Kabla ya kuitwa Tanganyika, Tanzania iliitwaje?

Nakubali maelezo ya Wikipedia ya Kiingereza si sahihi.
Kuhusu asili ya jina TANGANYIKA kwa ajili ya ziwa kuna taarifa iliyotungwa na mpelelezi wa Marekani HM Stanley aliyeandika majibu ya wenyeji wa wakati wake, ila ni tofauti na yale uliyosikia. Angalia Tanganyika (ziwa) - Wikipedia, kamusi elezo huru

Jina la ziwa limepokewa na Wazungu wapelelezi wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa Ujiji. Henry Morton Stanley aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba watu wa Ujiji hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina, ila tu ilimaanisha ziwa kubwa[1]. Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hili "Tanganika". Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitoka kwa aina ya samaki walioitwa vile. Baadaye Stanley alikumbuka neno "nika" katika lugha nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotanda" [2].

Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa makabila mengine: watu wa Marungu walisema "Kimana", wale wa Urungu "Iemba" na Wakawendi "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu, yaani "Iemba", inalingana na taarifa ya David Livingstone aliyekuta jina "Liemba" kuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa na jina hili linaendelea kutumiwa kwa meli ya MV Liemba inayosafirisha watu na bidhaa ziwani tangu mwaka 1914.
 
Kimsingi ni vile: Hapakuwa jina kwa ajili ya Tanzania kabla ya ukoloni. Maana maeneo ya Tanzania hayakuwa pamoja.
Unaweza kutaja Mrima (pwani la kaskazini), na maeneo mengi mengine; tungeweza kuyaita kufuatana na makabila (Unyamwezi, na kadhalika) ila makabila yalibadilikabadilika ukienda nyuma zaidi.
Tanzania ni nchi iliyoanzishwa na wakoloni, sawa na Kenya na nchi nyingi za Afrika.
Kwanza na Wajerumani waliopatana na Waingereza, Wabelgiji na Wareno kuhusu mipaka, halafu kuwalazimisha watu ndani ya mipaka hii kukubali -angalau kutii au kutopinga mno- serikali yao.
Pili na Waingereza walioamua kuwaachia Wabelgiji sehemu za Rwanda na Burundi kuwa gawio lao kwa kushiriki Vita Kuu ya Kwanza. Halafu Waingereza walichagua jina la "Tanganyika" (katika majadiliano yao waliangalia majina kama Smutsland, Eburnea, Azania, New Maryland, Windsorland, Victoria, Kilimanjaro na Tabora - linganisha Tanganyika - Wikipedia, kamusi elezo huru)
Tatu na watu wake wenyewe waliopokea koloni ya awali mikononi mwao na kundesha maendeleo yake.
 
ohh
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ahsante sana kwa ufafanuzi zaidi
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ahsante kwa ufafanuzi ila inabidi usome historia ya Tanzania kutokea vyanzo mbalimbali
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ahsante kwa ufafanuzi zaidi lakini inabidi tupate maelezo zaidi kutoka vyanzo mbalimbali
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ahsante sana kwa maelezo
 
Ndio. Iliitwa Mrima.

Rejea: Malenga wa Mrima πŸ˜‰
πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘

Ahsante ila inabidi tusome vyanzo mbalimbali zaidi.
 
πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„
 
Nimesoma kwenye kitabu cha Tippu Tip ameandika hivyo Ruanda Urundi
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ahsante! ila inabidi tupate majibu kutoka vyanzo mbalimbali.
 
kabla ya wezi kuja africa(mabeberu)hapakuwa na nchi,inayoitwa Tanganyika au tanzania.kulikuwa na vipande vya maeneo vilivyokuwa na utawala unaojitegemea.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…