Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Baraka ya Bwana hutajirisha,bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndie akupae nguvu za kupata utajiri.

Siri ipo hapo.
Unaweza hata kumiliki private jet?

Siri si unayo?

Muombe huyo bwana mungu umiliki private jet kama utaweza...πŸ˜„πŸ˜„

Sio kuongea ongea maandiko uchwara ya kufikirika tu.
 
Unaweza hata kumiliki private jet?

Siri si unayo?

Muombe huyo bwana mungu umiliki private jet kama utaweza...πŸ˜„πŸ˜„

Sio kuongea ongea maandiko uchwara ya kufikirika tu.
Yaani ushinde kanisani au msikitini bila mipango upate private jet ya burebure? Hiyo hajawahi kutokea. Tumepewa utashi na maarifa tuyatumie. Simba hawezi kula bila kuua, anatumia utashi wake kupata mlo otherwise atakufa.
 
Sasa hapo usije ukawachanganya watu wakahisi na mimi ni miongoni mwa watu waliofanikiwa kumbe nimefanikiwa kifikra tu kitu kilichonisukuma kufanya maamuzi magumu yaliyo nigharimu but now atleast naweza ona mwanga japo mifuko imetoboka.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
 
watu wa dini hii hapa ndipo pana wakawamisha sana.
You have bunch of keys, but u know nothing on how to use them, where the locks are to apply your keys so u keep applying the smart keys on wrong locks and nothing opens
Tena ni wengi, kwenye masuala ya akili timamu.
πŸ‘‰Wao Wana kuambia uta chomekaπŸ˜‚πŸ˜€
 
nilichojifunza mpka sasa ni kutomuonea mtu wivu..... unaweza ona wivu kwa mtu ulietakiwa kumuonea huruma....


nina jamaa yangu tulimaliza wote 4 akadunda maisha yakaendelea... miaka ya 2012 alikuja kufumuka mkwanja mrefu ndinga kali kawahamisha wazazi wake kawapeleka shamba kaporomosha mjengo wakae wasimamie mashamba..... sikujua chanzo cha kipato ila alikua akikutana na mimi stor zake ni pesa tu na sikuwahi hoji umetoboaje.
mwaka 2014 hivi akavuta benz ya maana 2016 nikakutana na jamaa yangu mwingine katika stor za hapa na pale akanidokeza jamaa yetu alikua mzee wa madawa akadakwa dubai ndio ikawa mwisho wake jinsi jamaa alivyokua ananipa stor nilihisi mwili kusisimka niliogopa sana ndio nikaanza kuunga matukio nikajifunza kutoona wivu ningejiskia vibaya jamaa kunipita mafanikio wakati sijui chanzo cha mapatonyake ni ujinga..

sijawahi muona jamaa yangu mpka leo naambiwa hajachomoka na wazazi wameshafarakana hakuna kilichosimama tena toka adakwe.... maisha hayako kirahisi ila tujifunze kupambana na kuamini kile kinachoweza kukupa faida hata kama ni ndogo ila uwe na amani.

leo nipo na familia yangu ila jamaa yangu yupo na familia ya wafungwa inaumiza sana ukifikiri
 
Easy Money High Risk Money......huyo jamaa itakuwa hakuwa na Kadi na hafahamiani na makada
 
Well
 
Mkuu ukikutana na Kada kashapata Mchongo mambo yake ya gizani yanameendea vizuri basi sisi wengine anatuona tupo tupo tu tunaishi bila mipango
 
Acha wogaπŸ˜‚πŸ˜‚
siogopi ila kwenye maisha kuna machaguo na mimi nilichagua amani zaidi kuliko kipato kikubwa kitakachoniweka roho juu.
mfano leo narudi home naona wanangu naweza saidia familia yangu naishi wa watu kwa uhuru hii kwangu ni amani na furaha kuliko kuwa na biashara haramu zitakazoniondoa mbele ya uso wa familia yangu.

hakuna kitu kinaumiza kama kuona familia inabaki haina baba kisa ulishindwa kuangalia fursa halali jela ipo kwa kila mtu ila nimejiapiza nitaingia kwa makosa ya kibinadamu kama kusingiziwa ila sio kwa pusha nikatishe furaha ya wanangu
 
Basi wewe utajiri utausikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…