Wachache sana watakuelewa. Maisha mazuri yanaumbwa na pesa inayozunguka mfukoni na mikononi mwako (cash flow). Siyo liabilities kama nyumba ya kulala na gari ya kutembelea.Tanzania, kwa maoni ya wengi, kujenga nyumba na kununua gari ndiyo kilele cha mafanikio. Kwangu nini sidhani kama tuko sahihi. Unaweza kuwa unaishi kwenye nyumba ya kupanga na unatumia usafiri wa public lakini ukawa na mafanikio kuliko mtu mwenye nyumba na gari.