Kabla ya kuingia lebo ya Wasafi, Rayvanny na Harmonize walikua wapi? Walipofikia leo wangeweza bila Wasafi? Label ipi ina karibia WCB hapa Bongo?

Yeap smooth vibes bro na ile THT ilikuwa ni chuo cha muziki lakini bado kilisimamia wasanii

Kuhusu issue ya diamond kuchukua 60/40 ni sawa kama biashara kutokana na investment aliyoweka ila kama suala la P funk ni ni kweli, yaani producers na wasanii wake wananyang'anywa total ownership ya kazi zao sidhani kama ni haki
THT kilikuwa ni kituo cha kulelea watoto yatima.

Huwezi kupewa ownership ya kazi zako ukiwa ndani ya label kazi zako ndio dhamana yako ya biashara ndio maana WCB ukitoka unalipa pesa unapewa rights zako zote. P Funk ukimaliza mkataba kwenye label yake rights anabaki nazo yeye ndio maana mpaka leo master za album za wasanii wake anazo yeye
 
Kuna mgawanyo wa faida na kuna umiliki,

Leo wewe unaweza kupiga show na ukapata 40% lakini haimaanishi hati miliki ya kazi yako ya sanaa kama mshairi na muimbaji au producer ni yako kwa 40%...

Au labda mimi sijaelewa fresh unijuze mkuu kwa wewe ulivyoelewa
Hivi jiulize kwanini vijana wengi hawakimbilii kwenda king's Music ya Alikiba ambapo ni bure kabisa wanapenda kwenda Wasafi?
 
Kumbe jibu unalijua sasa kwanini unapingana na wadau hapo juu

Ulichouliza na mada iliyopo mezani ni mbingu na ardhi ila wengi wa WCB fans mmeshaaminishwa kuwa mtu akitoa mawazo against wasafi bhasi anaichukia

Either ways, umeshinda mzee, nilikosea nyie mpo right 👏👏👏
 
Against inategemea na kitu gani ila hili label labda uamue kupinga kwani yupo sawa.

Mimi natamani siku Diamond amke aseme sasa mimi label basi, hela yake akanunune frequency TCRA aongeze idadi ya coverage ya mikoa kwa redio yake.
 
Ulichouliza na mada iliyopo mezani ni mbingu na ardhi ila wengi wa WCB fans mmeshaaminishwa kuwa mtu akitoa mawazo against wasafi bhasi anaichukia

Either ways, umeshinda mzee, nilikosea nyie mpo right 👏👏👏
Diamond Unaweza kumpinga kwenye vitu vingine ila kwa upande wangu naona label yake inamchango mkubwa Sana kwenye industry ya mziki wetu na hii ni facts nimejaribu kufuatilia malipo wanayopata wasanii wa nchi tofauti kwenye label mbalimbali hiyo 40 of share ni kubwa Sana hata ningekuwa ni mimi nisingekuwa namlipa hiyo percentage msanii wangu
 
Mimi siyo mpenzi wa hii miziki
Lakini ukweli tu hao sjui rayvany harmo washurukuru maana walitolewa kusiko julikana na wakafanywa wajulikane

Ni sawa,mtu Huna hata 100
Anakuja mtu anakudhirikisha
Deal la mln 200 deal inatiki anakupa mln 40,hapo utashukuru utaishia kusema umedhulumiwa

Ova
 
Hakuna kitu kinaitwa "Unyonyaji" kwenye dunia ya mabepari. Umepewa mkataba, unapewa muda ukausoma na kutafakari, ukaona unafaa, ukatia saini. Hakuna la ziada hapo.

Nitaamini Wasafi ni wanyonyaji siku akitokea mtu akatae mkataba wao mwanzoni kabisa kabla ya kupata umaarufu.

Kama unaona ni gharama nenda nje upambane kivyako ,mwenyewe, Shida iko wapi kwani? ila ujipange sasa...

  • Kajitaftie maneneja wenye uzoefu kama babu tale, salam na mkubwa fela
  • kajilipie shooting mwenyewe kwa milioni 50 hivi,
  • Tafuta mpiga picha wako wa social media
  • Jenga connection zako mwenyewe ziwe za radio, wanasiasa, n.k.
  • Anza kujivalisha nguo kali kwa pesa zako.
  • Kodisha mwenyewe ndege za kusafiri.
  • Andaa mwenyewe matamasha yako.
  • Ukizinguana na media kubwa, anzisha radio yako

Sio mtu unatolewa manzese huko, watu wanakubrand, wanakupambania unahit mpaka nje ya nchi, alafu wakichukua gawio lao la uwekezaji wao walofanya kwako unasema eti wanyonyaji. Hakuna free lunch dadek!

Msanii akipata jina kawa mkubwa na akishaona hela nyingi zinaingia kwenye label anaingia tamaa anatamani hela yote angekuwa anapata yeye, yaani anasahau kabisa alikotolewa na gharama zilizotumika kumfanya mpaka awe sehemu alipo.

Msanii kaitwa kupiga show kwa milioni 20, Lebo inachukua gawio lake 60% sawa na milioni 12 na wanamwachia msanii gawio lake 40% sawa na milioni 8, msanii anaanza kulalamika ohh nanyonywa !! anashindwa kujua hii ni biashara ambayo lebo imewekeza hela nyingi kwake takribani milioni 500, pesa hizi si zawadi jamani, Ni uwekezaji

Kumbuka sio kila msanii anarudisha pesa waliyotumia kumuwekezea, kuna kina lava lava sidhani kama pesa ya uwekezaji imerudi
🤣
 
Kwenye ile label ambaye atajaribu kubaki juu ni Harmonize tu, hao wengine wanakurupuka mwisho watakuwa mateja
 
Hyo lay nn cjui anasahau jins alivokua boya kabla ya kuchukuliwa na wasafi duh.
 
Back
Top Bottom