Mkuu Jerry ana tabia mbaya ya kulazimisha kupata kipato kiingi toka kwa wateja. usipokuwa makini naye na kama ni mtu unayefuatilia hela zako namna zinavyotumika lazma ugombane naye! kwa mfano unaweza mpelekea gari ambayo shida yake ni oxygen sensor tu, hiyo ni asubuh sasa jioni utapigiwa simu na sauti ya kike kuwa gari ipo tayari nenda kaichuke ukifika unakuta invoice ya milioni na ushee utakuta oil zote kaweka, kuna bush kaweka, na vitu vingine viiiiiingi,Huyo bwana mdogo Jerry mbona nasikia ana gharama sana hata ukienda tengeneza Japanese cars...na pia anabambikia gari matatizo yasiyokuwepo
ambavyo ilitakiwa ujulishwe kwanza then mkubaliane, shida yake nyingine anataka kile spare/oils akuuzie toka dukani kwake sasa huu ni ujinga maana binafsi huwa nina maduka ninayoyaamin hivyo sio lazma ninunue kwake kingine anapenda sana kulazimisha mteja atumie brand fulan za oil/spares hapo lengo anataka yeye ndo akuuzie mf wewe ushazoea oil fulan kwa gearbox na ndo inayotakiwa na mtengeneza gar basi yeye utakuta anasifia mioil fulan ya uarabun kwa kuwa tu akiuza hizo anapata faida kubwa.
Kwa kifupi japo ni fundi mzuri lakini si muaminifu ukiservice gari kwake tegemea kwenye bili lazma akuibie tena usipokuwa makini anakuibia sanaaaa.