Uchaguzi 2020 Kabla ya hii miaka mitano haijaisha, uwezo wa Mungu utakuwa umejidhirisha kwa wanaotuhumiwa kuhujumu uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Hujathibitisha Mungu yupo.

Imani hata wewe unaweza kujiaminisha ni Mungu.
 
Mungu wa CHADEMA ndiyo unaye msema! Lakini kama ni mungu wa kweli (Allah), huyo ameisha tenda na kaipa CCM ushindi wa kishindo. Saliti kalikimbizia mbali ubelgiji - ulaya.
 
Kamuulize G Lema ndoto zake ziliishia wapi? Ukitaka kujua hayo mawazo yako ni ushetani tu jitokeze uwekwe gerezani uone kama hiyo ndoto yako itatimia.
Ukitoka huko hata ndoto hutaikumbuka
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Imani hata wewe unaweza kujiaminisha ni Mungu.
Dah we jamaa na hoja zako za uthibitisho wa Mungu sijui unataka umuone kwa macho?

Mie nadhani ungeachana na hizi propaganda zako rahisi,eti anajichaficha wapi,nani aliyekwambia anajificha ficha.

Wewe kama dhamira yako imeisha isiwe tabu kwa wengine.
 
Bado hata wewe hujathibitisha Mungu yupo.
 
Dah! Heri "unge-peter" mbali tu maana kichwa kilishakujamu tayari. Unasema aliyekuleta hayupo? Na ndiye aliondoa Mr Kovidi-19??? Shame on you!!!
 
Kamuulize G Lema ndoto zake ziliishia wapi? Ukitaka kujua hayo mawazo yako ni ushetani tu jitokeze uwekwe gerezani uone kama hiyo ndoto yako itatimia.
Ukitoka huko hata ndoto hutaikumbuka
Si lazima iwe leo au kesho kama unavyofikiri wewe.
 
Hivi Chadema imeandikwa kwenye kitabu chochote cha dini kuwa lazima iwe na wabunge wengi Bungeni?
 
Wezi wa kura hakika watajuta ndani ya miaka hii 5. Hatima yao ndiyo ajira ya wahafidhina. Mwana kulitaka mwana kulipewa.
 
Kuna watu mnateseka sana moyoni na Magufuli kuwa Rais.
Hakuna mtu anateseka magu ni Mtanzania mwenzetu japo inasemekana ni waraia wa asili ya nchi jirani,hilo sio tatizo kwani waTanzania walio wengi tumetokea misitu ya Congo.
kama mTanzania ana haki zote tokea kuwa balozi wa nyumba kumi hadi raisi,sioni sababu ya mtu kusema anachukiwa,mshituko tunaokwenda nao na mtiririko ni namna gani viongozi wa Tanzania wanapatikana,
Je njia wanazopatia uongozi ni sahihi ? Sheria na kanuni tulizojiwekea zinafuatwa ? Ni kitu ambacho ilitakiwa tuwe mfano kwa jumuia za kimataifa ,WaTanzania ni watu wa amani sana sana na ni wavumilivu na wala sio waoga ,wanaamini kuna maisha baada ya uchaguzi.

Tanzania kwa nini tunashindwa kufuata simple rules za uchaguzi tulizojiwekea na kwa nini yanatokea mauaji ndani ya siku mbili tu za uchaguzi ,jambo gani linapelekea kufikia huko ? Watu wanapigwa wanaumizwa wanauliwa ! sababu nini uchaguzi wa siku moja tu ,tunaumizana ,hakuna ulazima w nani ni lazima awe kiongozi kwani wananchi wakiachiwa wachague na wakachagua ndio uhuru wenyewe kama waliemchagua hakufaa watamchagua mwengine .

Inaposemwa taratibu na mizengwe imetumika na ushahidi na malalamiko kila kona, ichunguzwe na kama ikithibitika waliohusika wachukuliwe hatua.

baada ya kampeni zilizogharimu mabilioni halafu yanatokea matatizo ,ukiangalia sijui kuteuliwa,kupitishwa fomu imekosewa haya ni mambo yanayoweza kurekebishwa na ndio sababu ya kuwepo tume ya kusimamia uchaguzi,yote yanarekebishika,kuliko kusema unamuondoa kwa sababu sehemu ya mke ameandika mume ,tarehe imekosewa,haya au hizi ndio sababu zinaweka kasoro ukiongeza na pingamizi ,haya yarekebishwa kitu pingamizi kiondolewe kabisa,tume ihusike kurekebisha kasoro hizo.

Uchaguzi uwe free and fair ,mi naamini hata bila ya mizengwe Magufuli angeweza kushinda hata kwa kura moja,hakuna sababu ya kudanganyana sijui ameshinda kwa asilimia 90, Zanzibar kule utumbo mtupu ni aibu na inawatia kasoro hao walioshinda na ni aibu,japo wanajikaza kisabuni,

Tuweni na maendeleo katika usimamiaji wa uchaguzi.polisi majeshi wote washirikishwe kikamilifu kuona haki na amani inatendeka, Tume ikubalike na kila mmoja wetu ,kampeni za kistaaarabu bila ya mtu mmoja kupigwa mabomu au kuzuiwa.

Leo viongozi wameshinda lakini kilichowatia simanzi ni mauaji yasio ya lazima hivi ndio mauaji haya yatawasaidia ,hivi mauaji haya yamesaidia wao kuwepo madarakani ? Nionavyo hayakuwasaidia hata kidogo wala hayahusiki na ushindi wao.

Mnataka kusema kuwa Magufuli na Mwinyi wameshinda kwa sababu maadui wao wameuliwa ? Waliokufa ni raia masikini just na wao wakishiriki katika mihemko ya uchaguzi .

Je kuna polisi yeyote alipigwa jiwe la kichwa na kumwagika damu ?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…