Kabla hujanunua European brand kwa mkumbo zingatia

Kabla hujanunua European brand kwa mkumbo zingatia

Huyo bwana mdogo Jerry mbona nasikia ana gharama sana hata ukienda tengeneza Japanese cars...na pia anabambikia gari matatizo yasiyokuwepo
Mkuu Jerry ana tabia mbaya ya kulazimisha kupata kipato kiingi toka kwa wateja. usipokuwa makini naye na kama ni mtu unayefuatilia hela zako namna zinavyotumika lazma ugombane naye! kwa mfano unaweza mpelekea gari ambayo shida yake ni oxygen sensor tu, hiyo ni asubuh sasa jioni utapigiwa simu na sauti ya kike kuwa gari ipo tayari nenda kaichuke ukifika unakuta invoice ya milioni na ushee utakuta oil zote kaweka, kuna bush kaweka, na vitu vingine viiiiiingi,

ambavyo ilitakiwa ujulishwe kwanza then mkubaliane, shida yake nyingine anataka kile spare/oils akuuzie toka dukani kwake sasa huu ni ujinga maana binafsi huwa nina maduka ninayoyaamin hivyo sio lazma ninunue kwake kingine anapenda sana kulazimisha mteja atumie brand fulan za oil/spares hapo lengo anataka yeye ndo akuuzie mf wewe ushazoea oil fulan kwa gearbox na ndo inayotakiwa na mtengeneza gar basi yeye utakuta anasifia mioil fulan ya uarabun kwa kuwa tu akiuza hizo anapata faida kubwa.

Kwa kifupi japo ni fundi mzuri lakini si muaminifu ukiservice gari kwake tegemea kwenye bili lazma akuibie tena usipokuwa makini anakuibia sanaaaa.
 
Nimesoma uzi huu kwa umakini! Pamoja na mawazo mbalimbali ya wadau juu ya hiyo invoice na gharama za utunzaji wa magari ya Ulaya, kuna tatizo moja ambalo waTZ tunalo. Hii ni haswa kwa wanaomiliki gari za Ulaya.

Wauzaji wa vipuri vya gari za Ulaya wengi (kwa wale niliowahi kufanya nao biashara) wanawapiga sana waTZ. Kipuri cha £100, wanamuuzia mtu kwa laki 6-7! Niliwahi kutaka timing belt na water pump za continental ambazo ni £120 muagizaji mmoja akanipa quotation ya laki 8.

Hiyo ac compressor ya Audi kwa brands kama Hella, Niessens na Lucas inapatikana kwa siyo zaidi ya £250 kama laki 7.6 hivi. Hata ukiweka usafirishaji na kodi bado haiwezi kufika 1.5M.

Najua wauza spares wa gari za Ulaya wataniona ‘mchawi’, ila wamiliki wa gari za Ulaya jiongezeni! La sivyo kesi kama hii ya Audi zitazidi kuwa nyingi.
 
Kama sio "muaminifu" hawezi kua fundi mzuri kwahiyo neno "fundi mzuri" futa mkuu.
Mkuu Jerry ana tabia mbaya ya kulazimisha kupata kipato kiingi toka kwa wateja. usipokuwa makini naye na kama ni mtu unayefuatilia hela zako namna zinavyotumika lazma ugombane naye! kwa mfano unaweza mpelekea gari ambayo shida yake ni oxygen sensor tu...
 
Tunaoendesha vigari vya Kijapani esp. Toyota tunabezwa sana humu ooh gari mbaya, mbovu, haziko stable na blaah blaah nyengine. Ni sawa ila zinatibika kwa wepesi bila kuua account bank.

Kabla hujajiingiza huko hebu cheki mambo ya Audi A6 huku na hii ni ya 2004. Kwa hisani ya Jerry Spare Parts. Mwenye gari ni bwamdogo mmoja tu kijana wangu.
Duuuh invoice imeshiba, kma hujajipanga unaipaki gereji kwanza. Mi naona ukiwa na German car lazma ubadilike mtazamo mambo flan mfano, lazma uwe mtu wa DIY(Do It Yourself) uijue gari yako vzuri wenzetu mbele ni kawaida mtu kuwa na ka-mini garage home, unanunua hata simple tools na diagnostic tools za kusomea error codes unaziclear mwenyewe kupunguza trip za garage, pia ujue kusource spare kma mfuko umebana agiza mwenyewe online unampelekea fundi anakufungia.

Au kuepuka yote hayo nunua German car ikiwa brand new and unauza b4 haijafika miaka ya major maintenance, ndo wanavofanya ulaya. Otherwise ni ukweli usiopingika Japanese cars ni reliable sana.
 
Wabongo wengi wanapenda malizana hapo hapo bila kwenda huko kutokana na usumbufu. Mimi mwenyewe niliwahi kubamizwa bamaga, na jamaa flani alikuwa anaendesha gari huku jimama linamnyonya rungu utam ukamzidia sijui hakuona mataa...
Labda utumie hilo suala kutatua shida zako za kifedha.

Kiuhalisia, ukinigonga sihangaiki na wewe, bima yako itaenda kutengeneza gari langu. Nikikugonga simalizani na wewe, trafiki akishapima mengine tunamalizana kwa bima.

Sioni mantiki ya kumalizana wakati tunalipa mamilioni bima, huoni wanaondoka na hela yako ya bure?
 
Uko sawa sema ungesema unawapa ushauri class gani ya income earners, kama unavyojua kuna classes tofauti


Niko na jamaa angu hapa ako na VW POLO, nmemuonyesha hii post akaniambia tuinywee hii tununue IST au PASSO kumbe mke wake anatusikiliza mara akaja akatuambia comfortability, stability and power .. Ndio tunayatafakari haya 3
Uko sawa mkuu, comfort, stability and power maybe European cars ndo wenyewe ila nikufungue macho........ Kama unataka yooote plus uimara/reliability jaribu LEXUS au INFINITI, kuna baadhi ya hizi machine zinawakalisha wajerumani kibao tu kwa kila kitu.
 
Nimesoma uzi huu kwa umakini! Pamoja na mawazo mbalimbali ya wadau juu ya hiyo invoice na gharama za utunzaji wa magari ya Ulaya, kuna tatizo moja ambalo waTZ tunalo. Hii ni haswa kwa wanaomiliki gari za Ulaya...
Wengi wenye magari ya ulaya sidhani kama wanajua kuagiza spares wenyewe.

Nadhani tuanzishe uzi wa machimbo ya online ya kununua spares za european cars.

Utafungua macho wengi sana.
 
Uko sawa mkuu, comfort, stability and power maybe European cars ndo wenyewe ila nikufungue macho........ Kama unataka yooote plus uimara/reliability jaribu LEXUS au INFINITI, kuna baadhi ya hizi machine zinawakalisha wajerumani kibao tu kwa kila kitu.
Mkuu hii ni research umenipa, ntaifanyia kazi
 
Sasa mbona watu wanaeema spea za Nissan ni ghali..?
Mmeona huyo mdudu Aud..?Hiyo compressor hata akisema abangaize used, hapati...
Vigari vya Japani vina raha yake sometimes..

Sent using Jamii Forums mobile app
Vifaa vya Nissan vilikuwa ghali zamani. Hivi sasa ni almost sawa na toyota and affordable.

Nachofikiri hapa Tatizo ni wingi wa haya magar kuwa kstika mzunguko. Makampuni yanatengeneza spea kama gar zipo nyingi barabarani.
 
Back
Top Bottom