Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Je, unaijua kesho yako itakuaje ?..

Je, unaweza kuamua kesho utakutana na nani au lipi ?...

Kama nikikurudisha 5 years back, je hapo ulipo ndipo ulipotaka kuwa kwa kitu ukifanyacho na kwa level uliyoifikia ?..

What I know, binadamu tuna control mchakato tu ili tuweze influence results ila hatuna UBAVU wa kutengeneza matokeo vile tunavyotaka sisi na kama ingekuwa hivyo, bhasi zaidi ya 80% ya biashara za Tanzania zisingekufa kabla ya kufikisha miaka 5 maana sidhani kama kuna mtu anaeanzisha biashara ili ife...

One thing nachoweza kukubaliana nawe ni kuwa kila kinachotokea mara nyingi hutokana na maamuzi tunayofanya ila sababu za kupelekea kufanya uamuzi fulani, kuna zile tunazoweza kuzicontrol na zile tusizoweza

Personally, huwa naamini sana katika jitihada sana na strategy za kufanya mambo lakini huwa sipuuzi uwepo wa circumstances ambazo zipo nje ya uwezo wangu, japo sizipi uzito sana ili nibaki persistent

Marais wote nchi yetu hawakutegemea kama wangekuwa marais. Na wale waliokuwa na uhakika wa kuwa Rais hawakuwa.
Maisha sio mchezo
 
Habari za jumapili!

Maisha sio Pouwa! Nakubaliana na wale wanaosema Maisha ni majaliwa. Na jitihada hazizidi kudura.
Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.

Ilifika hatua wakawa wanadharau wale ambao walikuwa wanaonekana hawana mipango na mikakati kutokana na kutoipenda shule.

Wengi walifikiri kuwa kabla ya miaka 30 tayari wangekuwa wamekomesha jeuri na kiburi cha Umaskini katika maisha yao.
Tayari kichwani walikuwa na picha za jumba kubwa la kifahari ambalo walijua ndio watakayoishi. Bongo zao zilishakuwa na miundombinu ya flyover ambapo gari yao ilikuwa ikipita juu yake huku ndani akiwa yeye na Pisikali moja matata ambayo ndio mkewe.

Kwa wasichana, wao nao walikuwa na maisha yao mazuri katika vichwa vyao. Wanaume Handsome, warefu na wenye vipato na Watanashati walikuwa katika fikra zao.

Sasa miaka imekimbia, hawaelewi nini kimetokea. Matumaini yameyoyoma, ngumi ya matumpa upper cut moja matata imepiga kidevu vijana chali.
Hata zile ramani za majengo na magari walizokuwa nazo miaka hiyo zimefutika.

Yule Mwanamke mrembo akilini waliyemfikiria wangekuja kumuoa wanawaona kwenye magazeti, filamu na kwenye riwaya. Hakuna faraja tena, tumaini limeota mbawa. Wamejiunga kwenye chama cha faraja ya mpito cha Kataa Ndoa.
Hawakumbiki tena ndoto ya kuwa na familia bora baada ya kuyapata maisha mazuri yanayotamanika.
Ni Tekniko Knockout.

Hawakujua kuwa maisha yanakupa yale ambayo hujayaomba na yale ambayo huyataki. Tena maisha hukupa yale ambayo hukudhania kwamba ungekuwa nayo. Kwa sababu maisha ni Nasibu, maisha ni bahati tuu.

Sasa mipango imevurugwa na kuvurugika. Kila kitu pangala pangala! Hata kupanga hawataki kupanga tena. Hata wakisema wapange wanaona wanapoteza muda wao. Sasa ni bora liende túu! Wapo tayari kwa lolote na huo ndio mfumo wa maisha unavyotaka.

Mtu ambaye alipanga kabla ya miaka 30 awe na jumba na gari leo hii hata kodi ya chumba cha laki moja hawezi kuhimili. Unaweza kuona pigo alilopigwa ni zito kwa kiwango kipi.

Kijana, unapopanga mipango yako. Muombe Mungu

Acha Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kukata tamaa ni mwiko tutatoboa tuuu
 
Kukata tamaa ni mwiko tutatoboa tuuu

Kuna ambao walikata tamaa lakini Dakika za mwisho wakatoboa wakiwa katika state hiyohiyo ya kukata tamaa.

Na waliokuwa na moyo mkuu usiokataa tamaa mpaka mwisho lakini wakashindwa kutoboa. Walikufa wakiwa hawaamini kama ngoma imelala wakiwa wamepigwa.


Mungu ndiye mwamuzi wa yote. Huna lolote utakalofanya kwa uwezo wako. Unaweza ukawa strong ukashindwa na aliyedhaifu
 
Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Kujenga nyumba na kununua gari ni hayo matokeo mafanikio ni kufikia lengo katika kazi au biashara unayofanya imekuwa kwa kiasi gani kuna watu wamefanya investment kubwa lakini wanaishi nyumba za kupanga

Kitu kingine vijana wana give up mapema sababu wanataka matokeo makubwa kwa haraka bila kuelewa kabla haujafanikiwa kuna indicator huwa zinakuonesha jambo unalolifanya linaenda kukupa matokeo makubwa haijalishi upo chini au kati kuna muda unahitaji subira
Tanzania, kwa maoni ya wengi, kujenga nyumba na kununua gari ndiyo kilele cha mafanikio. Kwangu nini sidhani kama tuko sahihi. Unaweza kuwa unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unatumia usafiri wa public lakini ukawa na mafanikio kuliko mtu mwenye nyumba na gari.
 
Tanzania, kwa maoni ya wengi, kujenga nyumba na kununua gari ndiyo kilele cha mafanikio. Kwangu nini sidhani kama tuko sahihi. Unaweza kuwa unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unatumia usafiri wa public lakini ukawa na mafanikio kuliko mtu mwenye nyumba na gari.
Hata Ulaya kujenga nyumba yako nzuri na kumiliki gari ni mafanikio Mkuu.

Mafanikio ni mafanikio popote. Uwe Ulaya, Asia au Afrika
 
Nskumbuka Jamaa mmoja shule nilimuuliza vipi milioni 80 unapiga kalamu chini na kuacha shule akasema hata milioni 100 hawezi kuufanya huo ujinga.
Jamaa kweli kapiga one Form four na six kapiga one pia kasoma UDSM ila sasa maisha yanamkimbiza kama alivyokuwa anayakimbiza masomo.
🤣🤣🤣🤣


Mil 100 ni hela ndogo Sana huwezi kuacha masomo Kama form four au six maana Kwa nchi zetu wengi Elimu ndo umetufanya tuone Mwanga so the guy Was Right.
 
Kuna ambao walikata tamaa lakini Dakika za mwisho wakatoboa wakiwa katika state hiyohiyo ya kukata tamaa.

Na waliokuwa na moyo mkuu usiokataa tamaa mpaka mwisho lakini wakashindwa kutoboa. Walikufa wakiwa hawaamini kama ngoma imelala wakiwa wamepigwa.


Mungu ndiye mwamuzi wa yote. Huna lolote utakalofanya kwa uwezo wako. Unaweza ukawa strong ukashindwa na aliyedhaifu
Jitihada bila Mungu ni bureee na Mungu ni mwamuzi wa yote lakini bado bila jitihada za dhati ni BURE pia.
 
Hata Ulaya kujenga nyumba yako nzuri na kumiliki gari ni mafanikio Mkuu.

Mafanikio ni mafanikio popote. Uwe Ulaya, Asia au Afrika
Nyumba na gari Mimi naona ni mahitaji ya muhimu Ila sio mafanikio. Mimi nayatazama mafanikio yangu ninapokuwa na uwezo wa kuwafanya watu wengine wapate Mahitaji yao kupitia mimi
 
Jitihada bila Mungu ni bureee na Mungu ni mwamuzi wa yote lakini bado bila jitihada za dhati ni BURE pia.

Mungu ndio hukupa hiyo roho ya jitihada ili akupe bahati yako.
Unafikiri spirit ya mtu kufanya kazi inatoka wapi?
Lakini pia mtu asipokuwa na ari ya kufanya kazi Unafikiri hiyo inatokana na nini?

Unaposema Mungu unamaanisha chanzo cha yote uyajuayo na yale usiyoyajua. Yawe mazuri au Mabaya. Yeye ndiye mbunifu, mtunzi na muimbaji wa kila kitu.
 
Bila jitihada ni uongo japo sio lazima ,unapofanya kazi kwa bidii basi unajiwekea nafasi zaidi ya Kufanikiwa.

Mafanikio bila ya jitihada ni ushirikina japo zali la mental lipo ,ila nafasi yake ni ndogo sana ...Pambana leo ukifika kileleni unapumzika huku maisha yanaenda safi.

Nini chanzo cha jitihada kwa mtu?
Nini chanzo cha msukumo wa jitihada kwati kufanya jambo fulani alafu mwingine akakosa huo msukumo?

Mimi naamini kila jambo Mungu ndiye mratibu na mshukiwa namba moja. Alfajiri na omega. Mweza wa yote mazuri au Mabaya, makubwa au madogo.

Ukishakuwa na attitude kuwa Mungu ni wamazuri pekee hapo ndio mwanzo wa kutojua maisha ni nini.
Mungu ni wa yote. Mazuri na mabaya.
 
Back
Top Bottom