, BBC, AL JAZEERA, DOSCOVERY CHANEL, NAT GEO na ZILE za muziki nafikiri itanitosha zaidi! NITALIPIA.
Siku hizi silipii kifurushi chochote.
Za kibongo na CCTV zote, RT, CHANEL FRANCE 24 English ktk other chanels zinanitosha sana! Nikilipiaga kifurushi naonaga kama wananiibia, huwa siinjoi kivile, hakukuwa na cnn.
Hizo zote nazipata bure maana zipo free to air kwenye satellite zingine ila uwe na dish kuanzia ukubwa wa cm150 na kuendelea.
 
[emoji102] [emoji102] [emoji30] [emoji30] [emoji30] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Mmmh! Chanel e? Ndo ipi hiyo labda? EAST AFRICA ama? Loh? Then hiyo sinema zetu ndo inaboa balaa wanaweka mifilamu ya ajabu ! Wiki nzima hiyohiyo hata ukisema leo nibadilishe radha khaa hovyo!! Kama vipi wafanye kila chanel kulipia 500 kwa mwezi unachagua unayotaka kuliko kutuwekea michanel kibaaao isiyo na tija! Hivi ile "bukkede"sijui nini ni lugha gani ile ?teh Wabadilike bwana!!!
 
Back
Top Bottom