Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Hata ukiwa na hiyo nyumba na gari hujamaliza. Nina nyumba na gari tangu nikiwa na miaka 27. Sasa nikaribia 31 lakini sina uhakika wa maisha na biashara zimekuwa zikienda vibaya sasa. Huwa napata stress nyingi pengine hata kuwazidi wasio na nyumba na gari.
 
Binafsi na kwa umri niliofikia pamoja na mapambano ya maisha naona kufanikiwa kwa kiwango kikubwa ni namna umeweza kuzitumia fursa au bahati ulizopata sasa apa inategemea mtu na mtu na bahati yake wengine bahati inakuja direct kabisa anapata nafasi flani nzuri au dili flani na linampa mafanikio ya pamoja ila wengine bahati inayokuja inakuhitaji juhudi kubwa sana ili utoboe. Lakini kufanikiwa Bila kudra au Bahati useme upambane n uongo.
 
Iyo nyumba na gari kuwa nayo by 30's sio issue..Issue ni una financial freedom na nyumba na gari ulivo navo ndio ulivokuwa unavitaka kwenye izo plans zako
 
Uko sahihi, ila hakunaga bahat au kudra tu inayokuja tu bila wewe kujihusisha kwa namna flan. Lazima uwe kwenye flow.
 
Upo sahihi ata ukiwa na talent lazima upate watu watakaiaminisha Jamii unatalent,upo sahihi kaka ila pia na maombi yanasaidia
 
Humu kila mtu siyo kijana(sio kijana aliezungumziwa na mtoa maada) kila member analeta story za ndugu na rafik

Labda nimuulize mtoa maada wewe kwako hali ikoje mkuu?
Mtoa mada alishasema ana umri wa 30s na hajaelewa bado na nuda unaenda maisha hajayapatia.
 
Mtoa mada alishasema ana umri wa 30s na hajaelewa bado na nuda unaenda maisha hajayapatia.
Maisha hayana formula kikubwa ni kupuyanga kulingana na upeo wako wa kufikiri na connection zingine

Kwa upande wangu mafanikio nayapima kulingana na malengo niloweka kwa kipindi husika mfano

1. Nilitaka nifike chuo- nimefika(nimefanikiwa)

2. Nilitaka niwe na biashara- ninayo(nimefanikiwa)

3. Nilitaka niwe na familia- nmeoa na mtoto juu

4. Nilitaka kujenga-najenga n.k

Kwahiyo ukiangalia kwa kiasi fulani nimefanikiwa japo kila nikifanikisha hili napanga lingine na hayo ndio maisha
 
Nime andika kwenye karatasi. Baadae nika vutie tumbaku.
👉Huenda vita niingia Ivan Stepanov
 
Uko sahihi Sana bro Eyce majuzi Kuna madogo want pata deal ya kusambaza sukari.
👉Imagine Wana pewa kwa Bei kitonga, ila wanavyo gonga people sio mchezo
 
Kaka nipeni laki 1, nawa choma na ma teacher kabisa😂😀
 
Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.
Sijui kwa watu wengine ila marafiki zangu wengi walioweza kufanya vizuri hadi chuo kikuu wengi zaidi hata ya 70% wana maisha mazuri kiuchumi. Vipanga karibu wote niliosoma nao wako njema. Na wale waliokuwa hawazingatii shule wengi wao hawako vizuri ni wachache waliobahatika kutoboa. Ingawa bahati zinahusika ila ni muhimu kupambana ili kama bahati itakuja ikukute uko tayari kwenda nayo sambamba. Kuna mdogo wangu alihitimu UDSM 2019 akakaa bila kazi hadi mwaka jana mwishoni bahati ya scholarship Ulaya ikamjia. Ile bahati ilikuja kwasababu dogo GPA yake ilikua safi na pia ni mtu mwenye nidhamu.
 
Semenya wa ukaldayo unashusha nondo za hatariii na kutema madini ya uhakika yaliyojitosheleza.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…