Kabla ya kuja wakoloni ukanda wa Afrika Mashariki uliitwa
AZANIA.
George Wauchope Azania Land of the Black People There often exists an undeclared state of war among people involved in the struggle for liberation as between those who support and those who are ag…
azanianrevolution.wordpress.com
Samahani mzee, hakika Azania si jina la eneo la Tanzania. Inawezekana sehemu za pwani za Tanzania ya leo zilihesabiwa kuwa sehemu ya Azania, lakini haina uhakika sana. Hakika ni maeneo makubwa ya tanzania hayakuwa "Azania".
Soma hapa
Azania (kwa
Kigiriki Ἀζανία) ni
jina la kihistoria kwa ajili ya sehemu mbalimbali za
pwani ya
Afrika ya Mashariki.
Asili yake ni zamani za
Waroma na
Wagiriki wa kale kwa eneo lililokuwa la
watu wa
Lugha za Kikushi.
Mapokeo ya Waroma na Wagiriki wa Kale
Mara ya kwanza jina hili limepatikana katika
mwandishi Mroma
Plinio Mzee (Gaius Plinius Secundus) aliyeishi wakati wa
karne ya 1 B.K.
Kufuatana na maelezo yake, Azania ni sehemu zile zilizoanza katika eneo la
Adulis (leo:
Eritrea) na kuelekea
kusini.
Kitabu cha mwongozo kwa ajili ya
mabaharia "
Periplus ya Bahari ya Eritrea" (
karne ya 2 BK) kinatoa maelezo zaidi zinazoonyesha ya kwamba jina la Azania labda lilimaanisha pwani ya Afrika ya Mashariki kutoka
Eritrea hadi sehemu za
Tanzania ya leo.
Mwandishi
Cosmas Indicopleustes wa
karne ya 6 B.K. aliandika Azania ni nchi chini ya
utawala wa
ufalme wa
Aksum, basi hapo isingeenea sana kusini kwa
pembe la Afrika.
Zanj ya Waarabu
Katika
karne zilizofuata
umbo la "Azania" halikutumika tena. Inawezekana ya kwamba sababu yake ilikuwa
Waarabu Waislamu waliochukua nafasi ya Wagiriki na Waroma wakitawala
biashara ya nje ya pwani ya Afrika ya Mashariki. Kuna uwezekano ya kuwa Waarabu walitumia matamshi tofauti ya neno kuwa "
Zanj" kwa ajili ya eneo lilelile.
"Zanj" imekuwa
asili ya neno
Zanzibar.
Matumizi ya neno Azania katika karne ya 20
Kuingia katika jina la "Tanzania"
Katika
karne ya 20 jina la Azania limefufuka tena.
Nchi huru za
Tanganyika na
Zanzibar ziliungana
tarehe 26 Aprili 1964 kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jina jipya lilitafutwa. Hapo jina lile la kihistoria "Azania" lilikumbukwa tena; kwa kuunganisha maneno ya Tanganyika, Zanzibar na Azania jina la nchi "
Tanzania" limepatikana.
(Isipokuwa Mohammed Iqbal aliyebuni neno Tanzania hakurejea jina "Azania", lakini wengine walikumbuka)
Kutaja Afrika Kusini
Kwa namna tofauti jina la Azania lilitumika pia
Afrika Kusini. Wakati wa
siasa ya
ubaguzi wa rangi sehemu ya
wapinzani wa siasa hii hawakutaka kutumia
jina rasmi la "South Africa / Zuid Afrika" tena. Walitafuta jina katika
historia iliyotangulia kufika kwa
Makaburu wakichukua jina la Azania. Ni hasa
vyama vya
PAC na
Azanian People´s Organization waliotaka kubadilisha jina la Afrika Kusini kuwa Azania. Lakini chama kikubwa cha
ANC haikukubali, hivyo mipango ilishindikana.