Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Tanzania, kwa maoni ya wengi, kujenga nyumba na kununua gari ndiyo kilele cha mafanikio. Kwangu nini sidhani kama tuko sahihi. Unaweza kuwa unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unatumia usafiri wa public lakini ukawa na mafanikio kuliko mtu mwenye nyumba na gari.
Wachache sana watakuelewa. Maisha mazuri yanaumbwa na pesa inayozunguka mfukoni na mikononi mwako (cash flow). Siyo liabilities kama nyumba ya kulala na gari ya kutembelea.
 
Sikubaliani na hoja kuwa mipango ya kimaisha ya vijana wengi inaharibika kwasabb hawamhusishi ama hawamuombi Mungu. Wapo walokole ama mashekhe promax wamefika 50 bado hawana hata kitanda.

Kila mtu ana FATE yake, yaani Kila mtu kachorewa roadmap ya maisha yake na mwenyezi Mungu. Ndiyo maana akina Laizer wanaokota tanzanite yenye thamani ya mabilioni wakati wengine hata mia mbovu hamuokoti.
Anachomaanisha mleta mada pamoja na jitihada zetu tumuweke sana mungu mbele
 
Kiukweli kabisa sijawahi kuwa na fikra za mbele na za ukubwa huo.

Siku zotee naamini mbele yangu siijui, kwasababu mipango, matamanio, na mategemeo havina mkataba na uhalisia katika maisha.

Watu wengi wanajenga nyumba kwa kujibana na kuishi kwa taaabu muda mrefu, ni bora kuwa mpangaji wa muda mrefu mwenye akili ya uwekezaji kuliko mwenye nyumba anayeishi kwa msoto mkali wa kulipa mikopo kisa kulinda ufahari wa kumiliki nyumba 😂😂
Nimekupenda bure

Mimi sipendekezi watu waishi nyumba za kupanga, bali watu wajenge nyumba ndogo za uwezo na mahitaji yao halisi siyo kujenga jumba kubwa kwa ajili ya ufahali tu

Bora kujenga hata chumba na sebule lakini utakuwa kwako na amani ya kutosha

Shida ya kupanga ni kuwa biashara hazieleweki kuna wakati utakuja kuishiwa hela ya kulipa kodi utajuta sana
 
Kuna mambo yananitokea physically afu unayarelate mbona kama nilishawahi kuyaona!
Ilishawahi kukutokea hii?
Mi hunitokea mara nyingi tu. Na ndio nazidi kuamini kua haya yanayotutokea yalishaandikwa.


Hamna ni saikolojia tu don't play average you have something to offer no body else has .

Don't take ur life for granted uta-achieve a lot
 
Sikubaliani na hoja kuwa mipango ya kimaisha ya vijana wengi inaharibika kwasabb hawamhusishi ama hawamuombi Mungu. Wapo walokole ama mashekhe promax wamefika 50 bado hawana hata kitanda.

Kila mtu ana FATE yake, yaani Kila mtu kachorewa roadmap ya maisha yake na mwenyezi Mungu. Ndiyo maana akina Laizer wanaokota tanzanite yenye thamani ya mabilioni wakati wengine hata mia mbovu hamuokoti.
si kwamba mpagani hana Mungu, na wapo wapagani waliofanikiwa. Ipo nguvu ya asili (Supreme power) iliyolela viumbe vyote duniani)
 
Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Kujenga nyumba na kununua gari ni hayo matokeo mafanikio ni kufikia lengo katika kazi au biashara unayofanya imekuwa kwa kiasi gani kuna watu wamefanya investment kubwa lakini wanaishi nyumba za kupanga

Kitu kingine vijana wana give up mapema sababu wanataka matokeo makubwa kwa haraka bila kuelewa kabla haujafanikiwa kuna indicator huwa zinakuonesha jambo unalolifanya linaenda kukupa matokeo makubwa haijalishi upo chini au kati kuna muda unahitaji subira
point to note
 
Siyo sahihi kuaminisha watu kwamba wanaofanikiwa ni wale wa Mungu tu

Wakati na bahati huwapata wote

Na kuna maelfu ya walokole ni Masikini wa kutupwa

Kufanikiwa ni jitihada na bahati
Hakuna relationship ya Iman na mafanikio.
Mafanikio ayapatayo mtu ni teyari alishapewagwa na muumba wake hata kabla hajaletwa duniani.
Hizi hustle tunazofanya ni asbabi tu.
Ila mambo tunayopitia yalishaandikwa kabla.
 
Nskumbuka Jamaa mmoja shule nilimuuliza vipi milioni 80 unapiga kalamu chini na kuacha shule akasema hata milioni 100 hawezi kuufanya huo ujinga.
Jamaa kweli kapiga one Form four na six kapiga one pia kasoma UDSM ila sasa maisha yanamkimbiza kama alivyokuwa anayakimbiza masomo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Maisha hayana formula hapa bongo kwasbb ya uhovyo hovyo. Aliyesoma sana nafasi yake inazibwa na kilaza mwenye godfather, mkulima bora anadhullumiwa na dalali, mfanyabiashara anayepambana anakwamishwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi, mwenye kipaji cha mchezo wowote anapoteza kipaji chake kwa kuwa hana godfather.

Tukiacha uhovyo hovyo tukajeshimu mifumo na taratibu, mambo yatatunyookea.
Ni kweli mkuu, mfumo ukinyooka hali itakuwa vizuri zaidi ila japo hata huko kwenye mifumo iliyonyooka, wapo watu wanaoamua nani apate na nani akose
 
Siyo kila utajiri ni mafanikio. Mafanikio ni utimilifu wa furaha. Je, hujawahi kuona tajiri ambaye hana furaha?
PESA inasadia katika kuwa na furaha

Maana ubapokuwa hauna PESA unakuwa hauwezi kuishi katika life path yako unakuwa MTU Wa kushika kila kitu ili mkono uende mahala pake.


Furaha inachangiwa kwa kiasi kikubwa ukiwa na PESA.
 
Siyo kila utajiri ni mafanikio. Mafanikio ni utimilifu wa furaha. Je, hujawahi kuona tajiri ambaye hana furaha?
Furaha haitafutwi, furaha haitokani na matokeo yoyote

Huhitaji hela au mali au kitu kingine chochote ili kuwa na furaha

Furaha haihitaji funguo sababu haijafungwa popote na kufuli

Furaha unayo tayari ndani yako, ni maamuzi yako kuwa na furaha na Huhitaji kuwa tajiri ili kuwa na furaha
 
Kuwa Mlokole au mwenye haki hakukufanyi ufanikiwe.
Unafanikiwa kwa sababu Mungu ndiye ameamua ufanikiwe.
Waliofanikiwa wengi wao wanakiri kuwa hawakutegemea kama wangefanikiwa. Yaani wanaita ni bahati.

Wengi wanaofeli wanafeli kwa sababu wanaamini katika uwezo wao wenyewe.

Tafuta waliofanikiwa wote wanafanana katika jambo moja. Kuamini kuwa mafanikio ni majaliwa ya Mungu
Nakubali Kuna Jamaa yangu katoka tak home ya 7.2Mil per year, akafukuzwa kazi akapata kazi ya take home 4.8 per year, now kaenda take home ya 30Mil per year, na huu mlolongo umetokea ndani ya miezi 5 iliyopita, na nikimuuliza anasema ni Mungu tu, ye mwenyewe haelewi amefikaje fikaje alipo, maana baada yakufukuzwa kazi ya 7.2 mil per year alihisi kukata tamaa, lkn baada yahapo kafanya interview 3 ndani ya miez 4 nazote katoboa. Nakipindi Cha nyuma kahudhuria interview kibao lkn bila mafanikio.
 
Hakuna relationship ya Iman na mafanikio.
Mafanikio ayapatayo mtu ni teyari alishapewagwa na muumba wake hata kabla hajaletwa duniani.
Hizi hustle tunazofanya ni asbabi tu.
Ila mambo tunayopitia yalishaandikwa kabla.
Ndo maana huwezi muomba Mungu akakupa utajiri au Mungu hawezi kukubariki sababu tu ni mkristo, Mungu anabariki watu wote hata ambao ni wapagani na hii ni kuonyesha anapenda binadamu wote
 
Huwezi kubali ila kuna siku uliiponda biblia kwamba ina miungu wengi
Ila mwamba wewe ni bingwa wa kubadilika kama kinyonga

Kipindi cha nyuma ulikua mtoto sahivi umekua

Kuiponda Biblia au Quran au kitabu chochote cha kidini sio kumponda Mungu.

Mkuu tunakua kwa sasa uzee umegonga hodi.
 
Back
Top Bottom