The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
- Thread starter
- #21
Mbona unachanganya mambo mazee?Net solutions hawakuja kui improve Tanesco walikuja kuleta mapendekezo na kuiandaa kuiuza..Saga la NBC in the long run limeiyumbisha sana Tanzania kuliko tunavyoweza kufikiri hasa kiuchumi.
Ilikua ni matakwa ya IMF kuiua NBC ili sekta binafsi ya kibenki iweze furukuta lakini kilichoipata NBC leo hamna mpambe anataka kizungumzia. Sekta ya benki imekua Yes... je implication yake kwa uchumi wa nchi ikoje ukilinganisha na nguvu ya NBC ya wakati ule? Je why benki nyingine zisingekuja kupambana na NBC?
Mkapa amekiri mara nyingi hadharani na kwenye kitabu chake kuwa ubinafsishaji kwa sehemu kubwa alikosea maana 80% ya mashirika ya umma yaliingia mifukoni mwa matapeli!
Hoja zile sile waliosimamia watu juu ya uwezo na aina ya mikataba ya hovyo ya ubinafsishaji ndizo zilikuja kuonekana wazi kweli waliopinga walikua na hoja tena kubwa sana.
Vipi NET group Solutions? ATCL? TRL?
Meremeta? Na mengine?
Shida yetu kubwa tunakimbilia sana kwenye petty issues when it comes to analysis
Mfano huu mkataba wa Tanzania na DP World ni wa hovyo usioelezeka! Hoja si kubinafsisha bandari Hoja ni mkataba wa hovyo!
Madini hadi leo yametufikisha wapi ukitulinganisha na Botswana na SA? Mbona kwao pia kuna sector binafsi?
HOJA sio ubinafsishaji hoja aina ya mikataba ya kishenzi ambayo nchi zetu zinaingia.
Net solutions wwalifanikiwa Kwa mfano kukusanya madeni yote ya serikali ingawa Kwa mujibu wa mkataba hawakuruhusiwa kufanya investment za Ku improve Tanesco.. Mkataba ulikuwa kuandaa mazingira ya Ku li privatise kitu ambacho baadae kikawa canceled..
Naona unalazimisha mifano ya ATCL..hutaki mifano ya TBL ,wala hutaki kukubali sehemu ya mabadiliko ya kuuza NBC ilizalisha NMB..bank kubwa kuliko zote Tz ambayo inamilikiwa na watanzania na Serikali asilimia 70...
NBC isingeweza kushindana na mabenki binafsi...
Mbona husemi jinsi Benki zingine za Serikali zilivyofilisika juzi tu?
TIB?
Tanzania womens Bank?
Twiga bank??