Kabla hujanunua European brand kwa mkumbo zingatia

Nimesoma uzi huu kwa umakini! Pamoja na mawazo mbalimbali ya wadau juu ya hiyo invoice na gharama za utunzaji wa magari ya Ulaya, kuna tatizo moja ambalo waTZ tunalo. Hii ni haswa kwa wanaomiliki gari za Ulaya...
Huyo Jerry sasa hivi anausoma huu uzi.

Na anatamani kumloga mtu...[emoji848][emoji848][emoji848][emoji706]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa yako itakua ni mgeni wa haya mambo ya magari akwa mfano hizo spare zake zote unaweza kuzipata kwa around 1.5m tena unaagiza mwenyewe toka mbele huko na kodi ndani humo humo pia kwa wanaomiliki magari ya ulaya zipo website zinazouza spare za magari kwa ghara nafuu sana pia hawa jamaa wenye garage ambazo biashara zao wanazitangaza mitandaoni ni wapigaji sana
 
Mwenyewe anadai bills ni confidential na hataki kushea na mtu. Tunavyoongea hapa huyu mwana mwenye hio bill kanisusia sababu Jerry Spare kaona hili bandiko kisha ammemaindi kinoma hataki tena wafanye biashara kwa madai amelikisha nyaraka muhimu ambayo ni confidential. Hiki ndio kinafanya wengi wa watu kuitana inbox kwenye biashara za mtandaoni hapa bongo sababu kila mtu anataka ampige kivyake.

Swala la bill linatakiwa liwe wazi na room for bargains iwepo. Imagine uende service na hela mbuzi kisha unafika unakuta bill million 1.5 huku budget yako ni laki 6! Ni uhuni wa hali ya juu.
 
Hahah bongo kila kitu ni siri yaani mpk bill ya matengenezo ya gari?Upumbavu mtupu huu mzee baba.
 
Mkuu Extrovert kweli kabisaa lazima uwazi uwepo kwenye biashara, dah pole kwa yaliyotokea ila meseji sent kwa Jerry abadilike sasa aache janjajanja ajue kuwa kuna mambo watu hawapendi.
 
Mkuu Extrovert kweli kabisaa lazima uwazi uwepo kwenye biashara, dah pole kwa yaliyotokea ila meseji sent kwa Jerry abadilike sasa aache janjajanja ajue kuwa kuna mambo watu hawapendi.
Natumai atabadilika
 
Natumai atabadilika
Abadilike kwa kweli jamaa anataka achaji watu binafsi kama vile ambavyo mtu akipeleka gari CFAO, au Diamond Motors au CMC Motors atachajiwa sasa anasahu kuwa magari mengi yanayopelekwa kwenye hizo kampuni ni ya makampuni, NGOs, serikali na taasisi za serikali, au watu wenye mihela yao ambapo kwa hao kupigwa ni sawa maana hapo kuna cha juu cha aliyepeleka kazi na kingine hiyo pesa haimuumi mtu maana si yake.
 
Huyo Jerry sasa hivi anausoma huu uzi.

Na anatamani kumloga mtu...[emoji848][emoji848][emoji848][emoji706]

Sent using Jamii Forums mobile app
kama namuona vile alivyomkasirikia huyu aliyeshare invoice hapa jamvini, ila naye mkuda sana eti huwa anataka mteja asiende kule gerejini ndani anataka tu uishie pale kwenye reception uongee na vile vibint vikuzubaishe akupige hela vizuri.
 
kama namuona vile alivyomkasirikia huyu aliyeshare invoice hapa jamvini, ila naye mkuda sana eti huwa anataka mteja asiende kule gerejini ndani anataka tu uishie pale kwenye reception uongee na vile vibint vikuzubaishe akupige hela vizuri.
Nachukia sana garage za namna hiyo....Sasa kama hatuuziani bangi sijui kwa nini akatae nikaone mzigo wangu unavyofungwa
 
Heheheee, kweli kabisa.
 
Haha
hahaha japo harrier vifaa vyake ni aghali ila sio kwa million 5 mkuu! Ulikuwa unanua engine nini?
Mkuu, genuine parts zisikie tu kwa jirani. Kuna kipindi nilitaka kubadilisha upper control arms, kuulizia bei, nikambiwa moja ni dola 250 kabla ya usafiri na kodi. Ilibidi nikatafute tu bush za kitaa niweke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…