Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Pole mkuu naelewa sometimes inauma sana pale unapokuwa na potential kubwa lakini haikufikishi unapopataka zaidi ya kupewa empty praises. Mungu afanye, take off yako iwezekane lakini pia kama, utaweza ni vyema kuongea na watu waliofanikiwa maana kama kuna kitu kinasumbua watu ambao wana akili sana ni kufuata certain patterns or formalities. Hopeful bro Ivan Stepanov ataongezea
 
Jamaa unanielewa saana nakushukuru
 
That's is life.... sometimes life give you what you didn't expect
 
Siyo sahihi kuaminisha watu kwamba wanaofanikiwa ni wale wa Mungu tu

Wakati na bahati huwapata wote

Na kuna maelfu ya walokole ni Masikini wa kutupwa

Kufanikiwa ni jitihada na bahati
Maandiko yanasema Mungu ndo humpa mtu nguvu za kupata utajiri...Na kuzielekeza hatua zake haimo katika uwezo wa mwanadamu
 
Nakubaliana na wewe, wote ambao tumefanikiwa kufika chuo kikuu tuko vizuri ulilinganisha na wale walioishia kidato cha tano. Wengi sasa hivi ni senior kwenye taasisi mbalimbali au wana mashirika yao. Elimu, connection vinasaidia sana kumvusha mtu.
 
Niongezee tu na kuna kundi kubwa la vijana ulaya ambao ni wa ovyo ufuska na ujinga wote wanafanya wao ila wengi wao uishia kuwa na maisha mazuri sana sababu ni mfumo wa serikali zao unawawezesha kabisa..

Huku kwetu Sera mbovu, siasa uchwara, mazingira ya rushwa, ujinga, elimu mbovu, serikali za hovyo ndio chanzo cha umaskini na ukosefu wa fursa kwa vijana wengi hasa barani Afrika.
 
Nakubaliana na wewe, wote ambao tumefanikiwa kufika chuo kikuu tuko vizuri ulilinganisha na wale walioishia kidato cha tano. Wengi sasa hivi ni senior kwenye taasisi mbalimbali au wana mashirika yao. Elimu, connection vinasaidia sana kumvusha mtu.
Ni kweli. Watu huwa wanajipa moyo kipuuzi sana. Kwamba ambao hawakusoma huwa wanakuja mabosi wa wasomi. Sasa hivi hata huku kwenye biashara wanaokimbiza ni wasomi na kama sio msomi utakuta ni University drop out.
 
Baraka ya Bwana hutajirisha,bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndie akupae nguvu za kupata utajiri.

Siri ipo hapo.
 
Hivyo vitu vya ghafla ni very rarely ila nathibitisha kabisa connection na mifumo mizuri ndio chachu ya maendelea kwa watu ndio maana kwa Tanzania vijana wengi wanaomba wapate kazi serikaliji huko kuna mfumo mzuri kwa watumishi hivyo walau kuleta unafuu wa maisha..
 
Maandiko yanasema Mungu ndo humpa mtu nguvu za kupata utajiri...Na kuzielekeza hatua zake haimo katika uwezo wa mwanadamu
Maandiko hayo ni hadithi za kutungwa sawa na Hekaya za Abunuwasi.

Maandiko hayo ni fiction stories hazina ukweli wala uhalisia wowote.

Ndio maana ume ambiwa hapo kuna walokole wengi wanajua hayo maandiko lakini kiuchumi ni maskini choka mbaya Höhehahe pangu pakavu tia mchuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…