Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Nakubali maelezo ya Wikipedia ya Kiingereza si sahihi.Hii historia ni uwongo wa kubuni tu. Jina Tanganyika halina uhusiano kabisa na maneno ya Tanga na Nyika, bali ni neno la kimanyema linalotokea huko Kigoma, Ujiji likiwa na maana inayokaribiana na ama "..wanaotoka Magharibi" au "...wanaochangangika." Ziwa Tanganyika lilipewa jina hilo zamani sana hata kabla ya nchi hii kukwa maana hiyo kuwa watu wa kutoka Kongo walikuwa wakiiangia Ujiji kutokea magharabi kwa kutumia ziwa hilo na kuchanganyika na watu wa ujiji.
Angalia ramani ya sehemu hiyo zamani sana kabla hakujawa nc nchi inyoitwa Tanganyika."
Kuhusu asili ya jina TANGANYIKA kwa ajili ya ziwa kuna taarifa iliyotungwa na mpelelezi wa Marekani HM Stanley aliyeandika majibu ya wenyeji wa wakati wake, ila ni tofauti na yale uliyosikia. Angalia Tanganyika (ziwa) - Wikipedia, kamusi elezo huru
Jina la ziwa limepokewa na Wazungu wapelelezi wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa Ujiji. Henry Morton Stanley aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba watu wa Ujiji hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina, ila tu ilimaanisha ziwa kubwa[1]. Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hili "Tanganika". Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitoka kwa aina ya samaki walioitwa vile. Baadaye Stanley alikumbuka neno "nika" katika lugha nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotanda" [2].
Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa makabila mengine: watu wa Marungu walisema "Kimana", wale wa Urungu "Iemba" na Wakawendi "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu, yaani "Iemba", inalingana na taarifa ya David Livingstone aliyekuta jina "Liemba" kuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa na jina hili linaendelea kutumiwa kwa meli ya MV Liemba inayosafirisha watu na bidhaa ziwani tangu mwaka 1914.