Kabla ya kujenga fly over Magomeni na fire panueni barabara Kimara - Ubungo

Kabla ya kujenga fly over Magomeni na fire panueni barabara Kimara - Ubungo

Wajinga sana hawa wangepanua mandela road au wamalize tatizo la Buguruni
Sasa imagine barabara kubwa kama ya mandela ambayo magari yote toka bandarini yanapita wala husikii plan zozote zaidi ya kuja na mambo ya flyovers. Imagine tangu uhuru... imagine
 
We are very short sighted.... Leo hii hapa Dar haitakiwi tena kujenga barabara 2... inatakiwa 3x3 tu kama Kimara - Kibaha
Akili hiyo watoe wapi babu... mwenye akili hizo alishaondoka nazo
 
Na Rais huyu tulie nae sijui kwakweli,,,haya yotee yangewezekana tungelikua na Rais mwenye maono makubwa,,mfatiliaji muwajibikaji na mkali panapobidi ili mambo yaendeee

Lkn doohhh basi tu,Tuvumilie
 
Nimeshangazwa sana na huyu waziri kusema wanatafuta hela kujenga fly over magomeni na fire na sehemu zingine lakini cha kushangaza hawajagusia kabisa kupanua kipande sumbufu kwa foleni kutoka ubungo hadi kimara, na barabara ya mandela.

Hivi jamani inahitajika hadi aje Tony Blair kutuambia hizi barabara ni tatizo kubwa kwa uchumi wetu? Inamaana hamjui hii ni njia malori yote yanaenda nchi jirani yanapita kila siku plus mikoa yote ya kati na kusini?

Mbona hawa viongozi wanashangaza sana na vipaumbele vyao. Miaka mitatu sasa hata street lights tu wameshindwa kumalizia tu barabara ya Mbezi- Kibaha wakati mwenzao alipanua barabara vizuri tena ndani ya muda mfupi. Si hata basi mfanye kuunganisha kile kipande hadi ubungo?

Nini kinazuia?

View attachment 2631745
Hii barabara ya Kimara ni kero kubwa sana tu. Foleni yake si mchezo. Serikali ilione hili itusaidie wanannchi wake.
 
Back
Top Bottom