Kabla ya kuvunja TTCL serikali ingefanya haya kwanza.
Kuhakikisha zoezi la kampuni zote za simu zinauza hisa Kwa wananchi kama ambavyo sheria inataka na iwapo wananchi wakishindwa kununua hisa hizo basi serikali inunue hisa hizo Kwa niaba ya wananchi...kama ambavyo serikali ina hisa NMB, puma n.k.
Kuiondoa TTCL Kwa sababu haileti faida na kuacha industry yote imilikiwe na watu wachache ni hatari sana...
Serikali ifanye tathmini ya kutosha..
Miaka ya nyuma tulikuwa na mashirika mengi ya umma. Kwa upande wa nguo tulikuwa na Urafiki, Mwatex, Mutex, kiwanda cha nyuzi Tabora, n.k. Kwa kilimo tulikuwa na UFI na. Tulikuwa na MOPROCO kilichokuwa
Kabla ya kuvunja TTCL serikali ingefanya haya kwanza.
Kuhakikisha zoezi la kampuni zote za simu zinauza hisa Kwa wananchi kama ambavyo sheria inataka na iwapo wananchi wakishindwa kununua hisa hizo basi serikali inunue hisa hizo Kwa niaba ya wananchi...kama ambavyo serikali ina hisa NMB, puma n.k.
Kuiondoa TTCL Kwa sababu haileti faida na kuacha industry yote imilikiwe na watu wachache ni hatari sana...
Serikali ifanye tathmini ya kutosha..
Hoja fikirishi kabisa. Lazima tujifunze kutokana na yaliyopita. Miaka ya nyuma kulikuwa na mashirika mengi ya Umma. Upande wa nguo kulikuwa na Urafiki, MUTEX, MWATEX, KILTEX, kiwanda cha nyuzi Tabora, n.k. Morogoro kulikuwa na kiwanda cha MOPROCO kilichokuwa kikitengeneza mafuta ya kupikia; na kingine cha kufua ngozi, kilichokuwa kikitengeneza viatu, mikanda, mikoba ya wakina mama, n.k. Kwa kilimo kulikuwa na kiwanda cha UFI, kilichokuwa kikitengeneza zana za kilimo kwa mkulima mdogo mdogo; na TRAMA kilichokuwa kikitengeneza matrekta hapo barabara ya Nyerere. Kwa usafiri kulikuwa na kiwanda cha BORA kilichokuwa kikitengeneza viatu na matairi ya baiskeli; na SWALA kilichokuwa kikitengeneza baiskeli zenyewe kwa usafiri wa Mtanzania wa kawaida. Arusha kulikuwa na kiwaanda cha matairi ya magari cha General Tyre kwa usafiri wa ngazi ya juu zaidi. Kawe kulikuwa na kampuni ya kusindika nyama. Kampuni hii ilikuwa muhimu sana wakati wa vita vya Kagera kwani tayari walikuwa na uzoefu wa kuweka nyama kwenye makopo. Hivyo ikawa rahisi kwao kuongeza tu uzalishaji kwa ajili ya kupeleka bidhaa mstari wa mbele. Dar es Salaam kulikuwa na kampuni ya usafiri ikiitwa DMT; baadaye ikavunjwa na kuanzishwa kampuni tanzu mbili za UDA na KAMATA. Hali kadhalika, mikoani kulikuwa na makampuni ya usafiri karibu kila mkoa. Shirika la reli lilikuwa na kitengo cha mabasi yaliyokuwa yakienda pale hakuna reli. Baadhi ya vituo vikuu vya mabasi ya Relwe vilikuwa Mikumi, Itigi, Iringa, Mbamba Bay, Port Itungi na Chunya. Mtu unanunua tikiti ya Relwe ukiwa Iringa unakwenda Bukoba. Unapanda basi hapo Iringa mpaka Itigi au Dodoma; halafu unapanda treni hadi Mwanza ambapo unapanda meli mpaka Bukoba. Buguruni kulikuwa na National Milling iliyokuwa ikishughulika na nafaka. Tanga kulikuwa na kampuni ya mashati ya Gossage. Keko kulikuwa na kiwanda cha mablanketi na kingine cha kutengeza dawa za binadamu. Huko Tanga kulikuwa pia na kiwanda cha Steel Rolling Mills ambacho ni muhimu sana kwa viwanda nchini. TIPPER hapo Kivukoni ilikuwa ikisafisha mafuta na mali gafi ya usafishaji huo ilikuwa ikipelekwa Tanga kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea.
Ili mradi basi kulikuwa na kiwanda cha kushughulikia kila aina ya maslahi ya mwananchi. Hizo ndizo zilikuwa fikra za Mwalimu. Miaka ya tisini mashirika hayo yakaanza kubinafsishwa kwa hoja kwamba yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara. Swali rahisi ni kwamba iweje shirika la umma lipate hasara wakati kampuni binafsi inayofanya biashara hiyo hiyo inashamiri na kuendelea kudunda. Ilifikia mpaka shirika la Reli likauzwa kwa Wahindi ambao hawakudumu nalo kwa mda mrefu. Serikali ikagutuka na kulirudisha kwa Umma. Hata nyumba za serikali ziliuzwa katika mazingira tatanishi.
Muhimu ilikuwa kudadisi nini kiini cha hasara katika shirika na kutatua tatizo hilo. Kwa mfano, miaka ya 80 kulikuwa na uhaba mkubwa wa sigara. Ikafikia mtu anakaa barabarani na sigara yake, sawa na muuza machungwa. Mtu anapita na kuvuta mkupuo mmoja na kulipa shilingi moja au senti kadhaa. Halafu sigara anapewa mwingine. Biashara hiyo ikashamiri haswa. Kushughulikia uhaba huo wa sigara, Meneja mkuu wa Shirika wa wakati huo, Brown Ng'wilulupi, akasema 'I will flood the market'. Ndani ya wiki mbili sigara zikaenea mitaani. Hizi ndizo hatua muafaka wa kupambana na matatizo. Chunguza kiini cha tatizo halafu fanya ipasavyo. Uhaba wa sigara ulikuwa ni kutokana na upungufu wa vichungi vya sigara. Brown Ng'wilulupi akalishughulikia tatizo hilo na uhaba wa sigara ukaisha hadi leo hii.
Serikali ilibinafsisha Shirika la Reli kwa kuwa lilikuwa likiendeshwa kwa hasara. Wahindi wakashindwa kuliendesha na Serikali ikalitwaa tena.
Vivyo hivyo kwa TTCL. Kabla ya kulibinafsisha, hatuna budi kuchunguza kiini cha matatizo yake na kuona jinsi ya kushughulikia matatizo hayo. Historia tayari imetuonyesha kwamba suluhu ya matatizo ya kampuni za Umma si kubinafsisha. Kama kampuni binafsi zinaweza kufanya biashara hiyo, kwa nini Serikali shindwe?