Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Mbona unachanganya mambo mazee?Net solutions hawakuja kui improve Tanesco walikuja kuleta mapendekezo na kuiandaa kuiuza..
Net solutions wwalifanikiwa Kwa mfano kukusanya madeni yote ya serikali ingawa Kwa mujibu wa mkataba hawakuruhusiwa kufanya investment za Ku improve Tanesco.. Mkataba ulikuwa kuandaa mazingira ya Ku li privatise kitu ambacho baadae kikawa canceled..

Naona unalazimisha mifano ya ATCL..hutaki mifano ya TBL ,wala hutaki kukubali sehemu ya mabadiliko ya kuuza NBC ilizalisha NMB..bank kubwa kuliko zote Tz ambayo inamilikiwa na watanzania na Serikali asilimia 70...
NBC isingeweza kushindana na mabenki binafsi...
Mbona husemi jinsi Benki zingine za Serikali zilivyofilisika juzi tu?
TIB?
Tanzania womens Bank?
Twiga bank??
 

...
Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi ....

Maelezo yako ni sahihi kuwa uwekezaji una tija. Ninalopinga kuhusu Mkataba wa bandari ni kampuni ya DPW kuwekeza kupitia mgongo wa nchi yao, Dubai. Mkataba wa IGA, una vifungu vinavyoipa DPW hadhi ya nchi.

Kwa kuwa DPW ina uwezo na uzoefu wa kuendesha bandari, tayari tarehe 28/2/2022 ilikuwa imeingia Mkataba wa Maelewano (Mou) na TPA. Haingii akilini kwa nini DPW haikuendelea na mpango huo, ikajisajiri BRELA kuanza kazi kwa kushirikiana na TPA, badala ya kulazimu Tanzania iingie Mkataba na Dubai, nchi yake, wenye masharti tata km Ibara ya 5(1,4)? Nia ya IGA ni nini wakati kuna makampuni mengi tu km ubinafsishaji wa mabenki wakati wa Mkapa na makampuni ya uchimbaji madini, ambayo naamini hakuna mikataba kati ya Tanzania na nchi zao, kwa kuwa tuna mahusiano ya kidemokrasia.
 
Ubinafsishaji wa Mkapa huwezi kuulingabisha na uuzwaji wa Bandari! Mkataba wa ubinafsishaji ilikuwa na tija na ukomo kuliko huu wa DP WORLD
 
Ulipaswa kuorodhesha mashirika yote yaliyobinafsishwa na mkapa, alafu tuangalie mangapi yamefaulu na mangapi yamefeli. ndio hapo utapata jibu

Mkapa kwenye kitabu chake anakiri alifanya makosa kwenye ubinafsishaji wa mashirika, mengi yalikufa.
 
Ubinafsishaji wa Mkapa huwezi kuulingabisha na uuzwaji wa Bandari! Mkataba wa ubinafsishaji ilikuwa na tija na ukomo kuliko huu wa DP WORLD
Hata hivyo mashirika mengi yalikufa, hayo anayotolea mfani ni machache sana. 80% yalienda na maji, bahati nzuri mkapa aliandika kitabu na alikiri kukosea
 
Fact...
 
Mbona majibu yametoka..hukusikia?
Imesainiwa IGA.. intergovernmental agreement...Mkataba wa bandari lazima utakuwa na kikomo..na mda wa review utakapo sainiwa.. huelewi nini?Bunge limeridhia serikali iende kuingia mkataba.., mkataba halisi bado...
Mkuu so kikomo ikiwa miaka 100 ni mfano tu, utakuwa mkataba mzuri? Kha mbona vigumu sana kuamini.

Udini upo hilo lipo wazi but process nzima ya uwezekaji sio kabisaaaa.

Kwani nini kila uwekezaji ni wao waarabu?

Tunaogopa kugeuzwa watumwa ndani ya nchi yetu…
 
Mnaotoa.Maelezo mengi ya kutetea uzuzu.Wa Samia mnanikera sana. Kwa kifupi hatutaki bandari wachukue hata mkataba ningeletewa.Mimi..ningewauliza je. ni.win win situation hamsini.kwa hamsini.tofauti na.hapo welcome. again
nilisoma historian.ya.Suez.canal. inasikitisha.hawa.mabeberu.wanatuona.kama kama.hatuna.ubongo.vile
 
Nimesema pale juu, kuboresha
Weka kumbukumbu zako sawa... NMB haikuzaliwa kwa kuuza NBC! NmB ilizaliwa kwa kuivunja NBC kisha kuiuza.

Pili hao TBL waliwahi zalisha hasara huko nyuma? TBL serikali iliuza hisa ngapi? Unafuu gani ulipatikana baada ya kuuza TBL? unafahamu TBL,KILOMBERO, NBC, Mkonge ni mashirika yaliuzwa yakiwa yanafanya vizuri sana?
Kwanini unataka tu nijadili ya TBL hutaki ya STAMICO, TRL, NET GROUP SOLUTIONS, MEREMETA, ATCL na mengine? Why unachagua upande?

Mbona SGR, Stiglers Gorge hamkutaka wawekezaji?

Kwani tusingeweza kopa pesa kuboresha bandari zetu? Sawa anapewa mbia kwa mkataba huu wa kishenzi namna hii?

Nimesema pale juu kupata mbia wa kuboresha bandari sio shida, shida ni kuliwa,!!

Mkataba wa DP world na TZ ni wa kishenzi kuliko aliouingia chief Mangungo shida iko hapo.
 
Watanzania wengi wana uelewa wa chini sana! Wapambe wengi wanafikiri shida ni DP world kuendesha bandari ilhali hoja kinzani ni mashaka makubwa juu ya mkataba huo!
 
Ulipaswa kuorodhesha mashirika yote yaliyobinafsishwa na mkapa, alafu tuangalie mangapi yamefaulu na mangapi yamefeli. ndio hapo utapata jibu

Mkapa kwenye kitabu chake anakiri alifanya makosa kwenye ubinafsishaji wa mashirika, mengi yalikufa.
Yaliyofaulu ni yale yaliyouzwa ilhali yakizalisha faida kubwa sana sana yaliwapa faida wageni...

Yale yaliyokuwa choka mbaya yaliingia mifukoni mwa wajanja wakalala mbele imebaki historia.
 
Mbona majibu yametoka..hukusikia?
Imesainiwa IGA.. intergovernmental agreement...Mkataba wa bandari lazima utakuwa na kikomo..na mda wa review utakapo sainiwa.. huelewi nini?Bunge limeridhia serikali iende kuingia mkataba.., mkataba halisi bado...
Uko brainwashed sana!

Why inte government agreement na DP world ni kampuni kama zilivyo GGM?

Kumbuka kilichopitishwa na bunge ni kama sheria itakayosimama badala ya TPA act ya 2004. Yajayo hayatatoka nje ya hiki kinachopigiwa kelele leo.
 
Umeandika mengi lakini sijui kwanini mnapenda kuwazuia watu kuwaza tofauti!
Madocuments si mliyaleta hadharani wenyewe? Sasa yanaposomwa kwanini hamtaki watu watoe mawazo yao hadharani?
NB:
1. Nchi hii Kuna matatizo ya msingi. Ubaguzi. Elimu duni... Maisha magumu. N.k. Stress ni kubwa. Ajabu hamtoi majibu zaidi ya kuwatukana wenye mawazo tofauti.
2. Kwenye uwekezaji umeamua kuelezea mazuri machache. Lakini ya ovyo mengi hujataja kabisa!
3. Ooh kumbe ni kweli. Mwl. JKN aliwakera ikabidi apewe maradhi.
4. So, tutarajie mtamtafuta mwekezaji aje aendeshe bunge? Make nalo haliperform vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…