Kabla ya kuvuja TTCL, Serikali ifanye haya kwanza...

naunga mkono hoja
 
Uzi upo humu tafuta Kuna bodi ya wakurugenzi vikaa tu walikula mil 600 mwaka Jana fautilia uone mama alimtoa mkurugenzi na wazee wengine kweny bodi
Kumtoa ndio adhabu?? Niibe bilion alafu unitoe kwenye nafasi yangu, hapo hasara ipo wapi?
 
Vipi na Yale magawio ya mashirika Kwa Serikali yameishia wapi ? Au yaliondoka na mwenye kuanzia!
Nchi hii ni ngumu sana!!
 
Si bure! We utakuwa na hang over ya ujamaa.
 
Du kumbe akili unazo
 
Nilipo ona Tangazo RUDI NYUMBANI KUMENOGA!; Nikafurahi!; ikawa TTCL NDIO MTANDAO WANGU PENDWA #.1!
Bando yangu PENDWA Kizalendo Zalendo ikawa BUFEE na JIACHIE!
TUSIACHE MBAÇHAO KWA MSAALA UPITAO!
Ukimsaidia mtoto wa jirani na kumtelekeza mwanao kwa sababu Yeyote, ujue mtoto wa jirani akifanikiwa atamsaidia babake...
 
Kosa moja haliachi mke!
Tuna vijana wengi wasomi na wazalendo wapewe shirika waliongoze!
Nchi hii hakuna uzalendo kila anayewekwa anaangalia pa kupiga. Sema tunatofautiana viwango vya aibu. Kuna wanaopiga 10% wengine wanapiga hadi 50%.
 
Mnufaika wa ttcl na hasara zake
 
Shida ya TTCL sio wafanyakazi walioajiriwa, ni uongozi hasa kutoka serikalini, TTCL ikiachiwa ijiendeshe yenyewe itafanya vizuri kwa kutumia wafanyakazi haohao ilionao.
 
TTCL iuzwe ili iweje na ili isaidie nini au imsaidie nani ?

Kwa taarifa yako kwa miundo mbinu tu na minara n.k. TTCL inaweza iziuze bundle wala simu na bado ikabreak even...

By the way hivi unajua nani anamiliki Halotel ? (Kwanini na sisi tusiwaze kupeleka TTCL hadi nchi za watu)

Unaongelea kuuza Shares unadhani masikini baada ya siku kadhaa hizo shares zake hataziuza au ndio kuchezeana Ponzi Scheme kwa mgongo wa shares....

Na vya kuuza vikishaisha then what ? ; Badala ya kufikiria ni vipi Kampuni kama hii inaweza kuwa industry pace setter na shamba darasa tunawaza mambo ya kuvunja (there is many ways to skin a cat); Na kama issue ni wezi magereza yamewekwa pale ili yawe mapambo ?
 
Nchi hii hakuna uzalendo kila anayewekwa anaangalia pa kupiga. Sema tunatofautiana viwango vya aibu. Kuna wanaopiga 10% wengine wanapiga hadi 50%.
Katiba Iseme mpigaji/mwizi wa mali ya Umma Apigwe Risasi Hadharani!
 
Kosa moja haliachi mke!
Tuna vijana wengi wasomi na wazalendo wapewe shirika waliongoze!
Naweza kuwa nafikiria vibaya ila naamini kama wewe. TTCL inahitaji damu changa yenye ubunifu unaoendana na mabadiliko na mahitaji ya sasa
 
Tatizo kubwa kwenye shirika la TTCL ni kwamba biashara wanayofanya ina ushindani mkubwa. Mengi ya haya mashirika hayatumii fedha nyingi kujitangaza na kukaba masoko muhimu. Wenzao kikao kimoja tu fedha inatolewa, jambo linafanyika, wenzao fedha inayopatikana kwenye kampuni inadhibitiwa na shirika husika.
Hawa wa serikali pesa yote tuna centralize kwa TRA. Tukihitaji huku kwa promotions na matangazo unapewa 20% ya ulichokiomba. Huwezi kushindana
Tuna dhana kwamba Vya serikali ni bora na havihitaji kutangazwa. Kwenye sekta uhifadhi na utalii ni hivyo hivyo, "watalii watakuja tu, hakuna Serengeti nyengine"
 
Haya mashirika yasiyotoa gawio na yanapayata ruzuku kutoka serikalini yapotezwe tu..naungana na Mh Rais
Mashirika hayo hayo, akichukua mtu binafsi utaona linaamka na baada ya muda mfupi linaanza kupata faida. Jiulize hapo
 
TTCL sio kwamba wako vibaya kihivyo. Hawategemei ruzuku hata senti moja toka serikalini. Kosa sio la wafanyakazi, kulikuwa na danadada nyingi mpaka tuliaminishiwa bungeni na Bazil Mramba kuwa Airtel ni kampuni Tanzu ya TTCL, hivyo TTCL mpamngo w kuanziza mobile service ukafa. Mnajua kilichotokea, TTCL imeingia kwenye soko la mobile katka mazingira magumu ya ushìndani ndio maana Mama nasema waachane na simu. Hata Halotel ana struggle mbona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…