Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Barikiwa mkuu
 
Uko sahihi bro, watu sahihi- connection ndo mtaji tosha.
👉Deal la sukari, hali wezi mfikia muuza bhangi wa kijiweni 😀
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji117] 1.RIGHT TIME, 2.RIGHT PLACE, 3.RIGHT PEOPLE, 4.READINESSP = FORTUNE (BAHATI).

kuna hii mentality ya kipumbavu kumsingizia Mungu kuwa ndiye anayepanga maisha ya watu yawe vipi, huu ni uongo na uzushi wa kijinga uliozushwa na wavivu walioshindwa kufanya kazi kwa kutegemea bahati ya Mungu.

Bahati ni neno zito ambalo haliji hivi hivi wala kumtokea mtu hivi hivi bali kuna factors zinazopelekea mtu akutane na hii bahati.

Unaweza kushinda ndani hufanyi kazi yoyote lakini ghafra ikakujia akili ya kubeti ukabeti na ukala hela ndefu ambayo kama ungefanya kazi usingeipata, hii tunaita bahati iliyotokea kwa muda sahihi uliobeti(right time) eneo sahihi(right place) kama ungelikuwa sehemu ya kukukeep bize huenda usingewaza hivi au usingefanya hivyo, na utayari wa kulifanya hilo jambo(readiness) hapa ndipo unaunda neno BAHATI.

Pia unaweza kuwa mkulima unayelima miaka na miaka lkn hufanikiwi, lkn ukakutana na madalali wanaokushauri ulime mazao fulani ama utunze mazao yako mpaka kipindi fulani ama ukusanye mazao fulan na uyafanyie biashara,

Kitendo cha kukutana na hawa madalali tunaita( RIGHT PEOPLE) muda uliokutana nao(RIGHT TIME), mahala ulipokutana nao(RIGHT PLACE) na ule utayari wako wa kuyafanyia kazi yale waliyokushauri ndie tutaita (READINESS) na matokeo ya utakachokipa ya hivi vitu vinne ndio tunaita Bahati, na kweli unakuta ukiyafanyia kazi mawazo yao unafanikiwa pakubwa zaidi ya hapo mwanzo, hii ndio bahati ilivyo na inavyokua, hapa wala hapahitaji uwepo wa Nguvu ya Mungu wala visingizio vya kitu fulani.

Uzembe wa kutumia akili ndio unawafanya watu waanze kumsingizia Mungu ndie mpangaji wa mambo, kwamba Mungu anapanga nani afanikiwe na nan asifanikiwe huu ni ushenzi na uongo wa hali ya juu uliotungwa na wahuni wa kidini ili kuwapa moyo wapumbavu wasiopenda kufanya kazi zaidi ya kusubiri miujiza ya kijinga.

Unapozaliwa tu jukumu la mafanikio by 80% ni lako wewe mwenyewe na 15% wazazi/walezi/watu wa kawaida na 5% ndio hiyo Bahati ambayo nayo huja mara chache sana na ikija huwa haiulizi uko mahala gani ni wewe tu kuwa tayari kuikumbatia hiyo bahati na ikija huwa inayabadiri maisha yako kabisa haijalishi ulikuwa ktk hali gani ya maisha, bahati ina asilimia chache sana ya kumpata mwanadamu/mtu ndiomaana kuna wengine huforce kupata bahati kupitia ushirikina na unajimu.

Maisha yamejawa usiri mwingi ambao waliofanikiwa tu ndio wanajua nini maana ya mafanikio, kuna njia nyingi za kujiweka karibu na mafanikio ambazo njia hizi nyingi waafrika haswa waTanzania tunazikwepa kwa sababu ya Uvivu wa kujifunza mambo mapya, uvivu wa kusoma vitabu&maandiko sensitive mitandaoni, Uvivu wa kuthubutu, ujinga na upumbavu wa kutegemea miujiza na bahati nasibu.

Ili uwe sehemu ya kuwa na bahati [emoji117]kwanza unatakiwa uwe mtu wa kuthubutu yale ambayo wengine wanayaogopa kufanya,
[emoji117]uwe na bidii ya kitu unachokifanya, kuwa smart tumia akili sana zaidi ya kutumia nguvu, ikiwezekana inoe akili yako haswa ifikili zaidi kuhusu ilo jambo unalofanya,
[emoji117]kuwa tayari kwa matokoeo na mabadiriko ya ukifanyacho, [emoji117]kuwa mjanja wa kucheza na fursa kwa muda sahihi na watu sahihi wa kitu ukifanyacho, hakikisha unachokifanya matokeo yake yamezungukwa na watu ambao kwako ni faida, yaani rasilimali watu.

La mwisho utayari, kuna watu wengi hata humu hukosa mishe na madeal ya maana kisa ujinga wao na uvivu wa kusuasua kuchukua hatua ya kushughulika na hilo jambo, muda unaopoteza kufanya maamuzi ndio hiyo bahati inakupita na kwa bahati mbaya, BAHATI inapokujia huja kwa upole sana, haikubembelezi, haikufokei, wala haikulazimishi, bali hukupa Uhuru wa kuamua kuifuata ama uendelee kuteseka na unachokifanya.

Bahati ikikupita imekupita, labda wewe mwenyewe uwe mtu wa Bahati yaan namaanisha kuna watu Bahati kwao ni kama kaka na dada, ikimpita leo, kesho inarudi, la msingi tuwe tayari kwa kuchukua hatua kwa kila fursa inayojitokeza mbele yetu, habari za kusema subiri sijui uombe ushauri, mtaendelea kuwasindikiza wenzenu katika UTAJIRI mpaka lini?

Tuamke jamani.
 
Hakunaga kitu kinaitwa roadmap wala nini huu ni uzushi mtupu, mnayatoa wapi haya mauzushi? Mbona kwenye masimulizi yenu ya biblia hayapo?

Je Mungu ndie hupanga mtu afanye uzinzi ili kiumbe fulani atokee ili hayo makusudi na mipango yake itimie? Yaani zinaa aliyoikataza Mungu aje aibariki kisa kutimiza mipango yake?

Kama ni hivyo basi hata zinaa sio dhambi maana inatimiza mipango ya Mungu ya kuwaleta wanadamu ambao wanafuata hiyo roadmap ya Mungu, alafu pia Huyo Mungu atakua anajichanganya mwenyewe maana ktk amri zake 10 kakataza baadhi ya mambo ambayo ndio hayo hayo yanapelekea hiyo roadmap kutimia, sasa kwanini mumsingizie Mungu?

Ukweli ni kwamba Muumba hana Muda wala hahusiki na kuzaliwa kwako maana alishaweka Misingi na sheria hapa duniani katika UUMBAJI WA KWANZA KUWA kushiriki ngono kati ya mwanaume na mwanamke haijarishi ni wanandoa ama wahuni au wanacheat hapo lazima mimba ibebwe tu na kiumbe kizaliwe no matter what, na kiumbe hiki kikizaliwa hakina utofauti na viumbe wengine waliozaliwa kupitia wazazi walioshiriki tendo la ngono ktk ndoa.

Pili kiumbe hiki kama kitafuata misingi na sheria za ulimwengu za mafanikio kulingana na eneo lake hiki kiumbe ni lazima kifanikiwe haijarishi kinamuabudu huyo Muumba, haijarishi kilizaliwa kwa ndoa ipi au kwa mzazi wake kubakwa au uzazi wa kupandikizwa, kitendo tu cha kuzaliwa tayari unakuwa chini ya sheria fulani ambazo ukizifuata lazima ufanikiwe, na sheria hizi wala hazihusu hiyo roadmap yenu mnayo lazimisha kusema Mungu kamuandikia kila mtu mafanikio fulani, Upuuzi mkubwa huo.

Sheria za mafanikio siku zote ni [emoji117]kufanya kazi kwa akili then kwa bidii, kufanya kazi inayoendana na utashi wako, ufahamu wako na Utu wako(talent/kipawa/kipaji), [emoji117]kufanya kazi au shughuri sahihi ktk sehemu sahihi na bidhaa sahihi mwisho kuzungukwa na watu sahihi ktk muda sahihi na hii ndio SIRI ya mafanikio kwa kwa viumbe wote haijarishi hawa viumbe wanafuata au hawafuati hizo ngonjera za kipuuzi za kidini, mafanikio hayamchagui mtu.

Mwisho, Tuache kujipa moyo na visingizio vya kijinga eti mafanikio yanaletwa kwa kusali sijui kumtegemea Mungu, huo ni uongo, kama huwezi kutumia akili ulizopewa bure basi subiri watu wakusaidie kuzitumia hizo akili zako kwa kukufanya mtumwa wao wa kuwatajirisha na kuwasindikiza ktk mafanikio,

Wafia dini amkeni na Mtumie akili badala ya hisia na upumbavu.
 
Unakua umefanikiwa kwenye nini sasa?
Kama ni mafanikio ya kiuchumi ambayo ndio yanazungumziwa hapa, huwezi kupanda public transport has a kwa Dar (daladala/mwendokasi Dar ni laana) huo ni uongo.

It's either bado unajitafuta au hizo hela ni za masharti, period.
 
Kama wahindi wanakaa kwenye apartment nzuri zenye AC Ila wanamiliki cash flow za wao kuwawezesha kula hadi na wajukuu.
Huku ni kujipa moyo.

Ukiwa na kipato cha kukaa kwenye apartments kama za hao wahindi tayari we una kipato cha maana, suala la kujenga ni maamuzi..sio umepanga nyumba hizi za kodi chini ya laki 2 nyumba nzima (wengine kodi inasumbua) ujilinganishe na wahindi.
 
I feel to cry kwenye huu uzi wallah😪😪😪
 
Your very true, kwa mfano mimi nikitaka tuu kujiendeleza na elimu kama kazi ntapoteza kama biashara itakufa yaani hii napambana nayo zaidi ya miaka kumi inanisumbua.
Now maisha yangu nimeamua yawe autopilot coz nimekutana na fursa nyingi mno local na International lakini hamna hata moja zimenifikisha walau nusu au robo ya ndoto zangu nimebaki kusifiwa tuu nina akili ila sina bahati.

Inauma inauma saana aiseeh
 
Pia waswahili vijicho vingi hata ukimpata wakukushika watakuroga tuu labda uame mkoa
 
Sikua mzinzi na sikutoboa na kuna wazinzi wengi wametoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…