Wafanyakazi wanadeka sana Mkuu
Hii Nchi ina watu milion 60 kati ya hao wafanyakazi hawafiki milion serkalini
Je ingekuwa wewe ungetoa kipaumbele kwa nani?
Kuna tusi ilikuwa nikutupie wallah nimelihifadhi
Kweli unatetea ufedhuli wa kuwanyima nyongeza watumishi miaka 6?
Unafahamu umuhimu wa wafanyakazi kupewa nyongeza kweli?
Hivi bei ya vitu na ughali wa maisha tangu 2014 mpaka sasa uko sawa?
Bei ya bidhaa na thamani ya fedha na mfumuko wa bei uko constant eeehh?
Gharama za maisha hazipandi eeehh?
Acha kujitoa ufahamu, suala la ngosha kuwanyima watumushi nyongeza ya mshahara na kuwapunguzia purchasing power yao siliungi mkono hata kidogo. Tena amekutana na watumishi waaminifu sana, wallah wangemfanyia miujiza na nguvu zingemuishia kama wasingekuwa wavumilivu .
Kuna mambo ngosha anazingua hili namba moja.
Mengine aliyozingua ni suala la pensheni na vikokotozi vyake, kubadili sheria ya mifuko ya pensheni eti pesa ya MTU unamwekea masharti ya kuchukua wakati huo mbunge anavuta yote kwa kigezo cha kipuuzi eti atatumia vibaya, unampangia matumizi MTU pesa yake? Uwehu kabisa huo.
Issue nyingine ngosha kazingua ni kubadilisha sheria ya mikopo vyuo vikuu, sheria itungwe mwaka huu eti kibabe tu iwaathiri na wa miaka ishirini nyuma, yaani ana bahati nchi inawanaojiita wasomi wapole sijui ndio wamerogwa vile, wako kimya tu hawafurukuti wenyewe na ukandamizi wote huu.
Endelea kumtetea kwa kila kitu huyo ngosha wako.
Namsifu kwa issue ya corona tu maana angetupiga lockdown wallah sisi machinga tungerest in peace kwa stress za marejesho ya vicoba na sio corona tena..
Wapiga kura vijana mkimpa kura ngosha kabla hajarekebisha hizi sheria mtakuwa mmerogwa si bure.