Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Katika nafasi yangu kuna wakati nilitakiwa kutoa taarifa mbalimbali ili kusifia ufanisi wa Serikali. Kuna wakati tulikuwa tunaona kabisa hamna ufanisi lakini tulipaswa kusifu tu.
Kuna siku wakaguzi Wizara ya Fedha walikuja kukagua mradi ambao tulikuwa tunautekeleza kwa fedha zao. Katika mradi huo ukweli asilimia karibu 50 ya fedha za mradi hazikutumika kwa Mradi - basi wale ndugu walipofika tu nikaelekezwa tukawapokea tukawaweka hoteli nzuri na kisha nina uhakika Bosi wangu aliwatengenezea tokeni fulani hivi na ukweli hawakufika hata kwenye Mradi wenyewe.
Mie niliyesubiri kwa hamu kuwapeleka kwenye Mradi nilishangaa naagwa na hata shauku yangu kuwa wangegundua kitu ikazimwa mara moja. Nawakumbuka vizuri tena mmoja alikuwa mmama na nina uhakika ameshastaafu, anakula pensheni Bukoba.
Mwenzake alikuwa kijana sana na hata mie namzidi umri najua bado yupo kazini na mwaka jana nilimwona kwenye TV.
Kilichonifanya kuacha kazi ni hicho hicho cha kuona makosa au kushuhudia vitendo vya kionezi lakni hatua hazichukuliwi. Tabia ya kuficha mno mambo mabaya imeshamiri katika utawala huu. Ndiyo maana gata CAG yule hakutakiwa.
Wafanyakazi wananyanyasika sana sana. Mkuchika huyu Mwenyezi Mungu anamwona. Mfanyakazi bila sababu yeyote anahamishwa kituo cha kazi na kushushwa cheo.
Mawaziri na hata Viongozi walioteuliwa na Rais ambao wamekuwa ni watu wa watu nao wamekiona cha mtema kuni. Kila wakishauri vinginevyo na Mkulu atakavyo wanapotezwa.
Hivi JK angekuwa hivyo ni kweli Magu angebaki kuwa Waziri awamu zote zile? Hivi kweli Magu hawei kuongoza bila kuonea onea tu watu. Hivi kweli Magu hagundui kuwa kuna taarifa anapewa zinamgombanisha na wananchi?
Magu Magu Magu - wananchi wako wanateseka sana. Wafanyakazi ndiyo balaa - sijui unawatakia nini?
Hata hivyo nimeona baadhi yao - mfano huku Idukilo hata walimu ambao walikuwa ni watu wagumu kugeuka sasa hawapo tayari kupigia kura CCM tena. Na hii imenivuta hata mimi na nimeamua kugombea - tena nagombea nafasi ya udiwani tu - kupitia upinzani.
Nina uhakika nitashinda na nitaendesha kampeni hata Mbunge asitoke CCM tena. Na leo hii natupilia mbali kadi ya CCM. Mmetuchosha Sana! Tumeacha kazi lkn na mtaani mnatusababishia umaskini. Singapore kabisa CCM hii! Tena Bangladesh kabisa!